Vitabu vinauzwa

Vitabu vinauzwa

clion dismas

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
185
Reaction score
169
Wanabodi
Heri na mwaka mpya
Ninawaletea vitabu 3, cha kwanza "MUNGU NA UPONYAJI KATIKA MATUNDA , NAFAKA NA MBOGAMBOGA", " USALAMA KATIKA MIFUMO YA UMEME" na " MAISHA YA CHUO".
Vitabu hivyo 3 vimeandikwa nami Clion odhiambo Dismas na kwa ufupi kabisa nitaelezea kimoja baada ya kingine.
1.Mungu na uponyaji katika matunda, nafaka na mbogamboga

Hiki kitabu kwa ufupi kinaelezea utabibu ambao mungu alitupatia hapo awali, kwa kutumia matabibu wasaidizi kama maji, matunda, hewa safi na nishati ya jua. Aina za vyakula alivyotuelekeza na nguvu zake za utabibu. Kimegusia pia afya ya meno na utabibu wake kwa kuendana na lishe. Kimeunganisha utaalamunwa leo na maneno ya mungu aliyotwambia miaka 2000 iliyopita juu ya tiba. Kitabu hiki toleo la kwanza ilikua mwaka 2016 na kilichapishwa rasmi 2017 na toleo la 2 ni mwaka 2018. Kinapatikana "uwaridi app" kwa wale wenye simu janja. Gharama yake shilingi 5000 tu za kitanzania. Na kwa wenyeji wa dar es salaam wanaweza kisoma pale maktaba ya taifa zipo nakala zake bure.

2. USALAMA KATIKA MIFUMO YA UMEME
Hiki ni kitabu nilichokiandika mahususi kwa wale wote wanaotaka kuuelewa umeme kama nishati lakini pia na matumizi ya nishati hii katika njia salama ambayo itamuacha mzalishaji, msambazaji na msafirishaji katika hali salama kabisa. Kitabu hiki kimeongelea earthing systems na mambo mengine mengi yahususo umeme mkubwa na mdogo.
Nimekilenga zaidi kwa wanafunzi wa sekondari, veta na wale wanaosoma au wamemaliza tayari elimu zao za juu katika kada ya umeme na elektroniki.
Kitabu hiki toleo la kwanza ni mwaka 2019 kitapatikana kupitia mtandaoni(uwaridi app) lakini pia na hard copies. Kitapatikana pia kwa gharama ya 5000 tu fedha za kitanzania.

3.MAISHA YA CHUO
Kitabu hiki kinamuunganisha mtu yeyote yule na mazingira ya chuo katika ngazi zote, astashahada, stashahada na aina zote za shahada.
Kimeongelea zaidi maisha ya chuo katika nyanja za ujasiriamali, uongozi na siasa, taaluma na mengine mengi katika uhalisia wa kitanzania na kimataifa.
Pia kinaweza somwa na rika zote, kimegusia maisha ya vyuo vya ndani ya nchi lakini pia kwa jirani zetu pale kenya. Muda si mrefu kitapatikana kupitia uwaridi app. Nacho pia toleo la kwanza ni mwaka 2019. Hard copies pia zitapatikana. Maisha ya chuo kitapatikana kwa shilingi 3500 za kitanzania mtandaoni lakini hard copy kwa 5000 tu.

WAPENDWA MNAKARIBISHWA NYOTE KWA DONDOO MASWALI AU USHAURI. MUWE NA AMANI YA BWANA.
Mawasiliano, email odhiamboclion@gmail.com
0759154479
 

Attachments

  • FB_IMG_15389000668198165.jpg
    FB_IMG_15389000668198165.jpg
    78.8 KB · Views: 55
  • IMG_20181220_171011_537.jpg
    IMG_20181220_171011_537.jpg
    106.8 KB · Views: 31
  • MAISHA YA CHUO(1).jpg
    MAISHA YA CHUO(1).jpg
    178.1 KB · Views: 56
Ndugu ahsante kwa swali
Nitakujibu kama ifuatavyo, naamini unawaongelea waadventista wasabato, ile ni taasisi ndugu ya dini iliyokua na watu na mfumo wa kiutawala.
Hii siyo kazi ya taasisi iyo uliyoitaja na yumkini pia sijaitaja katika bandiko langu. Kwa ufupi kabisa vitabu ivyo vimeidhinishwa na wanataaluma wa kada husika. Ahsante, lakini nisingependa tuzungumzie maswala ya dini. Taaluma haina dini.
 
Samahi kwa kuchelewa kukujibu ila ingia play store itafute uwaridi app itakuja na utaipakua. UWARIDI( UMOJA WA WAANDISHI WA RIWAYA WENYE DIRA)
Nikitaka kuweka kitabu changu huko inakuwaje. Malipo na mambo yakisheria yakoje?
 
Back
Top Bottom