Vita ya Raila Odinga na Mugabe

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Nimepokea kwa mshangao mwito wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga kumtaka Rais Mugabe wa Zimbabwe kujiuzulu au vipelekwe vikosi vya kijeshi kwenda kumng'oa.

Hivi WANAJAMII,
Kweli Odinga anastahili kumkemea Mugabe au alipaswa kuanza kujikemea mwenyewe na kisha kumkemea Rais KIBAKI?

Raila Odinga amesahau Vifo vilivyotokea nchini Kenya mara tuu baada ya uchaguzi mkuu?

Tena je Raila amesahau vituko vya kuwatia nguvuni waandishi wa habari hivi majuzi katika kukumbuka siku ya jamhuri?

Exaud J. Makyao
0784347001
 
Sioni cha kushangaa. Ukanzamizaji ni lazima ukemewe na kila mtu.
 
Raila Odinga amesahau Vifo vilivyotokea nchini Kenya mara tuu baada ya uchaguzi mkuu?

Have u ever heard about forgive and forget? Anachokisema ni kweli, Mugabe anaendelea tu kula vichwa vya raia wake continuously, Kenya kuna mauaji yanayoendelea? Mugabe must go! Now it is the time.
 
Odinga yuko sahihi bse Mugabe ata usuluhishi hataki sasa si kheri apinduliwe tuu au wale kichwa akapumzike kwa mola
 
Sioni cha kushangaa. Ukanzamizaji ni lazima ukemewe na kila mtu.

Vya kushangaa ni vingi katika kauli ya Raila:

1. Utatumia kipengele gani cha sheria za Zimbabwe "kumpindua" Mugabe?
2. Utapeleka Jeshi gani (UN, AU, la JK)) la kuivamia Zimbabwe kwa kanuni gani (which article in the UN, AU or TZ constitution)? Na hata ikivamiwa si watakufa watu wengi zaidi kuliko hao wa kipindupindu?

-- una habari Iraq ambako Mwamerika alimlazimisha Saddam Bin Hussein kuangamiza kwanza silaha zake KABLA YA KUMVAMIA kwamba hadi 13/12/08
Number Of Iraqis Slaughtered is "1,284,105" and U.S. Military Personnel Sacrificed (Officially acknowledged) is "4,209" !! Idadi hiyo eti lengo ni kumng'oa mtu mmoja tu lakini MiratKad na WAPENZI WA MAREKANI HAWAJAKEMEA au hata kuandamana alipokuja 'Kichaka' hapa Bongo.
-- hivi Nyerere aliwahi kutaja HESABU YA WAGANDA NA WATANZANIA WALIOPOTEZA MAISHA YAO TULIPOIVAMIA UGANDA? Lazima itakuwa ni MALAKI. Kisa? Kumng'oa Idi Amini na kumsimika rafiki yake Obote ambaye hata hivyo Waganda wakampindua tena!

3. Akina Raila, Watanzania na Afrika kwa jumla tuachane na MTAZAMO WA UPANDE MMOJA. Sisi tunakutana na wa-Zimbabwe wanaeleza HALI TOFAUTI KABISA NA HIYO YA BBC, CNN, VOA lakini wao hawana vyombo vya habari ambavyo vinaweza kutangaza au kuchapisha UKWELI ULIVYO. INASIKITISHA SANA PROPAGANDA ZINAZOSAMBAZWA, ndio maana SADC hawakubaliani nazo
4. Madhila na matatizo ya kiuchumi WALIOYASABABISHA NI HAO HAO WAINGEREZA NA MAREKANI na hata wanathubutu "kuangamiza wananchi" kwa kuiwekea vikwazo Zimbabwe ili Mugabe achukiwe. One of the methods used by the US to depopulate the BLACK race (in addition to biological weapons) is sanctions. Plse comrades, read news from other sources ......

TUFUMBUE MACHO WAFRIKA ...... MATAIFA YA MAGHARIBI SIO MARAFIKI!!!!
WAMESHINDWA MASHARIKI YA KATI HADI WANAPATA "KIPIGO" CHA MAANGAMIZI YA UCHUMI WAO. HIVI HAMJIULIZI KULIKONI PAMOJA NA WANAUCHUMI WAO WOTE NA VYUO VIKUU VYAO VYOTE WAMESHTUKIA WAMO KATIKA "ECONOMIC RECESSION" AMBAPO WAARABU WANAOFUATA ISLAMIC SHARIAH ILIYOANZISHWA NA ILLITERATE HAWAKUATHIRIKA????
 
Odinga, Tsangarai na Zuma hao ndio vibaraka wa wazungu wanaojipendekeza na wanaotumiwa kuhujumu Africa tuwe macho nao
 
Odinga, Tsangarai na Zuma hao ndio vibaraka wa wazungu wanaojipendekeza na wanaotumiwa kuhujumu Africa tuwe macho nao

Hata nami naomba kuwa kibaraka wa wazungu kwa kuunga mkono kung'olewa kwa Robert Mugabe, ana kila sifa ya kung'olewa kwa nguvu...

Nafikiri ifikie mahala tuwaangalie wazimbabwe na mateso wanayopitia kuliko kuendeleza malumbano ya vibaraka na wazalendo wauwaji... naona imekuwa tabia kwamba kila atoae mwito wa mugabe kung'olewa anahesabika kama ni kibaraka wa wazungu.

Ni kiongozi gani anayeweza kujiona kama yeye si kibaraka wa wazungu kwa namna moja au nyingine akiwemo Mugabe mwenyewe, wakati umefika waafrika tuukatae ufedhuli wa Mugabe an ango'olewe
 
Nimepokea kwa mshangao mwito wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga kumtaka Rais Mugabe wa Zimbabwe kujiuzulu au vipelekwe vikosi vya kijeshi kwenda kumng'oa.

Hivi WANAJAMII,
Kweli Odinga anastahili kumkemea Mugabe au alipaswa kuanza kujikemea mwenyewe na kisha kumkemea Rais KIBAKI?

Raila Odinga amesahau Vifo vilivyotokea nchini Kenya mara tuu baada ya uchaguzi mkuu?

Tena je Raila amesahau vituko vya kuwatia nguvuni waandishi wa habari hivi majuzi katika kukumbuka siku ya jamhuri?

Exaud J. Makyao
0784347001
economist umechanganya 'supply and demand' hapa,issue ni kwamba Mugabe anendelea kuua,hayo matatizo ya wengine uliowataja hayapo tena yalikuwa ya mpito, uwepo wa Odinga au Kibaki hauleti mateso kwa wakenya,kilichobaki ni historia...
Mugabe anaendeleza matateso kwa raia wa Zimbabwe.

Akamatwe na ahukumiwe kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu
 
Hata nami naomba kuwa kibaraka wa wazungu kwa kuunga mkono kung'olewa kwa Robert Mugabe, ana kila sifa ya kung'olewa kwa nguvu...

Nafikiri ifikie mahala tuwaangalie wazimbabwe na mateso wanayopitia kuliko kuendeleza malumbano ya vibaraka na wazalendo wauwaji... naona imekuwa tabia kwamba kila atoae mwito wa mugabe kung'olewa anahesabika kama ni kibaraka wa wazungu.

Ni kiongozi gani anayeweza kujiona kama yeye si kibaraka wa wazungu kwa namna moja au nyingine akiwemo Mugabe mwenyewe, wakati umefika waafrika tuukatae ufedhuli wa Mugabe an ango'olewe

Nivizuri urudie historia ya siasa ya Zimbabwe na wazungu ndo utaweza elewa lini Mugabe amaanza kuwa kiongozi mbaya na kwa sababu zipi. wazimbabwe kuteseka nikwasababu Sabotage zinazofanywa na wazungu kwa kutokubali siasa za kuwamilikisha wazungu 80% ya aridhi ya Zimbabwe. Fungua macho!!
 
[QUOTE=Bull;341674]Nivizuri urudie historia ya siasa ya Zimbabwe na wazungu ndo utaweza elewa lini Mugabe amaanza kuwa kiongozi mbaya na kwa sababu zipi. wazimbabwe kuteseka nikwasababu Sabotage zinazofanywa na wazungu kwa kutokubali siasa za kuwamilikisha wazungu 80% ya aridhi ya Zimbabwe. Fungua macho!![/QUOTE]

Mkuu Bull , visingizio vya Mzee mzima Mugabe juu ya hali ya Zimbabwe kwa sasa havina substance yoyote.
Pamoja na kutokubaliana na waingereza huo sio mwisho wa dunia.
Mugabe alitakiwa awe mwanasiasa wa kizazi kipya ili kudeal na wazungu hao.Kwa kupambana nao ana kwa ana itamwia vigumu sana kubreak through.
Hivi sasa serikali inamshinda kuendesha,chakula hamna,madawa hamna muindombinu ndio kwaheri.Kipindupindu kilichotokea ndio uthibitisho wa kuisha kwa miundombinu ya maji.
Kimsingi cholera inatokana na wadudu waitwao ecoli, wanaoishi katika kinyesi cha binadamu.Hivyo basi miundombinu ya maji machafu na maji safi isipopata matunzo(maintainance) matokeo yake ndio kutoboka mabomba na kuchangayika kwa maji hayo.Ndicho kinachoendelea Zimbabwe.Hapa DSM vile vile tumeona hili.
Raila kutaka Mugabe apinduliwe ni kilio cha mtu aliyekata tamaa na Mugabe.
Mugabe haonyeshi nia yoyote jatika kucompromise na maadui zake, na maadui zake wanamfix vilivyo kwa kumyima misaada.
 
Back
Top Bottom