Vita ya Lissu, Ndugai yakolea

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
666
421
MOTO wa kuwashtaki kwa wananchi Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai uliowashwa na Chadema, jijini Dar es Salaam Februari 10 mwaka huu, unaendelea huku chama hicho kikieleza kuwa kitawabana viongozi hao hadi wajiuzulu.

Mbali na hilo, chama hicho kimesema Bunge, halina uwezo wa kuanzisha chombo cha habari kitakachokuwa chanzo cha habari kwa vyombo vingine vya habari.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa alisema kwamba Spika wa Bunge naye hana uwezo wa kuunda Kamati za Bunge na kwamba wanachokifanya viongozi hao ni kudhoofisha mamlaka ya mhimili huo wa taifa.

Katika mkakati wa kumbana Spika na naibu wake ili wajiuzulu, Dk Slaa alisisitiza kuwa watatumia nguvu ya umma pamoja na mikutano inayoendelea nchi nzima ili kuwashtaki na mikutano hiyo inaanzia mkoani Arusha.

"Tunaanzia Arusha mjini na mkutano wetu utafanyika kesho, atakuwepo Mwenyekiti wa chama taifa, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama" alisema Dk Slaa na kuongeza:

"Kila kanda itakuwa na ratiba zake, lengo letu ni kufanya mikutano na kuwaeleza wananchi ukweli na tutakwenda hadi vijijini."

Alisema mikutano hiyo kwa kila kanda inaweza kuchukua hadi mwezi mzima, huku akisisitiza kuwa kauli zinazotolewa na Makinda na Ndugai ni udikteta na kutaka kuirudisha Tanzania miaka 50 iliyopita.

Dk Slaa aliponda kitendo cha Makinda kuvunja baadhi ya Kamati za Bunge pamoja na Kashilillah kusema kwamba ofisi yake itazuia kuonyesha moja kwa moja vipindi vya Bunge, kabla ya juzi kuifuta kauli hiyo kwa maelezo kuwa sasa Bunge litaanzisha televisheni yake na vituo vingine vitakuwa vikichukua matangazo ya Bunge kupitia Televisheni hiyo.

"Anachokifanya Kashilillah ni kinyume na Katiba Ibara ya 18, Katibu wa Bunge. Hana uwezo wa kutoa tamko la kuzuia jambo fulani bila Bunge zima kuridhia mabadiliko hayo" alisema Dk Slaa na kuongeza;

"Hata Makinda naye hana mamlaka ya kuunda Kamati za Bunge, kifupi ni kwamba wanachokifanya ni kinyume na Kanuni ya Bunge ya 151(1) na 152(2)."

Chadema ambacho ni chama kikuu cha upinzani, mara kwa mara kimekuwa kikilalamikia utendaji kazi wa Spika na naibu wake.

Wakati huohuo, mabishano ya kurushiana maneno ya kashfa, ubabe na kutupiana lawama juu ya matumizi ya Kanuni za Bunge, viliibuka juzi kati ya Naibu Spika, Job Ndugai na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu walipohamishia malumbano yao nje ya Bunge.

Ndugai na Lissu walipambanishwa katika Kipindi cha Kipima Joto kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV.

Mwongozaji wa kipindi hicho, Rainfred Masako, alila zimika kufanya kazi ya ziada ili kupunguza jazba za Ndugai na Lissu, ambao kila mmoja alikuwa akimtupia lawama mwe nzake kuhusu masuala ya Bunge.

Awali wakati kipindi hicho kilipoanza, Masako alisema kuwa amewaalika viongozi hao ili kuzungumzia kanuni mbalimbali za kuendesha shughuli za Bunge.

Wakiwa wenye ghadhabu na kurushiana maneno ya uhasama, kila mmoja alionekana kumpania mwenzake na mara kadhaa mwongozaji alilazimisha kuwarudisha kwenye mstari, baada ya wawili hao kutoka nje ya mada.

Akianza kumtuhumu mwe nzake, Lissu alisema: "Mimi sina tatizo na kanuni…nasema kwa kiasi kikubwa ziko sawa, lakini tatizo ni hawa wanaozitafsiri. Spika wa Bunge amekuwa akionyesha upendeleo kwa chama chake na kushindwa kuzitafsiri Kanuni za Bunge."

Lissu alimtuhumu moja kwa moja Naibu Spika na Ndugai kuwa wameshindwa kuliongoza Bunge kwa kufuata kanuni na kwamba inavyoonyesha, wanafanya hivyo kwa kutokuelewa kanuni au kwa makusudi.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki, alisema kuwa tangu kuanza kwa Bunge la 10, Spika Anne Makinda na Ndugai wamekuwa wakiendesha Bunge kwa ubabe na kukandamiza hoja za upinzani, bila sababu.

"Mimi ninachofahamu, Spika anatakiwa kuendesha Bunge kwa kufuata kanuni, haki bila chuki wala upendeleo," alisema.

Alisema kuwa hadi sasa wa pinzani wamewasilisha rufani tisa mbele ya Kamati ya Kanuni za Bunge, lakini mpaka sasa ha zijafanyiwa kazi. Hata hivyo, Ndugai alimjibu akisema kuwa Bunge li naendeshwa kwa kanuni na kila kinacholalamikiwa na wapinzani walishirikishwa kikamilifu.

"Kinacholalamikiwa na watu ni utovu wa nidhamu wa baadhi ya wabunge ama kwa kuzikiuka kanuni au kufanya makusudi.

Kambi ya upinzani, inatumika kama wabunge wengine, kupa nga taratibu za mkutano na hata vikao bungeni. Hapa kuna Mnadhimu wa Serikali, kuna Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu," alisema na kuongeza:

"Upande wa pili kuna Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, wote tunashirikiana na hawa ndiyo wanamshauri Spika kwa pamoja kama kuna jambo."

Kauli hiyo ya Ndugai ilisababisha kuibuka kwa malumbano yaliyojaa jazba na vijembe kutoka katika pande zote mbili, huku Lissu akisisitiza kuwa pamoja na hayo, Spika anapindisha kanuni.

Sehemu ya malumbano yao yalikuwa hivi:

Lissu: Tatizo linaweza kuwa siyo Kanuni za Bunge, bali tatizo ni tafsiri ya kanuni mbele ya Spika, sijaelewa anafanya hivyo ama kwa kutokujua kanuni, au kufanya uamuzi kwa makusudi?

Ndugai: Kinacholalamikiwa na watu ni utovu wa nidhamu, kuna matumizi ya kanuni kama vile mwongozo, taarifa na kuhusu utaratibu, yaani vipengele hivi mbunge anaweza kuzungumza ovyo tu na Lissu ndiyo amekuwa kinara wa vurugu hizo.

Lissu: Ngoja nitoe mfano, Tangu kuanza kwa Bunge la 10, Spika Makinda na Naibu wake, tumeshawasilisha rufani tisa mbele ya Kamati ya Kanuni za Bunge, hoja binafsi kukandamizwa na uamuzi wa ubabe kwa wabunge wa kambi ya upinzani.

Ndugai: Kama kuna rufani hizo, taratibu zipo na zitafuatwa, ila mimi mpaka sasa sijapata nakala yoyote hata hiyo inayonitaka kujiuzulu. Lakini, mbona wewe Lissu tumekufikisha mbele ya Kamati ya Maadili na bado hujashughulikiwa?

Lissu: Unaona sasa, nikisema Spika hajui Kanuni za Bunge au anatumia makusudi naonekana mtovu wa nidhamu na hivi ndivyo siku zote Bunge linavyokuwa.

Ndugai: Tatizo ndiyo hilo kwa ndugu yangu, rafiki yangu Lissu, yaani anapenda kulaumu tu uongozi, staha ni pamoja na mavazi na mazungumzo, halafu hatua ya kutoa namba zetu za simu kule Mwembeyanga kwa kweli hayapendezi, labda aiombe radhi jamii.

Lissu: Hapa tuko kwenye mjadala wa Kanuni za Bunge, mambo ya Mwembeyanga si mahala pake, hilo pia ni tatizo ninalolifananisha na ukiukwaji wa kanuni. Nafikiri ingekuwa bora zaidi tukazingatia mjadala wetu.

Ndugai: Yaani ukashinikize kwa wananchi Mwembeyanga kuniondoa madarakani nisiseme, tatizo la Lissu ndiyo hilo tunatakiwa kuwa wavumilivu. Wenye mamlaka ya kuniondoa mimi ni wabunge, kama walivyonipatia nafasi hiyo.

Baada ya kuona malumbano yamezidi kuongezeka mwendeshaji kipindi alihamishia mjadala kwa watu wengine walioalikwa kwenye kipindi hicho hali iliyochangia kushusha jazba.

Ndugai apandisha munkari

Hata hivyo, katika mjadala huo, Ndugai alionekana kujaa hasira baada ya kubanwa maswali kutoka kwa wachangiaji wengine walioshiriki mjadala huo na wananchi waliokuwa wakipiga simu.

Washiriki wengine walikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiraia ya kufuatilia Mwenendo wa Bunge, Pakozi Azaniye na Mtafiti wa Masuala ya Haki za Binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pansience Mlowe.

Akichangia mjadala huo, Azaniye alisema: "Wakati mwingine tuliona Spika alipotafsiri Kanuni na mbunge akaitumia tafsiri hiyo kwa mbunge mwingine tofauti na kanuni ilivyo.

Akitoa taarifa za Bunge lililomalizika Azaniye alisema katika hoja binafsi 30 ni hoja 18 tu ndizo zimeshajadiliwa hatua iliyosababisha hasara ya kupotea kwa saa 12 na zaidi ya 300 milioni kujitokeza.

Hata hivyo, kila mmoja alipopewa nafasi ya kuaga, Lissu alitaka kuwepo utaratibu wa Bunge zima kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni, lakini Ndugai alitumia nafasi hiyo kumshambulia Lissu kwa utovu wa nidhamu na kulidhalilisha Bunge, kabla ya Masako kumkatiza akimtaka atumie nafasi hiyo kueleza mwenendo wa Bunge na utendaji wake.





source: mwananchi
 
Huyo mwandishi wa habari aliyeandika habari hii anashangaza sana hasa anapoandika kuhusu kipindi cha kipima joto cha ITV. Wengi tulikishuhudia kipindi hicho na baadhi ya mambo anayoripoti hayakuwa kama inavyotajwa hapa. Anyway hawa ndio waandishi wetu wa siku hizi, na gazeti la mwananchi limeanza kupoteza umakini.

Yani anapotosha hata jina la Marcos Albanie na kumuita Pakozi Azanie! Hahaha kazi kweli kweli
 
Huyo mwandishi wa habari aliyeandika habari hii anashangaza sana hasa anapoandika kuhusu kipindi cha kipima joto cha ITV. Wengi tulikishuhudia kipindi hicho na baadhi ya mambo anayoripoti hayakuwa kama inavyotajwa hapa. Anyway hawa ndio waandishi wetu wa siku hizi, na gazeti la mwananchi limeanza kupoteza umakini.

Yani anapotosha hata jina la Marcos Albanie na kumuita Pakozi Azanie! Hahaha kazi kweli kweli

huyu jamaa kakurupuka au kasimuliwa habari? Yawezekana yuko training/internship?
 
Huyu mwandishi ni kilaza wa kufa mtu! Ameandika aliyo taka yeye wakati wengi wetu tulio shuhudia kipima joto tunajua washiriki walicho jadili. Uandishi wa namna hii bila shaka una malengo maalumu ya kuficha uhalisia wa kilicho onekana.

Kibaya zaidi ukilaza wa mwandishi umejidhihirisha mpaka kwenye kuto kulijua jina la mkurugenzi wa taasisi ya kiraia inayo fuatilia mambo ya bunge! Bwana huyo anaitwa Marcosy Albanie mwandishi yeye kaandika jina analotaka yeye ili kukidhi matakwa ya ukilaza wake. Mwananchi linaelekea kufuata mkondo wa kale ka gazeti ambako kakitoka kiwandani kanaenda moja kwa moja kufungia maandazi.
 
Huyo mwandishi wa habari aliyeandika habari hii anashangaza sana hasa anapoandika kuhusu kipindi cha kipima joto cha ITV. Wengi tulikishuhudia kipindi hicho na baadhi ya mambo anayoripoti hayakuwa kama inavyotajwa hapa. Anyway hawa ndio waandishi wetu wa siku hizi, na gazeti la mwananchi limeanza kupoteza umakini.

Yani anapotosha hata jina la Marcos Albanie na kumuita Pakozi Azanie! Hahaha kazi kweli kweli

leo nimekupa like manake nimeshangazwa na hii habari kiukweli lkn swali je ni mwadish wa habari ama editor alikosea??
hvi kwani wewe editor ukiletewa habari na mwandish hunasababu ya kuihakiki??
 
Mkuu Mwita Maranya.
Tatizo la mwandishi ni lipi zaidi ya kukosea jina kama ulivyoainisha?. Naomba utujuze tulioko kijijini na mifuko yetu siyo mirefu kuwa na television.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita Maranya.
Tatizo la mwandishi ni lipi zaidi ya kukosea jina kama ulivyoainisha?. Naomba utujuze tulioko kijijini na mifuko yetu siyo mirefu kuwa na television.

Hoja za msingi alizozungumza Lissu hajazizungumza zaidi ya kuiandika habari hiyo kishabiki na kinafiki. Daaaaah Mwananchi karibu katika ulimwengu mwingine yalipo magazeti mengine kama Majira, Mtanzania. Karibu sana kwa ukanjanja huu.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mwandishi ni kilaza wa kufa mtu! Ameandika aliyo taka yeye wakati wengi wetu tulio shuhudia kipima joto tunajua washiriki walicho jadili. Uandishi wa namna hii bila shaka una malengo maalumu ya kuficha uhalisia wa kilicho onekana.

Kibaya zaidi ukilaza wa mwandishi umejidhihirisha mpaka kwenye kuto kulijua jina la mkurugenzi wa taasisi ya kiraia inayo fuatilia mambo ya bunge! Bwana huyo anaitwa Marcosy Albanie mwandishi yeye kaandika jina analotaka yeye ili kukidhi matakwa ya ukilaza wake. Mwananchi linaelekea kufuata mkondo wa kale ka gazeti ambako kakitoka kiwandani kanaenda moja kwa moja kufungia maandazi.

hivi ile video inayoonesha mjadala wa kipima joto imeondolewa? najaribu kuitafuta nimeshindwa!!!!! msaada tafadhali kama twaweza kuipata. Na je kipima joto huwa kuna marudio?
 
Hoja za msingi alizozungumza Lissu hajazizungumza zaidi ya kuiandika habari hiyo kishabiki na kinafiki. Daaaaah Mwananchi karibu katika ulimwengu mwingine yalipo magazeti mengine kama Majira, Mtanzania. Karibu sana kwa ukanjanja huu.

Chaguzi kitaifa zinakaribia. Magazeti yasiyokuwa na nguzo kisiasa lazima yaanze kujimbambanua.

Politician knows, a pen is mighter than the sword. Fedelis Butahe ameishakamilisa kazi yake aliyopewa na wanasiasa kupitia kwa editor.
 
Inasikitisha gazeti la mwananchi limetekwa na mafisadi sasa linaandika uongo wa wazi
uliowashwa na Chadema, jijini Dar es Salaam Februari 10 mwaka huu,
unaendelea huku chama hicho kikieleza kuwa kitawabana viongozi hao hadi
wajiuzulu.

Mbali na hilo, chama hicho kimesema Bunge, halina uwezo wa kuanzisha
chombo cha habari kitakachokuwa chanzo cha habari kwa vyombo vingine vya
habari.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu, Katibu Mkuu
wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa alisema kwamba Spika wa Bunge naye
hana uwezo wa kuunda Kamati za Bunge na kwamba wanachokifanya viongozi
hao ni kudhoofisha mamlaka ya mhimili huo wa taifa.

Katika mkakati wa kumbana Spika na naibu wake ili wajiuzulu, Dk Slaa
alisisitiza kuwa watatumia nguvu ya umma pamoja na mikutano inayoendelea
nchi nzima ili kuwashtaki na mikutano hiyo inaanzia mkoani Arusha.

“Tunaanzia Arusha mjini na mkutano wetu utafanyika kesho, atakuwepo
Mwenyekiti wa chama taifa, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa
chama” alisema Dk Slaa na kuongeza:

“Kila kanda itakuwa na ratiba zake, lengo letu ni kufanya mikutano na
kuwaeleza wananchi ukweli na tutakwenda hadi vijijini.”

Alisema mikutano hiyo kwa kila kanda inaweza kuchukua hadi mwezi mzima,
huku akisisitiza kuwa kauli zinazotolewa na Makinda na Ndugai ni
udikteta na kutaka kuirudisha Tanzania miaka 50 iliyopita.

Dk Slaa aliponda kitendo cha Makinda kuvunja baadhi ya Kamati za Bunge
pamoja na Kashilillah kusema kwamba ofisi yake itazuia kuonyesha moja
kwa moja vipindi vya Bunge, kabla ya juzi kuifuta kauli hiyo kwa maelezo
kuwa sasa Bunge litaanzisha televisheni yake na vituo vingine vitakuwa
vikichukua matangazo ya Bunge kupitia Televisheni hiyo.

“Anachokifanya Kashilillah ni kinyume na Katiba Ibara ya 18, Katibu wa
Bunge. Hana uwezo wa kutoa tamko la kuzuia jambo fulani bila Bunge zima
kuridhia mabadiliko hayo” alisema Dk Slaa na kuongeza;

“Hata Makinda naye hana mamlaka ya kuunda Kamati za Bunge, kifupi ni
kwamba wanachokifanya ni kinyume na Kanuni ya Bunge ya 151(1) na
152(2).”

Chadema ambacho ni chama kikuu cha upinzani, mara kwa mara kimekuwa
kikilalamikia utendaji kazi wa Spika na naibu wake.

Wakati huohuo, mabishano ya kurushiana maneno ya kashfa, ubabe na
kutupiana lawama juu ya matumizi ya Kanuni za Bunge, viliibuka juzi kati
ya Naibu Spika, Job Ndugai na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Tundu Lissu walipohamishia malumbano yao nje ya Bunge.

Ndugai na Lissu walipambanishwa katika Kipindi cha Kipima Joto
kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV.

Mwongozaji wa kipindi hicho, Rainfred Masako, alila zimika kufanya kazi
ya ziada ili kupunguza jazba za Ndugai na Lissu, ambao kila mmoja
alikuwa akimtupia lawama mwe nzake kuhusu masuala ya Bunge.

Awali wakati kipindi hicho kilipoanza, Masako alisema kuwa amewaalika
viongozi hao ili kuzungumzia kanuni mbalimbali za kuendesha shughuli za
Bunge.

Wakiwa wenye ghadhabu na kurushiana maneno ya uhasama, kila mmoja
alionekana kumpania mwenzake na mara kadhaa mwongozaji alilazimisha
kuwarudisha kwenye mstari, baada ya wawili hao kutoka nje ya mada.

Akianza kumtuhumu mwe nzake, Lissu alisema: “Mimi sina tatizo na
kanuni…nasema kwa kiasi kikubwa ziko sawa, lakini tatizo ni hawa
wanaozitafsiri. Spika wa Bunge amekuwa akionyesha upendeleo kwa chama
chake na kushindwa kuzitafsiri Kanuni za Bunge.”

Lissu alimtuhumu moja kwa moja Naibu Spika na Ndugai kuwa wameshindwa
kuliongoza Bunge kwa kufuata kanuni na kwamba inavyoonyesha, wanafanya
hivyo kwa kutokuelewa kanuni au kwa makusudi.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki, alisema kuwa tangu kuanza kwa Bunge la
10, Spika Anne Makinda na Ndugai wamekuwa wakiendesha Bunge kwa ubabe
na kukandamiza hoja za upinzani, bila sababu.

“Mimi ninachofahamu, Spika anatakiwa kuendesha Bunge kwa kufuata kanuni,
haki bila chuki wala upendeleo,” alisema.

Alisema kuwa hadi sasa wa pinzani wamewasilisha rufani tisa mbele ya
Kamati ya Kanuni za Bunge, lakini mpaka sasa ha zijafanyiwa kazi. Hata
hivyo, Ndugai alimjibu akisema kuwa Bunge li naendeshwa kwa kanuni na
kila kinacholalamikiwa na wapinzani walishirikishwa kikamilifu.

“Kinacholalamikiwa na watu ni utovu wa nidhamu wa baadhi ya wabunge ama
kwa kuzikiuka kanuni au kufanya makusudi.

Kambi ya upinzani, inatumika kama wabunge wengine, kupa nga taratibu za
mkutano na hata vikao bungeni. Hapa kuna Mnadhimu wa Serikali, kuna
Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu,” alisema na kuongeza:

“Upande wa pili kuna Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mnadhimu wa Kambi ya
Upinzani na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, wote tunashirikiana na
hawa ndiyo wanamshauri Spika kwa pamoja kama kuna jambo.”

Kauli hiyo ya Ndugai ilisababisha kuibuka kwa malumbano yaliyojaa jazba
na vijembe kutoka katika pande zote mbili, huku Lissu akisisitiza kuwa
pamoja na hayo, Spika anapindisha kanuni.

Sehemu ya malumbano yao yalikuwa hivi:

Lissu: Tatizo linaweza kuwa siyo Kanuni za Bunge
 
hivi ile video inayoonesha mjadala wa kipima joto imeondolewa? najaribu kuitafuta nimeshindwa!!!!! msaada tafadhali kama twaweza kuipata. Na je kipima joto huwa kuna marudio?

Mkuu.
Kipima joto huwa hakina marudio na sikumbuki kama ilishawekwa video ya kipima joto cha juzi hapa jukwaani.

Kama kuna mdau anaijua link yenye hiyo video atuwekee.
 
Huyo mwandishi wa habari aliyeandika habari hii anashangaza sana hasa anapoandika kuhusu kipindi cha kipima joto cha ITV. Wengi tulikishuhudia kipindi hicho na baadhi ya mambo anayoripoti hayakuwa kama inavyotajwa hapa. Anyway hawa ndio waandishi wetu wa siku hizi, na gazeti la mwananchi limeanza kupoteza umakini.

Yani anapotosha hata jina la Marcos Albanie na kumuita Pakozi Azanie! Hahaha kazi kweli kweli

Mambo ya bahasha ya kaki hayo, imevuruga macho, akili hadi roho.. hawa ndo Mwakyembe alishawahi kuwaita WAHANDISI wa habari wakaja juu.... kazi ipo
 
Me naomba wanaojua kipindi cha kipima joto kinarudiwa lini, watuambie ili sisi tuliokosa tuangalie.
 
Tafadhali tujulisheni kama huwa kuna marudio nasi tuone??? Maana mwananchi sasa ni mwana majira,mwanamtanzania N.k.
 
Back
Top Bottom