Mbona alitumia Napalm. Aliipiga Hanoi mfululizo kwa B52 bombers. Mrusi aliwapa Vietnam Kaskazini SAM missiles wakaweka mraba wa ulinzi juu ya anga la Vietnam. Ndege zilianguka kweli. Siku moja kijana wa miaka 19 (mpiga mizinga na makombora ya kutungua ndege SAM missiles) alifanikiwa kutungua ndege 19 za Marekani na ikatangazwa Ulimwengu mzima. Wavietnam wanasema wanahistoria walitumia theluthi 2 ya muda wote wa vita kuchimba mahandaki na njia za chini kwa chini katika nchi yote. Walisafirisha makombora kama kuni kwa migui kutoka Kaskazini hadi kusini kwa njia za maficho. Moja ilikuwa maarufu kama Ho Chi Minh Trail. Silaha, vyakula vyote vilisafirishwa kwa miguu wakati wa msimu wa mvua nyingi za monsoon. Mtu mmoja vietcong guerilla angepewa kombira moja tu ahakikishe linafika ama Khen Sahn ama Bien Hoa salama kutumiwa