Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,790
- 24,382
NOTE: Nitapitia baadaye kurekebesha typos pole pole; ukikutana nazo usizitilie maanani.
Miaka takriban 45 iliyopita, Iraq ilipitia wakati mgumu sana. Kwanza, mwaka 1979 ulikuwa na matukio mawili makubwa ndani ya Iraqi na Iran. Mwaka huo, mwezi July huko Iraq, Saddam Hussein alimpindua rais al-Bakr ambaye alikuwa anataka kuunganisha Iraq na Syria kusudi yeye awe Rais halafu Hafaz -el-hDssad awe makamu wa rais, jambo ambalo Saddam hakulipenda kwa vile yeye ndiye alikuwa makamu wa rais wa Iraq wakati huo, hivyo muungano huo ungempunguzia madaraka. Kwa upande wa Iran, Ayatollah Ruholla Khomein alimpindua mfalme (Shah) wa Iran na kuweka utawala wa kiislamu. Mfalme huyo alikuja kujilaumu sana kwani siku za nyuma kidogo, Khomein alikuwa amehukumiwa na mahakani hukumu ya kifo, lakini kwa vile alikuwa ni Ayatollah (kiongozi wa kidini), basi mfalme akamnusuru na kifo ila akamuamru akaishi uhamishoni ambapo Khomein alitumia maisha yake yote akiwa Uturuki na Iraq akiwa anarekodi kanda za kuhamasisha watu wa Iran waupoinge utawala wa Mfamle bali wakubali serikali ya kiislamu. Hata hivyo mwaka 1978, Saddam Hussein ambaye alikuwa makamu wa rais wakati hakupendezwa na propaganda hizo za kidini zilizokuwa zinaendeshwa na Khomein, akaamua kumfukuza kutoka Iraq, ndipo Khomein akakimbilia Paris Ufaransa huku akiendelea na kampeini zake za kupinga utawala wa kifalme huko Iran ili kuweka utawala wa kiislamu. Baadaye mwishoni mwa mwaka 1979 ndipo Khomein alifanikiwa kuitisha maandamano makubwa sana kupitia kanda zake zile ambayo yamlishinda mfalme akakimbia nchi na kusababisha Khomein aunde serikali ya kiislamu ambayo bado iko madarakani hadi leo.
Kati ya mwaka 1979 na 1980 uhusiano kati ya Iran na Iraq ulidororoa sana hasa kwa vile Saddam hakupenda kampein za Khomein za kutaka hata Iraq nayo iongozwe kiislamu. Baada ya msuguano wa kiitikadi wa mwaka mmoja Saddam akaamua kutuma majeshi yake kuivamia Iran ili kuondoa utawala huo wa kidini. Ikumbukwe Saddam alikuwa ni liberal alikuwa hataki kuendsha nchi kdini, ndiyo maana kwenye serikali yake kulikuwa na wakristu na wanawake, jambo ambalo Khomein alikuwa akipinga sana.
Vita ili ilidumu kwa miaka minane, kuanzia 1980 hadi 1988. Iraq ilikuwa na silaha nyingi za kirusi wakati Iran ilikuwa na silaha nyingi za kimarekani zilizoanchwa Shah. Kutokana na kuwa wakati wa mapinduzi utawala wa Khomein uliteka wamarekani wengi waliokuwa wanafanya kazi ubalozini, Marekani ilamua kuanza kusaida Saddam. Kuna mambo mengine sana yaliyotokea ndani ya kipindi hicho cha miaka minane na kuna wakati Marekani iliisaidia pia Iran ili kuokoa mateka wa kimarekani walikuwa wamatekwa huko Lebanon. Haiyo ndumila kuwili ya Marekani ilimkasirisha sana Saddam kiasi kuwa hata baada ya vita kuisha hakuisamehe marekani kabisa. Baada ya vita ile, Khomeini hakudumu hata mwaka mmoja akafariki mwezi June 1989.
View: https://www.youtube.com/watch?v=ZuAJ35F235Q
Kilichojifisha hapo katikati ni kwamba, kabla ya Saddam kuingia madarakani, Iraq ilikuwa imetoa contract kwa kampuni moja ya kifaransa kujenga kbinu vya nuclear. Mwaka 1981, wakati Iraq imeanza kuishambulia Iran, ndipo Israel ilikwenda kubomoa vinu vyake vya nuclear kabla hata havijakamilika.
View: https://www.youtube.com/watch?v=1ogqKsGcYyc
Miaka miwili baada ya vita ya Iran, Saddam bado alikuwa na usongo sana wa kutaka kuikosesha marekani mafuta na awe na uwezo wa kupanga bei ya ,mmafuta duniani. Ila kwa vile wakati huo Marekani ilikuwa hainunui mafuta ya Iran au ya Iraq badala yake ilikuwa inanunua mafuta ya Kuwait, basi Saddam akaamua kuivamia Kuwait mwezi August 1990 ili aweze kucontrol mafuta hayo na hivyo kuiminya Marekani.
Uvamizi wa Kuwait ulikabiliwa na shutuma za kimataifa, ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa azimio nambari 660 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililotaka Iraq kujiondoa mara moja kutoka Kuwait, na kuwekwa kwa vikwazo vya uchumi dhidi ya Iraq kupitia azimio namba 661 la Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa masukumo kutoka kwa Waziri mkuu wa Uingereza wakati huo Margaret Thatcher na Rais wa marekani George H. W Bush.
Baadaye, Azimio namba 678 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitishwa tarehe 29 Novemba 1990 na kuitaka Iraq iondoe majeshi yake kutoka Kuwait kabla ya tarehe 15 Januari 1991. Azimio hilo pia liliunda muungano wa kijeshi wa kujiandaa kuyandoa majeshi ya Iraq kutoka Kuwait kwa nguvi iwapo hayatafanya hivyo kwa hiari kabla ya tarehe 15 January. Nchi nyingi zilijiunga na muungano huo uliongozwa na Marekani.
Wakati huo mkuu wa majeshi ya Marekani alikuwa General Coilin Powel na kamanda aliyepewa jukumu la kuongoza muungano huo alikuwa General Norman Schwarzkopf. Ilipofika tarehe 16 Januari 1991, George H.W Bush alitangaza vita kuanza.
View: https://www.youtube.com/watch?v=KJ6qpFpIFkY
na ndipo Genera Shwarzkoof akaanza kazi aliyotumwa; hebu msikilze hapo.
View: https://www.youtube.com/watch?v=wKi3NwLFkX4
Baada ya siku 20 tu, jeshi lote la Saddam lilikuwa lisheavunjwa vunjwa na vita ikaisha rasmi tarehe 28 february 1991
View: https://www.youtube.com/watch?v=sSmI_z-RDEY
Jisomee vitabu hivi