Vita ya Baraza la Wafamasia (Pharmacy Council) na TFDA inavyoangamiza Afya za watanzania

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,935
2,000
.
Baraza la wafamasia (Pharmacy Council) liliaanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2002.TFDA ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 1 ya mwaka 2003. Vikiwa ni vyombo viwili vyenye majukumu tofauti.

Kutokana na kung’ang’ania kinachoitwa ulaji na visa yapo majukumu ya TFDA yamechukuliwa na kupelekwa Pharmacy Council ambako sasa afya ya mtanzania haina mwenyewe.

Kitu kilicho cha ajabu ni kuwa TFDA toka ilipoanzishwa ilitengeneza mfumo ambao usajiri wa awali na usimamizi wa awali ulifanywa na wafamasia wa wilaya mpaka mkoa kasha TFDA makao makuu ukishirikina na timu ya afanyakazi wa TFDA katika ngazi mbalimbali. TFDA pia ilianza kujengewa nguvu ya rasilimali watu ambapo ilikuwa na hadi sasa inao wafanyakazi wengi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuanzia zile za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.

Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA; kituko cha ajabu Pharmacy Council hakina wafanyakazi wanaozidi hata 30 kama siyo 20. Tetesi zinasema kisa cha hayo ni kuwa Pharmacy Council walikuwa hawana hela/ulaji waliamua kuchukua ili na wapate ulaji na si kuwaachia TFDA kila kitu. Na la pili kulikuwa na watu wana-madeal ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa na kupitisha dawa zao, hivyo kama zingekuwa chini ya TFDA ilikuwa ni kikwazo kwao. Kwani Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa kigingi kwao.

Kitu cha ajabu ni hiki maduka ya dawa yanafunguliwa hakuna udhibiti, ukaguzi wala usimamizi. Mfano tu Dare s salaam yenye karibu asilimia 80 ya Pharmacy zote nchini ambazo zinakadoriwa kufika kama si kuzidi 500, na maduka kadhaa ya Dawa Muhimu pamoja na utitiri wa maduka ya Dawa Baridi; kwa idadi ya staff waliyonayo pharmacy Council hawawezi kumaliza hata tukiwapa miaka miwili tu kukagua maduka yote ya Dar pekee.

Swali la ziada nini kuhusu ya mikoani? Ni nani anayeweza kuwakamata wafanyabiashara wa dawa bandia na zilizoharibika? Je ni watanzania wangapi wanaaathirika kama si kufa kutokana na kung’ang’ania majukumu ambayo hawayawezi?

Huku mtaani kuna madawa mengi sana feki na yaliyokwisha muda lakini bado yanauzwa.
Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})

Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.
 
Michael Scofield

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
1,225
1,195
Vyombo hivi vyote vya serikali, anaevianzisha ni serikali, Utendaji wake hauendani na maudhui mazima ya kuanzishwa kwake
Serikali inaangalia chombo fulani kimekusanya shillingi ngapi kwa mwaka! kama hakijafikia malengo ndio utaona wanaanzisha chombo kingine.
Hapo unaweza kukuta labda TFDA wako bize na kukamata bidhaa feki, zilizo chini ya kiwango, zilizopita muda wake., lakini wakasahau kupiga mafaini na kukusanya pesa kwa serikali kuu, ndio maana wakaleta mambo ya phamacy council.

Tatizo karibu vyombo vyote vya usimamizi vilivyoundwa na serikali lengo lake au dhumuni kubwa ni kuikusanyia mapato serikali tu, havina usimamizi wowote, pindi tatizo likitokea hakuna kuwajibika...

Kikosi cha zimamoto kinakagua stika za fire, badala ya kukagua kama gari linakizimia moto na kinafanya kazi.. Dar Express liliwaka moto huku stika ya fire ikiwa inamwezi mmoja tangu ikatwe, lakini mtungi wa kuzimia moto hamna.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,204
2,000
Pia ikumbukwe kuwa kuna ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ambaye pia majukumu yake yana overlap na hizo taasisi zingine.

Cha msingi ni kukaa chini na kuainisha majukumu ya kila taasisi
 
Ubungo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
1,236
0
Kumbe ARV fake ziliingizwa sokoni kwa kutumia mkakati huu, sasa nimeelewa.
 
Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,438
2,000
Pia ikumbukwe kuwa kuna ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ambaye pia majukumu yake yana overlap na hizo taasisi zingine.

Cha msingi ni kukaa chini na kuainisha majukumu ya kila taasisi

with this gvt? No! No.! Acha tu watuue weeee! Tukichoka kufa tutawaondoa. Imefikia hataua kwenye utendaji hakuna mzalendo hata mmoja! Mtu anahamishia kitengo kwa rafiki yake ili tu wapige dili.
 
meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,163
2,000
wote mnataka ulaji tu.iwe pharmacy council au TFDA.cha muhimu ni kuanisha mipaka ya ulaji tu.
 
Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
11,014
2,000
MSD kuna vipimo fake vya kupima HIV ! Sijui wamewakusudia nini watanzania.!

Kuhusu Fake HIV test kits nadhani tatizo lilikua a failed system from Korea...

Hili la Madabaida na Nyoni Vs. Ndomondo ni KWELI

Kuna mengine yanakuja, maadam watu wameamua kufunguka, basi hii ni nje ma kwa taifa
 
Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,017
1,225
Pia ikumbukwe kuwa kuna ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ambaye pia majukumu yake yana overlap na hizo taasisi zingine.

Cha msingi ni kukaa chini na kuainisha majukumu ya kila taasisi
Usisahau chombo cha TBA ambacho nacho kinafanya yaleyale wafanyayo TFDA. Bongo bwana, iliumbwa kufanyika kichekesho cha duniani.
 
Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,017
1,225
Kuhusu Fake HIV test kits nadhani tatizo lilikua a failed system from Korea...

Hili la Madabaida na Nyoni Vs. Ndomondo ni KWELI

Kuna mengine yanakuja, maadam watu wameamua kufunguka, basi hii ni nje ma kwa taifa
Tatizo la nyoni alitaka kila anachokiamua yeye lazima kifanyike, alikuwa mungumtu. Akikuagiza kufanya na ukaanza kuuliza maswali ujue tayari amekuandika kwenye kitabu cheusi. Wapo wengi pale wizara ya Afya wenye roha kama ile ambao hawajaondoka na nyoni na bado wanadidimiza wizara ya afya. Wengi wao walisimikwa na nyoni mwenyewe.
 
Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,743
0
Vyombo hivi vyote vya serikali, anaevianzisha ni serikali, Utendaji wake hauendani na maudhui mazima ya kuanzishwa kwake
Serikali inaangalia chombo fulani kimekusanya shillingi ngapi kwa mwaka! kama hakijafikia malengo ndio utaona wanaanzisha chombo kingine.
Hapo unaweza kukuta labda TFDA wako bize na kukamata bidhaa feki, zilizo chini ya kiwango, zilizopita muda wake., lakini wakasahau kupiga mafaini na kukusanya pesa kwa serikali kuu, ndio maana wakaleta mambo ya phamacy council.

Tatizo karibu vyombo vyote vya usimamizi vilivyoundwa na serikali lengo lake au dhumuni kubwa ni kuikusanyia mapato serikali tu, havina usimamizi wowote, pindi tatizo likitokea hakuna kuwajibika...

Kikosi cha zimamoto kinakagua stika za fire, badala ya kukagua kama gari linakizimia moto na kinafanya kazi.. Dar Express liliwaka moto huku stika ya fire ikiwa inamwezi mmoja tangu ikatwe, lakini mtungi wa kuzimia moto hamna.
hapa ndipo wahusika wanapochemka,
 
FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,084
1,225
.

Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA;

Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})

Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.

Hili jambo la Pharmacy Council kusimamia maduka yote ya dawa nchini ni sawa na hakimu kisimamia kesi yake mwenyewe!. Pharmacy Council imejaa wafanyabiashara, na sasa wanameona ni sawa kujisamamia mwenyewe. Na yote hii ni ulafi wa hela. Lakini tofauti na sector nyingine, pharmacy inagusa uhai wa watu, maisha ya watanzania yamewekwa rehani kwa sababu tu watu wachache wanataka hela!

Pharmacy Council ingesimamia nidhamu ya wafamasia na sio zaidi ya hapo. Na sielewi imekuwaje jina Madabida linaibuka kila kunapokuwa na utata wa madawa hapa nchini? ARV, na sasa pharmacy!
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Kwa utendaji wa Serikali hii mambo yote yanafanyika kisiasa, kuna kichekesho kingine ambacho kuna Waraka umetoka juu ofisi ya Waziri Mkuu ukiwaondoa maafisa Afya na Maafisa mipango miji kujihusisha na Upitishaji wa fomu za wafanya biashara wakati wa kupata Leseni eti kwa kisingizio cha kwamba kada hizi zinachelewesha uwekezaji hapa nchini, na hii imechangia kuzagaa kwa biashara zisizo rasmi katika maeneo mengi hapa nchini na kusababisha madhara makubwa kwa walaji ambao ni watanzania wa hali ya chini.
 
Photo me

Member
Nov 11, 2012
7

Hawa Pharmacy council na TFDA viongozi wote ni wafamasia ingawa TFDA inahusisha madaktari na wanasiasa pamoja na wataalamu wengine.Kama vile haitoshi hata MSD viongozi wake ni wafamasia!Waliogawa dawa feki hospitali za serikali ni wafamasia!(Serikali imewaajiri sana wasilete wimbo wa kufichia udhaifu wao eti wako wachache)Pharmacy nyingi mikoani zimesajiliwa kwa majina yao ingawa hawataki kuwepo kuuza dawa badala yake wanaweka wake zao ama watu wasio na ujuzi ili wawalipe kidogo.Kada hii ina vilaza wengi sana na hata humu kwenye mitandao hutawaona wakitoa michango ya maana kwani inasemekana wengi wao ni computerphobic!Nadhani Nyoni asilaumiwe kwani yeye sasa hayupo tena na madudu yanaendelea kuwepo tu!Kuna umuhimu wa kupitia upya mitaala ya hawa jamaa kwani inaonekana hawalisaidii taifa!Mtu akisoma nje akaja hapa atasumbuka kupata usajili na atanyanyaswa mradi tu wabaki wao waliosoma sana hasa Muhimbili!Ingawa wengi waliohuku mikoani wako empty upstairs!wamebaki kuwa wanasiasa tu na wapiga dili za manunuzi hewa ya dawa!
 
Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,070
1,750
inasikitisha sana inapofika mahala hadi msd kusambaza dawa feki tutapona kweli
 
assuredly4

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
1,216
1,195
.
Baraza la wafamasia (Pharmacy Council) liliaanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2002.TFDA ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 1 ya mwaka 2003. Vikiwa ni vyombo viwili vyenye majukumu tofauti.
Suala hili naona halina ubishi kwani ni taasisi za serikali

Kutokana na kung’ang’ania kinachoitwa ulaji na visa yapo majukumu ya TFDA yamechukuliwa na kupelekwa Pharmacy Council ambako sasa afya ya mtanzania haina mwenyewe.
hili naona halina ukweli na mtoa mada anaonekana ni mtumishi wa TFDA anayetaka kuupotosha umma badala ya kuwaambia watanzania ukweli wa nn kilitokea.kuanzishwa chombo chochote cha Serikali huwa lazima Baraza la mawaziri na rais mwenyewe akubali. vilevile hata TFDA/Pharmacy Council vimundwa hivyo na vinaweza kufutwa kwa maamuzi ya serikali. Afya ya watanzania ina mwenyewe kwani ni waziri wa afya akisaidiwa na watendaji wake pamoja na taasisi zake.Ukisoma sheria mbili za TFDA na Pharmacy council utaona TFDA wana jukumu la kusajili na kutoa vibali kwa dawa zote, vifaa tiba, vipodozi vyote na vyakula vyote lakini Pharmacy Council imepewa jukumu la kusajili viuo vya kutolea hudma za dawa yaani famasi zote ikiwemo za hospitali na maduka ya dawa muhimu. lengo kubwa ya sheria hizi ilikuwa kuepusha mgongano wa maslahi ambayo ayngetokea endapo TFDA pekee ndio wangekuwa wanafanya kazi zote hizi.

Kitu kilicho cha ajabu ni kuwa TFDA toka ilipoanzishwa ilitengeneza mfumo ambao usajiri wa awali na usimamizi wa awali ulifanywa na wafamasia wa wilaya mpaka mkoa kasha TFDA makao makuu ukishirikina na timu ya afanyakazi wa TFDA katika ngazi mbalimbali. TFDA pia ilianza kujengewa nguvu ya rasilimali watu ambapo ilikuwa na hadi sasa inao wafanyakazi wengi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuanzia zile za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.
je hao walioko TFDA wana utaalamu gani ambao baraza la wafamasia hawana, nimepata taarifa kuwa baraza la famasi nao wanafanya kazi kwa kuwatumia wataalam kuanzia ngazi ya wilaya. hapa naona mleta mada anajichanganya na aya inayofuata kwani kama TFDA ina watumishi wa kutosha mbona wanatumia watalaam walioko wilayani?

Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA; kituko cha ajabu Pharmacy Council hakina wafanyakazi wanaozidi hata 30 kama siyo 20. Tetesi zinasema kisa cha hayo ni kuwa Pharmacy Council walikuwa hawana hela/ulaji waliamua kuchukua ili na wapate ulaji na si kuwaachia TFDA kila kitu. Na la pili kulikuwa na watu wana-madeal ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa na kupitisha dawa zao, hivyo kama zingekuwa chini ya TFDA ilikuwa ni kikwazo kwao. Kwani Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa kigingi kwao.
si kweli wamechukua bali wamepewa na serikali ndio maana sheria ilipitishwa na bunge la tanzania. kuhusu eti famasi hawakuwa na ulaji nalo naona liko biased kwasababu mm nijuavyo watumishi wote wanalipwa na serikali sasa ulaji ulikosekanaje? vilevile kuhusu idadi ya watumishi kuwa 30 sioni tatizo kwani sio wakati wote taasisi ikiwa na watu wengi ndipo inakuwa na utendaji kazi mzuri. hebu jiulize TRA inawafanyakazi wangapi, mbona bado hamridhiki kuwa wanakusanya mapato ya serikali kwa ufanisi. ukifutilia utagundua hata TFDA ilianza na watumishi wachache lkn leo nadhani wako zaidi ya 100. kuhusu utekelezaji wa kazi walizopewa kwa mtizamo wangu sioni kama watashindwa kwasababu nimearifiwa bado wanatumia wafamasia walioko mikoani na wilayani kufanya ukaguzi na kuwasilisha taarifa kwenye ofisi zao. wafamasia wanasajiliwa na baraza la wafamasia kwa maoni yangu nadhani watafanya vizuri zaidi na kwa umakini wakijua wakidanganya wanaweza kufutiwa usajili na baraza tofauti na ilivyokuwa kwa TFDA.kuhusu madili ya kuanzisha maduka makubwa hilo nalo linahiaji ushahidi, ungetuletea taarifa ya wafanyakazi walioanzisha maduka makubwa baada ya madaraka ya kusajili maduka kuhamishiwa na serikali katika baraza la wafamasia hapo mm ningekuelewa, bila data nitakuhesabu ni mleta umbeya tu.

Kitu cha ajabu ni hiki maduka ya dawa yanafunguliwa hakuna udhibiti, ukaguzi wala usimamizi. Mfano tu Dare s salaam yenye karibu asilimia 80 ya Pharmacy zote nchini ambazo zinakadoriwa kufika kama si kuzidi 500, na maduka kadhaa ya Dawa Muhimu pamoja na utitiri wa maduka ya Dawa Baridi; kwa idadi ya staff waliyonayo pharmacy Council hawawezi kumaliza hata tukiwapa miaka miwili tu kukagua maduka yote ya Dar pekee.
mm nadhani tuwe objective tusiwe subjective, ubakaji ni kosa la jinai lkn mbona watu wanaendelea kubaka je serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake, hili sio kweli, ndiyo maana hatua zinachukuliwa kwa wahusika. mm naamini hata TFDA enzi zao hawakufika maeneo yote na maduka yaliendelea kufunguliwa kana kwamba hawapo. kwa mawazo yangu utii wa sheria bila shurti una mambo mengi na utekelezaji hufanyika hatua kwa hatua. kwa mfano wiki hii nimesikia baraza la wafamasia linaendesha operesheni ya kufunga maduka yanayokiuka sheria, nadhani ni hatua ya kupongezwa. badala ya kuvilaumu vyombo vya serikali wakati mwingine tuvishauri namna bora ya kutekeleza sheria. mfano ww mleta mada ninaamini pale unapoishi umeshuhudia kuna watu wamefungua maduka ya dawa bila vibali vya baraza la wafamasia, je umetoa taarifa kwa baraza ili hatua zichukuliwe, kama sivyo, ukiwa raia wa nchi hii umehatarisha usalama wa familia yako na jamii inayokuzunguka kwani kuna siku utakuwa ofisini mwanafamilia ataugua wataenda kununua dawa feki na kutumia na kupata madhara

Swali la ziada nini kuhusu ya mikoani? Ni nani anayeweza kuwakamata wafanyabiashara wa dawa bandia na zilizoharibika? Je ni watanzania wangapi wanaaathirika kama si kufa kutokana na kung’ang’ania majukumu ambayo hawayawezi?
mm nafikiri mleta mada hajazisoma sheria za TFDA na Baraza la wafamasia bali kutokana na yeye kukosa ulaji, huenda aliokuwa anaupata kupitia haya maduka ya dawa yaliyohamia baraza la wafamasia ndiyo maana anapiga kelele zisizo na hata chembe ya ukweli. ukisoma sheria utaona jukumu la ubora na usalama wa dawa bado liko TFDA, yeye angekuja hapa akatuambia akiwa mmoja wa wafanyakazi wa TFDA amefanya nn kuzuia dawa bandia kutengenezwa nchini, kuingia na kuuzwa kwa ndugu zetu mikoani? wingi wa watumishi wa TFDA umesaidiaje kuzuia dawa feki/bandia za ARV, malaria na nyinginezo kuuzwa nchini.kwa upande wangu siwezi kuwalaumu TFDA kwani dawa bandia ni tatizo la kidunia, kama ilivyo kwa makosa ya jinai, la msingi ni kuongeza jitihada kupambana na makosa hayo

Huku mtaani kuna madawa mengi sana feki na yaliyokwisha muda lakini bado yanauzwa.
hili ni jukumu la TFDA kisheria kama hapo juu panavyofafanua, soma sheria zote mbili utapata muktadha halisi

Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})
tupatie ushahidi ili tuweke kwenye kumbukumbu kwa matumizi ya kisiasa miaka ijayo endapo wataendelea kugombea ili tuyakomboe baadhi ya majimbo

Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.
ebu tafuta majadiliano ya bunge, kisha yalete hapa ili watu tupate fursa ya kuchambua kila neno na kujua ukweli,
 
assuredly4

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
1,216
1,195
.

Baraza la wafamasia (Pharmacy Council) liliaanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2002.TFDA ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 1 ya mwaka 2003. Vikiwa ni vyombo viwili vyenye majukumu tofauti.

Kutokana na kung'ang'ania kinachoitwa ulaji na visa yapo majukumu ya TFDA yamechukuliwa na kupelekwa Pharmacy Council ambako sasa afya ya mtanzania haina mwenyewe.

Kitu kilicho cha ajabu ni kuwa TFDA toka ilipoanzishwa ilitengeneza mfumo ambao usajiri wa awali na usimamizi wa awali ulifanywa na wafamasia wa wilaya mpaka mkoa kasha TFDA makao makuu ukishirikina na timu ya afanyakazi wa TFDA katika ngazi mbalimbali. TFDA pia ilianza kujengewa nguvu ya rasilimali watu ambapo ilikuwa na hadi sasa inao wafanyakazi wengi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuanzia zile za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.

Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA; kituko cha ajabu Pharmacy Council hakina wafanyakazi wanaozidi hata 30 kama siyo 20. Tetesi zinasema kisa cha hayo ni kuwa Pharmacy Council walikuwa hawana hela/ulaji waliamua kuchukua ili na wapate ulaji na si kuwaachia TFDA kila kitu. Na la pili kulikuwa na watu wana-madeal ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa na kupitisha dawa zao, hivyo kama zingekuwa chini ya TFDA ilikuwa ni kikwazo kwao. Kwani Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa kigingi kwao.

Kitu cha ajabu ni hiki maduka ya dawa yanafunguliwa hakuna udhibiti, ukaguzi wala usimamizi. Mfano tu Dare s salaam yenye karibu asilimia 80 ya Pharmacy zote nchini ambazo zinakadoriwa kufika kama si kuzidi 500, na maduka kadhaa ya Dawa Muhimu pamoja na utitiri wa maduka ya Dawa Baridi; kwa idadi ya staff waliyonayo pharmacy Council hawawezi kumaliza hata tukiwapa miaka miwili tu kukagua maduka yote ya Dar pekee.

Swali la ziada nini kuhusu ya mikoani? Ni nani anayeweza kuwakamata wafanyabiashara wa dawa bandia na zilizoharibika? Je ni watanzania wangapi wanaaathirika kama si kufa kutokana na kung'ang'ania majukumu ambayo hawayawezi?

Huku mtaani kuna madawa mengi sana feki na yaliyokwisha muda lakini bado yanauzwa.
Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})

Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.

mm naona nijaribu kuchangia mada hii ili kupanua mjadala kwa wana jf /gt

1. Baraza la wafamasia (Pharmacy Council) na TFDA ni taasisi za serikali

2. Kutokana na kung'ang'ania kinachoitwa ulaji na visa yapo majukumu ya TFDA yamechukuliwa na kupelekwa Pharmacy Council ambako sasa afya ya mtanzania haina mwenyewe.

hili naona halina ukweli na mtoa mada anaonekana ni mtumishi wa TFDA anayetaka kuupotosha umma badala ya kuwaambia watanzania ukweli wa nn kilitokea.kuanzishwa chombo chochote cha Serikali huwa lazima Baraza la mawaziri na rais mwenyewe akubali. vilevile hata TFDA/Pharmacy Council vimeundwa hivyo na vinaweza kufutwa kwa maamuzi ya serikali. Afya ya watanzania ina mwenyewe kwani ni waziri wa afya akisaidiwa na watendaji wake pamoja na taasisi zake.Ukisoma sheria mbili za TFDA na Pharmacy council utaona TFDA wana jukumu la kusajili na kutoa vibali kwa dawa zote, vifaa tiba, vipodozi vyote na vyakula vyote lakini Pharmacy Council imepewa jukumu la kusajili vituo vya kutolea huduma za dawa yaani famasi zote ikiwemo za hospitali na maduka ya dawa muhimu.

kwa mtizamo wangu uwepo wa sheria hizi ni kuepusha mgongano wa maslahi ambao ungetokea endapo TFDA pekee ndio wangekuwa wanafanya kazi zote hizi.

3. Kitu kilicho cha ajabu ni kuwa TFDA toka ilipoanzishwa ilitengeneza mfumo ambao usajiri wa awali na usimamizi wa awali ulifanywa na wafamasia wa wilaya mpaka mkoa kasha TFDA makao makuu ukishirikina na timu ya afanyakazi wa TFDA katika ngazi mbalimbali. TFDA pia ilianza kujengewa nguvu ya rasilimali watu ambapo ilikuwa na hadi sasa inao wafanyakazi wengi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuanzia zile za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.

je hao walioko TFDA wana utaalamu gani ambao baraza la wafamasia hawana, nimepata taarifa kuwa baraza la famasi nao wanafanya kazi kwa kuwatumia wataalam kuanzia ngazi ya wilaya. hapa naona mleta mada anajichanganya na aya inayofuata kwani kama TFDA ina watumishi wa kutosha mbona wanatumia watalaam walioko wilayani?

4. Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA; kituko cha ajabu Pharmacy Council hakina wafanyakazi wanaozidi hata 30 kama siyo 20. Tetesi zinasema kisa cha hayo ni kuwa Pharmacy Council walikuwa hawana hela/ulaji waliamua kuchukua ili na wapate ulaji na si kuwaachia TFDA kila kitu. Na la pili kulikuwa na watu wana-madeal ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa na kupitisha dawa zao, hivyo kama zingekuwa chini ya TFDA ilikuwa ni kikwazo kwao. Kwani Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa kigingi kwao.

Si kweli wamechukua majukumu ya TFDA bali wamepewa na serikali Kisheria ndio maana sheria ilipitishwa na bunge la tanzania. kuhusu eti baraza la wafamasia hawakuwa na ulaji nalo naona liko biased kwasababu mm nijuavyo watumishi wote wanalipwa na serikali sasa ulaji ulikosekanaje?

vilevile kuhusu idadi ya watumishi kuwa 30 sioni tatizo kwani sio wakati wote taasisi ikiwa na watu wengi ndipo inakuwa na utendaji kazi mzuri. hebu jiulize TRA inawafanyakazi wangapi, mbona bado haturidhiki na ukusanyaji wa mapato ya serikali na tunaona hayana ufanisi. ukifutilia utagundua hata TFDA ilianza na watumishi wachache lkn leo wamefikia hapo walipo. kuhusu utekelezaji wa kazi walizopewa kwa mtizamo wangu sioni kama watashindwa kwasababu nimepata taarifa kuwa nao wanatumia wafamasia walioko mikoani na wilayani kufanya ukaguzi na kuwasilisha taarifa kwenye ofisi zao. wafamasia wanasajiliwa na baraza la wafamasia kwa maoni yangu nadhani watafanya vizuri zaidi na kwa umakini wakijua wakidanganya wanaweza kufutiwa usajili na baraza tofauti na ilivyokuwa kwa TFDA.

kuhusu madili ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa hilo nalo linahitaji ushahidi, ungetuletea taarifa ya wafanyakazi wa baraza la wafamasia au ndugu zao walioanzisha maduka makubwa baada ya madaraka ya kusajili maduka kuhamishiwa na serikali katika baraza la wafamasia hapo mm ningekuelewa, bila data nitakuhesabu ni mleta umbeya tu. data utakazoleta zianishe je hawakufuata sheria, kuna kifungu cha sheria wanachokiuka lakini hawachukuliwi hatua n.k.

5. Kitu cha ajabu ni hiki maduka ya dawa yanafunguliwa hakuna udhibiti, ukaguzi wala usimamizi. Mfano tu Dare s salaam yenye karibu asilimia 80 ya Pharmacy zote nchini ambazo zinakadoriwa kufika kama si kuzidi 500, na maduka kadhaa ya Dawa Muhimu pamoja na utitiri wa maduka ya Dawa Baridi; kwa idadi ya staff waliyonayo pharmacy Council hawawezi kumaliza hata tukiwapa miaka miwili tu kukagua maduka yote ya Dar pekee.
mm nadhani tuwe objective tusiwe subjective, ubakaji ni kosa la jinai lkn mbona watu wanaendelea kubaka je serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake, hili sio kweli, ndiyo maana hatua zinachukuliwa kwa wahusika. TFDA ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha ubora na usalama wa dawa kwa walaji nilitarajia wawe wanashinda mitaani kuchukua dawa katika maduka yote yasiyo na kibali cha kufanya biashara hiyo kutoka baraza la wafamasia. mm nashawishika kusema hata TFDA enzi zao hawakufika maeneo yote na maduka yaliendelea kufunguliwa kana kwamba hawapo.

kwa mawazo yangu utii wa sheria bila shurti una mambo mengi na utekelezaji hufanyika hatua kwa hatua. kwa mfano wiki hii nimesikia baraza la wafamasia linaendesha operesheni ya kufunga maduka yanayokiuka sheria, nadhani ni hatua ya kupongezwa. badala ya kuvilaumu vyombo vya serikali wakati mwingine tuvishauri namna bora ya kutekeleza sheria. mfano ww mleta mada ninaamini pale unapoishi umeshuhudia kuna watu wamefungua maduka ya dawa bila vibali vya baraza la wafamasia, je umetoa taarifa kwa baraza ili hatua zichukuliwe, kama sivyo, ukiwa raia wa nchi hii umehatarisha usalama wa familia yako na jamii inayokuzunguka kwani kuna siku utakuwa ofisini mwanafamilia ataugua wataenda kununua dawa feki na kutumia na kupata madhara.

6. Swali la ziada nini kuhusu ya mikoani? Ni nani anayeweza kuwakamata wafanyabiashara wa dawa bandia na zilizoharibika? Je ni watanzania wangapi wanaaathirika kama si kufa kutokana na kung'ang'ania majukumu ambayo hawayawezi?
mm nafikiri mleta mada hajazisoma sheria za TFDA na Baraza la wafamasia bali kutokana na yeye kukosa ulaji, huenda aliokuwa anaupata kupitia haya maduka ya dawa yaliyohamia baraza la wafamasia ndiyo maana anapiga kelele zisizo na hata chembe ya ukweli. ukisoma sheria utaona jukumu la ubora na usalama wa dawa bado liko TFDA, yeye angekuja hapa akatuambia akiwa mmoja wa wafanyakazi wa TFDA amefanya nn kuzuia dawa bandia kutengenezwa nchini, kuingia na kuuzwa kwa ndugu zetu mikoani? wingi wa watumishi wa TFDA umesaidiaje kuzuia dawa feki/bandia za ARV, malaria na nyinginezo kuuzwa nchini.kwa upande wangu siwezi kuwalaumu TFDA kwani dawa bandia ni tatizo la kidunia, kama ilivyo kwa makosa ya jinai, la msingi ni kuongeza jitihada kupambana na makosa hayo kwa kushirikiano na vyombo vingine kama TBS, Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali .

7. Huku mtaani kuna madawa mengi sana feki na yaliyokwisha muda lakini bado yanauzwa.
hili ni jukumu la TFDA kisheria kama hapo juu panavyofafanua, soma sheria zote mbili utapata muktadha halisi

8. Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})
tupatie ushahidi ili tuweke kwenye kumbukumbu kwa matumizi ya kisiasa miaka ijayo endapo wataendelea kugombea ili tuyakomboe baadhi ya majimbo

9. Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.
ebu tafuta majadiliano ya bunge, kisha yalete hapa ili watu tupate fursa ya kuchambua kila neno na kujua ukweli,

ningependa kushauri watanzania tutoe taarifa za uhalifu kwenye vyombo vinavyohusika TFDA,TBS,FCC, Baraza la wafamasia na polisi ili tupunguze makosa ya jinai yakiwemo uuzaji wa dawa bandia. kuna baadhi yetu maeneo tunayoishi kuna viwanda vya kutengeneza dawa vilivyojengwa ndani ya nyumba za watu, tuwataje ili washughulikiwe.hii ni moja ya tabia ya wapangaji wa kichina/kihindi, ndio maana china adhabu yao ni kunyonga tu ili kuwapunguza wahalifu. Hakuna nchi yoyote duniani iliyofanikiwa kudhibiti makosa ya jinai bila wananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu
 
Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
11,014
2,000
Tatizo la nyoni alitaka kila anachokiamua yeye lazima kifanyike, alikuwa mungumtu. Akikuagiza kufanya na ukaanza kuuliza maswali ujue tayari amekuandika kwenye kitabu cheusi. Wapo wengi pale wizara ya Afya wenye roha kama ile ambao hawajaondoka na nyoni na bado wanadidimiza wizara ya afya. Wengi wao walisimikwa na nyoni mwenyewe.
yule mama ni shetani mtu kabisa

her effects zitatukosti for decades
 
kuna baadhi ya vitu unavyoomba kama ushahidi as if you are not a Tanzanian....

maelezo yako mengi yamekaa ki system zaidi kuliko reality iliyo kwenye ground... SORT OF THIS IS HOW IT IS WRITTEN, vua koti lako vaa la reality mkuu
 
Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,595
1,195
Tatizo la nyoni alitaka kila anachokiamua yeye lazima kifanyike, alikuwa mungumtu. Akikuagiza kufanya na ukaanza kuuliza maswali ujue tayari amekuandika kwenye kitabu cheusi. Wapo wengi pale wizara ya Afya wenye roha kama ile ambao hawajaondoka na nyoni na bado wanadidimiza wizara ya afya. Wengi wao walisimikwa na nyoni mwenyewe.

Hivi Nyoni yu wapi siku hizi, ati kapewa ubalozi nje?????
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom