Vita ya Kagasheki na Dk Aman ngoma nzito,madiwani waburuzwa Takukuru

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Bukoba wameingia matatani baada ya kuhojiwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kupokea rushwa ili kusaini waraka wa kumng'oa Meya wa Manispaa hiyo Dk Anatory Amani.Tuhuma nyingine ni kuhongwa safari za matembezi nchini Uganda.Kamanda wa TAKUKURU amethibitisha kuhojiwa kwa madiwani hao
 
Kagasheki anaingiaje hapo?
Au ndo prezoo wa li'movie zima?
kiini hasa cha mgogoro ni malumbano yalipo kati ya Kagasheki(mbunge) na Amani(meya) juu ya uvunjaji na ujenzi wa soko jipya la Bukoba lkn hii ikiwa ni pamoja na Ushindani katika Siasa yakiwa ni maandalizi ya kuwania nafasi ya kiti cha Ubunge 2015 kwa tiketi ya CCM
 
Ukifuatilia kwa undani utabaini kuwa kinachogombaniwa ni maslahi na siyo haki ya wananchi ambavyo kila mwanasiasa wa Tanzania atataka mwananchi wa kawaida aelewe.Funjo nyingi za wanasiasa na halmashauri au wabunge na madiwani ni maslahi na hofu ya kupinduana katika nyadhifa zao kisiasa. Wabunge mara nyingi kwa vile wako mbali na wananchi hawatamani kuona madiwani wanapata nguvu na umaarufu kwa kuhofia kukosa nafasi zao awamu zijazo.
 
Baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Bukoba wameingia matatani baada ya kuhojiwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kupokea rushwa ili kusaini waraka wa kumng'oa Meya wa Manispaa hiyo Dk Anatory Amani.Tuhuma nyingine ni kuhongwa safari za matembezi nchini Uganda.Kamanda wa TAKUKURU amethibitisha kuhojiwa kwa madiwani hao

Kwa hiyo jamaa wamebainika kula mlungula? Au TAKUKURU nao wamehongwa ili goma lizime?
Manake serikali dhalimu ina watumishi dhalimu. Ukitia pilipili kwenye mboga watu wanatia klorokwini kwenye ugali, Ngoma droo.
 
Back
Top Bottom