Hii miaka ya 2020 ni moto sana kwa Dunia

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Wote mtakumbuka baada ya kupigwa na Knockout nzito sana kutoka kwa Bondia covid 19, ugonjwa ulikunguta Dunia nzima miaka ya 2020 hadi kuanza kupunguza makali 2021 baada ya kuanzia huko China mwishoni mwa mwaka 2019 kwa kuwatembezea kichapo Wachina.

Baada ya Covid19 yaani ugonjwa wa Corona, Dunia haikupoa mara gafla Urusi na Ukraine wakatangaza vita 2021 hadi hii leo bado Ukraine anaendelea kupokea na kula kwenzi kutoka kwa kaka yake Urusi.

Bado hatujaendelea vizuri na vita ya Ukraine na Urusi, mzozo wa muda mrefu wa Palestina na Israel nao ukachochewa moto na wanamgambo wa hamas. Jambo lililopelekea macho yote kuhamia Mashariki ya Kati.

Huu mzozo wa Palestina na Israel umepelekea nguvu yote na macho ya Dunia kuhamia Israel. Wakati muda huo huo Ukraine ambaye aliyekuwa akideka na kulia sana kwa nchi za Ulaya na Magharibu akisahaulika.

Kwa mtazamo wangu Urusi sasa hivi anachekelea dogo (Ukraine) kaachwa peke yake, mama kaenda kupiga story kwa jirani. Sasa Ukraine atakula kwenzi za kimya kimya mpaka aombe poo. Urusi hatatumia hii vita ya Israel kufanya ujasusi na umafia wa kimya kimya huko Ukraine. Ukraine hakuna kudeka tena, ni mwendo wa kwenzi. 😂😂😂
 
Wote mtakumbuka baada ya kupigwa na Knockout nzito sana kutoka kwa Bondia covid 19, ugonjwa ulikunguta Dunia nzima miaka ya 2020 hadi kuanza kupunguza makali 2021 baada ya kuanzia huko china mwishoni mwa mwaka 2019 kwa kuwatembezea kichapo Wachina.
ka tena, ni mwendo wa kwenzi 😂😂😂
Umeongea kitu kuntu sana
 
"..hatatumia.."

AU

"..atatumia.."?????

Uandishi mwingine unatia mashaka
 
Ishu kubwa hapa ni Ukraine ingawaje bado vita inaendelea huko...ukiona wahuni Wagner wanaamua kuandamana mtaani na siraha kwenda kuchukua Nchi mpaka inapelekea mauti ya kiongozi wao jua Nchi hakuna hapo tulilishwa propaganda nyingi za matangopori..
 
Back
Top Bottom