Vita ya Baraza la Wafamasia (Pharmacy Council) na TFDA inavyoangamiza Afya za watanzania

Kuna haja ya kutumia mwarobaini, mkwinini, n.k kwa kuwa hizi dawa zinazopikwa hapa nyumbani na zinazoletwa na meli ni janga la kitaifa.
Ikiwa kama watu wanalishwa panadol za unga wa ngano, ARV bandia n.k tutarajie wakina Dr Ndodi wengi zaidi, kwa kuwa udhaifu unaoelezwa humu ndio mtaji wa biashara yao.
 
Pharmacy board na Tfda zote ni taasisi chini ya Wizara moja, tunachotaka ni ushirikiano , kama mnagombania ukubwa hayo ni mambo yenu , fuateni sheria zinazowaongoza , msiwafanye wafanyabiashara ya dawa kama ngazi yenu ya kupandia juu , bila kushirikiana na wauza dawa kila siku itakuwa tabu , kama tfda ndiyo inasimamia mafunzo na pharmacy board ni wakaguzi sasa ugomvi wa nini ?
 
Kama ni kweli baadhi ya majukumu yamepelekwa Baraza la wafamasia kutoka TFDA ni jambo la kuipongeza Serikali, maana nina hasira na hawa jamaa TFDA. Kama tungekuwa China, hawa jamaa wangekuwa marehem siku nyingi, maana haiwezekani, dawa kama ARV feki zitengenezwe hapa hapa nchini, zipelekwe MSD, zisambazwe hospitalini na mgonjwa huko Mara ndio agundue kuwa amepewa dawa za rangi mbili tofauti kama wali, walikuwa wapi???? Majuzi juzi tena vitendanishi feki vya ARV MSD?? nini kazi yao kwa mujibu wa sheria? kufungua maduka??? Mbona FDA ya marekani ambayo naamini TFDA imenakili huko mfumo, hawahusiki na maduka?? Badala ya TFDA kuhakiki ubora wa dawa, mnataka maduka so what????
 
Serikali ikae na taasisi hizi mbili na kila moja ifanye kazi kwa maslahi ya wananchi. Sheria ya 2003 ya TFDA inatamka majukumu makuu ya kuanzishwa TFDA ni "to control safety, quality and efficacy of food, drugs, cosmetics and medical devices". Sifahamu ya Baraza la Wafamasia sheria mpya. Hivyo, TFDA wajizatiti kuangalia dawa feki maana ndio jukumu lao kuu na si kufungua maduka.
Kama kuna taasisi itakayolaumiwa na wananchi ni TFDA, maana ndio waanzilishi wa ADDO, ati mtu anafundishwa kwa siku 20 anaruhusiwa kuuza dawa hata zinazoitaji cheti cha daktari, Umeona wapi upumbafu kama huu??? lakini TFDA wameruhusu kwa maslahi binafsi, na huenda mtoa mada na TFDA wanasikitika kwa sababu ya kukosa ulaji huu, kama kweli serikali imepeleka masula ya maduka Baraza la wafamasia.
 
ebu tafuta majadiliano ya bunge, kisha yalete hapa ili watu tupate fursa ya kuchambua kila neno na kujua ukweli,

Wewe mbona unatia aibu, si unafanya kazi karibu na ofisi za Bunge, unaonashida gani kwenda kuomba ansard? Mtu wa Songea na Tabora wasemaje?
Yaani, hata ku-google unaona uvivu?

Mimi kutokujibu hoja zako si kwamba zinamashiko bali ziko too low to be replied.
 
kuna baadhi ya vitu unavyoomba kama ushahidi as if you are not a Tanzanian....

maelezo yako mengi yamekaa ki system zaidi kuliko reality iliyo kwenye ground... SORT OF THIS IS HOW IT IS WRITTEN, vua koti lako vaa la reality mkuu

Mkuu na furahi kwasababu nawe umemwona. Japo mimi nafikiri ni kidamper wa watu fulani anataka kuwatetea lakini anahoja za kitoto.

Msome vizuri utagundua hofu na hasira alivyonavyo, pia utagundua namna fulani ya kujifanya hajui kabisa.
 
Pharmacy board na Tfda zote ni taasisi chini ya Wizara moja, tunachotaka ni ushirikiano , kama mnagombania ukubwa hayo ni mambo yenu , fuateni sheria zinazowaongoza , msiwafanye wafanyabiashara ya dawa kama ngazi yenu ya kupandia juu , bila kushirikiana na wauza dawa kila siku itakuwa tabu , kama tfda ndiyo inasimamia mafunzo na pharmacy board ni wakaguzi sasa ugomvi wa nini ?[/ B]

Kwasasa mafunzo na mazagaza yote yanayohusika na Maduka ya Dawa yako chini ya Pharmacy Council.

Ujinga mkubwa tunaolalamikia ni huu. Pharmacy Council kuchukua jukumu ambalo hawana rasilimali watu na vifaa toka taasisi iliyokwisha kujijenga na inaendelea kujijenga kwa kasi. Matokeo yake ni kama ule ujinga wa kuhamisha waalimu toka shule 5 za sekondari zilizokuwapo awali na kupeleka kwenye shule 60 za kata mlizofungua karibuni .Eti mkiwa na matumaini ya kuinua kiwango cha elimu...ni uzuzu tu.

Angalia wanafanya ukaguzi sasa, umewahi kufikiria juu ya loyality ya hao team staff wa kuazima? Ni kwa kiasi gani huwezi kuwa na ufanisi kwa kutegemea mainly wafanyakazi wa kuazima?

Kumbuka staff wa Council hawafiki ishirini.
 
Naamini wewe ni "low thinker" ni bora ungeenda kwenye facebook. Assuredly kaweka facts, weka facts zako pia, hapa jukwaani ni sehemu ya porojo. Tuambie majukumu ya TFDA ni nini??? na Baraza la Wafamasia ni nini?? ikiwezekana weka sheria zao mbili tuzijadili. Nina vyoona, unalalamika baada ya mabadiliko haya yaliyokuwa yanawapa ulaji. Kuzagaa kwa dawa feki mitaani ni jukumu la TFDA au Baraza la Wafamasia??? Kuzagaa kwa ARV feki ni TFDA au Baraza la Wafamasia?? tushawishi with facts, hapa ni jukwaa huru were people dare to talk openly!! kama hao watumishi walikuwa na madeal, tuambie ni maduka yapi wamefungua na yanamilikiwa na nani, ili tujadili.
 
Mnyamahodzo! mbona unajidhalilisha na kuonyesha jinsi gani unaumia kwa mabadiliko hayo na kukosa ulaji???,. Hapo juu ulisema, TFDA ilijijengea mfumo wa kutoka wilayani, mikoani hadi makao makuu; tuelimishe, hao staff wa wilayani ni wa TFDA au halmashauri?? si ni sawa tu na Baraza la wafamasia kutumia staff wa halmashauri au manispaa za Dar??? Isitoshe, wote wako wizara ya afya, na ni jukumu la wizara husika kupeleka watumishi na ninaamini wizara ya afya inaweza hata kuhamisha staff kutoka TFDA na kupeleka Baraza. Nilitegemea TFDA washukuru maana wamepunguziwa majukumu,
Kwasasa mafunzo na mazagaza yote yanayohusika na Maduka ya Dawa yako chini ya Pharmacy Council.

Ujinga mkubwa tunaolalamikia ni huu. Pharmacy Council kuchukua jukumu ambalo hawana rasilimali watu na vifaa toka taasisi iliyokwisha kujijenga na inaendelea kujijenga kwa kasi. Matokeo yake ni kama ule ujinga wa kuhamisha waalimu toka shule 5 za sekondari zilizokuwapo awali na kupeleka kwenye shule 60 za kata mlizofungua karibuni .Eti mkiwa na matumaini ya kuinua kiwango cha elimu...ni uzuzu tu.

Angalia wanafanya ukaguzi sasa, umewahi kufikiria juu ya loyality ya hao team staff wa kuazima? Ni kwa kiasi gani huwezi kuwa na ufanisi kwa kutegemea mainly wafanyakazi wa kuazima?

Kumbuka staff wa Council hawafiki ishirini.
 
kuna baadhi ya vitu unavyoomba kama ushahidi as if you are not a Tanzanian....

maelezo yako mengi yamekaa ki system zaidi kuliko reality iliyo kwenye ground... SORT OF THIS IS HOW IT IS WRITTEN, vua koti lako vaa la reality mkuu

sasa hivi akina nyoni na kundi lake wameondoka, kinachowashinda kuperform/kutekeleza vizuri majukumu yenu kama TFDA/PC ni nini? ninyi ni taasisi za serikali acheni majungu fanyeni kazi ss tutawapongeza
 
.
Baraza la wafamasia (Pharmacy Council) liliaanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2002.TFDA ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 1 ya mwaka 2003. Vikiwa ni vyombo viwili vyenye majukumu tofauti.

Kutokana na kung’ang’ania kinachoitwa ulaji na visa yapo majukumu ya TFDA yamechukuliwa na kupelekwa Pharmacy Council ambako sasa afya ya mtanzania haina mwenyewe.

Kitu kilicho cha ajabu ni kuwa TFDA toka ilipoanzishwa ilitengeneza mfumo ambao usajiri wa awali na usimamizi wa awali ulifanywa na wafamasia wa wilaya mpaka mkoa kasha TFDA makao makuu ukishirikina na timu ya afanyakazi wa TFDA katika ngazi mbalimbali. TFDA pia ilianza kujengewa nguvu ya rasilimali watu ambapo ilikuwa na hadi sasa inao wafanyakazi wengi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuanzia zile za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.

Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA; kituko cha ajabu Pharmacy Council hakina wafanyakazi wanaozidi hata 30 kama siyo 20. Tetesi zinasema kisa cha hayo ni kuwa Pharmacy Council walikuwa hawana hela/ulaji waliamua kuchukua ili na wapate ulaji na si kuwaachia TFDA kila kitu. Na la pili kulikuwa na watu wana-madeal ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa na kupitisha dawa zao, hivyo kama zingekuwa chini ya TFDA ilikuwa ni kikwazo kwao. Kwani Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa kigingi kwao.

Kitu cha ajabu ni hiki maduka ya dawa yanafunguliwa hakuna udhibiti, ukaguzi wala usimamizi. Mfano tu Dare s salaam yenye karibu asilimia 80 ya Pharmacy zote nchini ambazo zinakadoriwa kufika kama si kuzidi 500, na maduka kadhaa ya Dawa Muhimu pamoja na utitiri wa maduka ya Dawa Baridi; kwa idadi ya staff waliyonayo pharmacy Council hawawezi kumaliza hata tukiwapa miaka miwili tu kukagua maduka yote ya Dar pekee.

Swali la ziada nini kuhusu ya mikoani? Ni nani anayeweza kuwakamata wafanyabiashara wa dawa bandia na zilizoharibika? Je ni watanzania wangapi wanaaathirika kama si kufa kutokana na kung’ang’ania majukumu ambayo hawayawezi?

Huku mtaani kuna madawa mengi sana feki na yaliyokwisha muda lakini bado yanauzwa.
Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})

Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.

In short Pharmacy council inasimamia profession (Practice) wakati TFDA inadeal na Products...try to be informed before gossiping...
 
mm naona nijaribu kuchangia mada hii ili kupanua mjadala kwa wana jf /gt

1. Baraza la wafamasia (Pharmacy Council) na TFDA ni taasisi za serikali

2. Kutokana na kung’ang’ania kinachoitwa ulaji na visa yapo majukumu ya TFDA yamechukuliwa na kupelekwa Pharmacy Council ambako sasa afya ya mtanzania haina mwenyewe.

hili naona halina ukweli na mtoa mada anaonekana ni mtumishi wa TFDA anayetaka kuupotosha umma badala ya kuwaambia watanzania ukweli wa nn kilitokea.kuanzishwa chombo chochote cha Serikali huwa lazima Baraza la mawaziri na rais mwenyewe akubali. vilevile hata TFDA/Pharmacy Council vimeundwa hivyo na vinaweza kufutwa kwa maamuzi ya serikali. Afya ya watanzania ina mwenyewe kwani ni waziri wa afya akisaidiwa na watendaji wake pamoja na taasisi zake.Ukisoma sheria mbili za TFDA na Pharmacy council utaona TFDA wana jukumu la kusajili na kutoa vibali kwa dawa zote, vifaa tiba, vipodozi vyote na vyakula vyote lakini Pharmacy Council imepewa jukumu la kusajili vituo vya kutolea huduma za dawa yaani famasi zote ikiwemo za hospitali na maduka ya dawa muhimu.

kwa mtizamo wangu uwepo wa sheria hizi ni kuepusha mgongano wa maslahi ambao ungetokea endapo TFDA pekee ndio wangekuwa wanafanya kazi zote hizi.

3. Kitu kilicho cha ajabu ni kuwa TFDA toka ilipoanzishwa ilitengeneza mfumo ambao usajiri wa awali na usimamizi wa awali ulifanywa na wafamasia wa wilaya mpaka mkoa kasha TFDA makao makuu ukishirikina na timu ya afanyakazi wa TFDA katika ngazi mbalimbali. TFDA pia ilianza kujengewa nguvu ya rasilimali watu ambapo ilikuwa na hadi sasa inao wafanyakazi wengi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuanzia zile za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.

je hao walioko TFDA wana utaalamu gani ambao baraza la wafamasia hawana, nimepata taarifa kuwa baraza la famasi nao wanafanya kazi kwa kuwatumia wataalam kuanzia ngazi ya wilaya. hapa naona mleta mada anajichanganya na aya inayofuata kwani kama TFDA ina watumishi wa kutosha mbona wanatumia watalaam walioko wilayani?

4. Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA; kituko cha ajabu Pharmacy Council hakina wafanyakazi wanaozidi hata 30 kama siyo 20. Tetesi zinasema kisa cha hayo ni kuwa Pharmacy Council walikuwa hawana hela/ulaji waliamua kuchukua ili na wapate ulaji na si kuwaachia TFDA kila kitu. Na la pili kulikuwa na watu wana-madeal ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa na kupitisha dawa zao, hivyo kama zingekuwa chini ya TFDA ilikuwa ni kikwazo kwao. Kwani Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa kigingi kwao.

Si kweli wamechukua majukumu ya TFDA bali wamepewa na serikali Kisheria ndio maana sheria ilipitishwa na bunge la tanzania. kuhusu eti baraza la wafamasia hawakuwa na ulaji nalo naona liko biased kwasababu mm nijuavyo watumishi wote wanalipwa na serikali sasa ulaji ulikosekanaje?

vilevile kuhusu idadi ya watumishi kuwa 30 sioni tatizo kwani sio wakati wote taasisi ikiwa na watu wengi ndipo inakuwa na utendaji kazi mzuri. hebu jiulize TRA inawafanyakazi wangapi, mbona bado haturidhiki na ukusanyaji wa mapato ya serikali na tunaona hayana ufanisi. ukifutilia utagundua hata TFDA ilianza na watumishi wachache lkn leo wamefikia hapo walipo. kuhusu utekelezaji wa kazi walizopewa kwa mtizamo wangu sioni kama watashindwa kwasababu nimepata taarifa kuwa nao wanatumia wafamasia walioko mikoani na wilayani kufanya ukaguzi na kuwasilisha taarifa kwenye ofisi zao. wafamasia wanasajiliwa na baraza la wafamasia kwa maoni yangu nadhani watafanya vizuri zaidi na kwa umakini wakijua wakidanganya wanaweza kufutiwa usajili na baraza tofauti na ilivyokuwa kwa TFDA.

kuhusu madili ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa hilo nalo linahitaji ushahidi, ungetuletea taarifa ya wafanyakazi wa baraza la wafamasia au ndugu zao walioanzisha maduka makubwa baada ya madaraka ya kusajili maduka kuhamishiwa na serikali katika baraza la wafamasia hapo mm ningekuelewa, bila data nitakuhesabu ni mleta umbeya tu. data utakazoleta zianishe je hawakufuata sheria, kuna kifungu cha sheria wanachokiuka lakini hawachukuliwi hatua n.k.

5. Kitu cha ajabu ni hiki maduka ya dawa yanafunguliwa hakuna udhibiti, ukaguzi wala usimamizi. Mfano tu Dare s salaam yenye karibu asilimia 80 ya Pharmacy zote nchini ambazo zinakadoriwa kufika kama si kuzidi 500, na maduka kadhaa ya Dawa Muhimu pamoja na utitiri wa maduka ya Dawa Baridi; kwa idadi ya staff waliyonayo pharmacy Council hawawezi kumaliza hata tukiwapa miaka miwili tu kukagua maduka yote ya Dar pekee.
mm nadhani tuwe objective tusiwe subjective, ubakaji ni kosa la jinai lkn mbona watu wanaendelea kubaka je serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake, hili sio kweli, ndiyo maana hatua zinachukuliwa kwa wahusika. TFDA ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha ubora na usalama wa dawa kwa walaji nilitarajia wawe wanashinda mitaani kuchukua dawa katika maduka yote yasiyo na kibali cha kufanya biashara hiyo kutoka baraza la wafamasia. mm nashawishika kusema hata TFDA enzi zao hawakufika maeneo yote na maduka yaliendelea kufunguliwa kana kwamba hawapo.

kwa mawazo yangu utii wa sheria bila shurti una mambo mengi na utekelezaji hufanyika hatua kwa hatua. kwa mfano wiki hii nimesikia baraza la wafamasia linaendesha operesheni ya kufunga maduka yanayokiuka sheria, nadhani ni hatua ya kupongezwa. badala ya kuvilaumu vyombo vya serikali wakati mwingine tuvishauri namna bora ya kutekeleza sheria. mfano ww mleta mada ninaamini pale unapoishi umeshuhudia kuna watu wamefungua maduka ya dawa bila vibali vya baraza la wafamasia, je umetoa taarifa kwa baraza ili hatua zichukuliwe, kama sivyo, ukiwa raia wa nchi hii umehatarisha usalama wa familia yako na jamii inayokuzunguka kwani kuna siku utakuwa ofisini mwanafamilia ataugua wataenda kununua dawa feki na kutumia na kupata madhara.

6. Swali la ziada nini kuhusu ya mikoani? Ni nani anayeweza kuwakamata wafanyabiashara wa dawa bandia na zilizoharibika? Je ni watanzania wangapi wanaaathirika kama si kufa kutokana na kung’ang’ania majukumu ambayo hawayawezi?
mm nafikiri mleta mada hajazisoma sheria za TFDA na Baraza la wafamasia bali kutokana na yeye kukosa ulaji, huenda aliokuwa anaupata kupitia haya maduka ya dawa yaliyohamia baraza la wafamasia ndiyo maana anapiga kelele zisizo na hata chembe ya ukweli. ukisoma sheria utaona jukumu la ubora na usalama wa dawa bado liko TFDA, yeye angekuja hapa akatuambia akiwa mmoja wa wafanyakazi wa TFDA amefanya nn kuzuia dawa bandia kutengenezwa nchini, kuingia na kuuzwa kwa ndugu zetu mikoani? wingi wa watumishi wa TFDA umesaidiaje kuzuia dawa feki/bandia za ARV, malaria na nyinginezo kuuzwa nchini.kwa upande wangu siwezi kuwalaumu TFDA kwani dawa bandia ni tatizo la kidunia, kama ilivyo kwa makosa ya jinai, la msingi ni kuongeza jitihada kupambana na makosa hayo kwa kushirikiano na vyombo vingine kama TBS, Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali .

7. Huku mtaani kuna madawa mengi sana feki na yaliyokwisha muda lakini bado yanauzwa.
hili ni jukumu la TFDA kisheria kama hapo juu panavyofafanua, soma sheria zote mbili utapata muktadha halisi

8. Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})
tupatie ushahidi ili tuweke kwenye kumbukumbu kwa matumizi ya kisiasa miaka ijayo endapo wataendelea kugombea ili tuyakomboe baadhi ya majimbo

9. Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.
ebu tafuta majadiliano ya bunge, kisha yalete hapa ili watu tupate fursa ya kuchambua kila neno na kujua ukweli,

ningependa kushauri watanzania tutoe taarifa za uhalifu kwenye vyombo vinavyohusika TFDA,TBS,FCC, Baraza la wafamasia na polisi ili tupunguze makosa ya jinai yakiwemo uuzaji wa dawa bandia. kuna baadhi yetu maeneo tunayoishi kuna viwanda vya kutengeneza dawa vilivyojengwa ndani ya nyumba za watu, tuwataje ili washughulikiwe.hii ni moja ya tabia ya wapangaji wa kichina/kihindi, ndio maana china adhabu yao ni kunyonga tu ili kuwapunguza wahalifu. Hakuna nchi yoyote duniani iliyofanikiwa kudhibiti makosa ya jinai bila wananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu

Well said...watz tumekuwa waongo na kutengeneza uongo ufanane na ukweli...hii ni hatar sana mimi naamini kila taasisi hapa ina majukumu yake na huo ulaji anaosema huyu ndugu mimi si uoni sababu wote ni watumishi wa serikali...au ulaji gani anaousema huyu..mwisho wa kufikiri ni mwanzo wa matatizo na tusikubali akili ndogo ya umbeya na uswahili itawale akili kubwa...think big!
 
sasa hivi akina nyoni na kundi lake wameondoka, kinachowashinda kuperform/kutekeleza vizuri majukumu yenu kama TFDA/PC ni nini? ninyi ni taasisi za serikali acheni majungu fanyeni kazi ss tutawapongeza

sifanyi kazi TFDA wa PC, ila nafahamu hali ilivyo kwa kiasi fulani

tatizo lililopo kubwa pale ni namna serikali inavyowapanga watendaji wake hasa kwenye fani ya famasia, kuna kitu cha makusudi cha kuweka some weak people kwenye sensitive position ili waburuze mambo yao

HILO PIA NI FACT
 
mm naona nijaribu kuchangia mada hii ili kupanua mjadala kwa wana jf /gt

1. Baraza la wafamasia (Pharmacy Council) na TFDA ni taasisi za serikali

2. Kutokana na kung’ang’ania kinachoitwa ulaji na visa yapo majukumu ya TFDA yamechukuliwa na kupelekwa Pharmacy Council ambako sasa afya ya mtanzania haina mwenyewe.

hili naona halina ukweli na mtoa mada anaonekana ni mtumishi wa TFDA anayetaka kuupotosha umma badala ya kuwaambia watanzania ukweli wa nn kilitokea.kuanzishwa chombo chochote cha Serikali huwa lazima Baraza la mawaziri na rais mwenyewe akubali. vilevile hata TFDA/Pharmacy Council vimeundwa hivyo na vinaweza kufutwa kwa maamuzi ya serikali. Afya ya watanzania ina mwenyewe kwani ni waziri wa afya akisaidiwa na watendaji wake pamoja na taasisi zake.Ukisoma sheria mbili za TFDA na Pharmacy council utaona TFDA wana jukumu la kusajili na kutoa vibali kwa dawa zote, vifaa tiba, vipodozi vyote na vyakula vyote lakini Pharmacy Council imepewa jukumu la kusajili vituo vya kutolea huduma za dawa yaani famasi zote ikiwemo za hospitali na maduka ya dawa muhimu.

kwa mtizamo wangu uwepo wa sheria hizi ni kuepusha mgongano wa maslahi ambao ungetokea endapo TFDA pekee ndio wangekuwa wanafanya kazi zote hizi.

3. Kitu kilicho cha ajabu ni kuwa TFDA toka ilipoanzishwa ilitengeneza mfumo ambao usajiri wa awali na usimamizi wa awali ulifanywa na wafamasia wa wilaya mpaka mkoa kasha TFDA makao makuu ukishirikina na timu ya afanyakazi wa TFDA katika ngazi mbalimbali. TFDA pia ilianza kujengewa nguvu ya rasilimali watu ambapo ilikuwa na hadi sasa inao wafanyakazi wengi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuanzia zile za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.

je hao walioko TFDA wana utaalamu gani ambao baraza la wafamasia hawana, nimepata taarifa kuwa baraza la famasi nao wanafanya kazi kwa kuwatumia wataalam kuanzia ngazi ya wilaya. hapa naona mleta mada anajichanganya na aya inayofuata kwani kama TFDA ina watumishi wa kutosha mbona wanatumia watalaam walioko wilayani?

4. Hivi karibuni Pharmacy Council wamechukua jukumu la kusimamia maduka yote ya Dawa (Pharmacy), maduka ya dawa muhimu (Accredited Drugs Dispensing Outlet-ADDO) na Maduka ya dawa baridi ambayo awali lilikuwa chini ya TFDA; kituko cha ajabu Pharmacy Council hakina wafanyakazi wanaozidi hata 30 kama siyo 20. Tetesi zinasema kisa cha hayo ni kuwa Pharmacy Council walikuwa hawana hela/ulaji waliamua kuchukua ili na wapate ulaji na si kuwaachia TFDA kila kitu. Na la pili kulikuwa na watu wana-madeal ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa na kupitisha dawa zao, hivyo kama zingekuwa chini ya TFDA ilikuwa ni kikwazo kwao. Kwani Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa kigingi kwao.

Si kweli wamechukua majukumu ya TFDA bali wamepewa na serikali Kisheria ndio maana sheria ilipitishwa na bunge la tanzania. kuhusu eti baraza la wafamasia hawakuwa na ulaji nalo naona liko biased kwasababu mm nijuavyo watumishi wote wanalipwa na serikali sasa ulaji ulikosekanaje?

vilevile kuhusu idadi ya watumishi kuwa 30 sioni tatizo kwani sio wakati wote taasisi ikiwa na watu wengi ndipo inakuwa na utendaji kazi mzuri. hebu jiulize TRA inawafanyakazi wangapi, mbona bado haturidhiki na ukusanyaji wa mapato ya serikali na tunaona hayana ufanisi. ukifutilia utagundua hata TFDA ilianza na watumishi wachache lkn leo wamefikia hapo walipo. kuhusu utekelezaji wa kazi walizopewa kwa mtizamo wangu sioni kama watashindwa kwasababu nimepata taarifa kuwa nao wanatumia wafamasia walioko mikoani na wilayani kufanya ukaguzi na kuwasilisha taarifa kwenye ofisi zao. wafamasia wanasajiliwa na baraza la wafamasia kwa maoni yangu nadhani watafanya vizuri zaidi na kwa umakini wakijua wakidanganya wanaweza kufutiwa usajili na baraza tofauti na ilivyokuwa kwa TFDA.

kuhusu madili ya kuanzisha maduka makubwa ya dawa hilo nalo linahitaji ushahidi, ungetuletea taarifa ya wafanyakazi wa baraza la wafamasia au ndugu zao walioanzisha maduka makubwa baada ya madaraka ya kusajili maduka kuhamishiwa na serikali katika baraza la wafamasia hapo mm ningekuelewa, bila data nitakuhesabu ni mleta umbeya tu. data utakazoleta zianishe je hawakufuata sheria, kuna kifungu cha sheria wanachokiuka lakini hawachukuliwi hatua n.k.

5. Kitu cha ajabu ni hiki maduka ya dawa yanafunguliwa hakuna udhibiti, ukaguzi wala usimamizi. Mfano tu Dare s salaam yenye karibu asilimia 80 ya Pharmacy zote nchini ambazo zinakadoriwa kufika kama si kuzidi 500, na maduka kadhaa ya Dawa Muhimu pamoja na utitiri wa maduka ya Dawa Baridi; kwa idadi ya staff waliyonayo pharmacy Council hawawezi kumaliza hata tukiwapa miaka miwili tu kukagua maduka yote ya Dar pekee.
mm nadhani tuwe objective tusiwe subjective, ubakaji ni kosa la jinai lkn mbona watu wanaendelea kubaka je serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake, hili sio kweli, ndiyo maana hatua zinachukuliwa kwa wahusika. TFDA ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha ubora na usalama wa dawa kwa walaji nilitarajia wawe wanashinda mitaani kuchukua dawa katika maduka yote yasiyo na kibali cha kufanya biashara hiyo kutoka baraza la wafamasia. mm nashawishika kusema hata TFDA enzi zao hawakufika maeneo yote na maduka yaliendelea kufunguliwa kana kwamba hawapo.

kwa mawazo yangu utii wa sheria bila shurti una mambo mengi na utekelezaji hufanyika hatua kwa hatua. kwa mfano wiki hii nimesikia baraza la wafamasia linaendesha operesheni ya kufunga maduka yanayokiuka sheria, nadhani ni hatua ya kupongezwa. badala ya kuvilaumu vyombo vya serikali wakati mwingine tuvishauri namna bora ya kutekeleza sheria. mfano ww mleta mada ninaamini pale unapoishi umeshuhudia kuna watu wamefungua maduka ya dawa bila vibali vya baraza la wafamasia, je umetoa taarifa kwa baraza ili hatua zichukuliwe, kama sivyo, ukiwa raia wa nchi hii umehatarisha usalama wa familia yako na jamii inayokuzunguka kwani kuna siku utakuwa ofisini mwanafamilia ataugua wataenda kununua dawa feki na kutumia na kupata madhara.

6. Swali la ziada nini kuhusu ya mikoani? Ni nani anayeweza kuwakamata wafanyabiashara wa dawa bandia na zilizoharibika? Je ni watanzania wangapi wanaaathirika kama si kufa kutokana na kung’ang’ania majukumu ambayo hawayawezi?
mm nafikiri mleta mada hajazisoma sheria za TFDA na Baraza la wafamasia bali kutokana na yeye kukosa ulaji, huenda aliokuwa anaupata kupitia haya maduka ya dawa yaliyohamia baraza la wafamasia ndiyo maana anapiga kelele zisizo na hata chembe ya ukweli. ukisoma sheria utaona jukumu la ubora na usalama wa dawa bado liko TFDA, yeye angekuja hapa akatuambia akiwa mmoja wa wafanyakazi wa TFDA amefanya nn kuzuia dawa bandia kutengenezwa nchini, kuingia na kuuzwa kwa ndugu zetu mikoani? wingi wa watumishi wa TFDA umesaidiaje kuzuia dawa feki/bandia za ARV, malaria na nyinginezo kuuzwa nchini.kwa upande wangu siwezi kuwalaumu TFDA kwani dawa bandia ni tatizo la kidunia, kama ilivyo kwa makosa ya jinai, la msingi ni kuongeza jitihada kupambana na makosa hayo kwa kushirikiano na vyombo vingine kama TBS, Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali .

7. Huku mtaani kuna madawa mengi sana feki na yaliyokwisha muda lakini bado yanauzwa.
hili ni jukumu la TFDA kisheria kama hapo juu panavyofafanua, soma sheria zote mbili utapata muktadha halisi

8. Waliochangia kufika hapa tulipo ni Zarina Madabida (Mbunge viti maalumu-CCM), Ms Kinyawa (Mrajisi wa Baraza la wafamasia), Ms Blandina Nyoni (Katibu wa Wizara ya Afya aliyefukuzwa). Ambapo inatajwa kama tetesi kwamba kulikuwa na bifu la chini kwa chini kati ya Ms Nyoni na Ms Madabida dhidi ya Ms Ndomondo (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA {she has resigned})
tupatie ushahidi ili tuweke kwenye kumbukumbu kwa matumizi ya kisiasa miaka ijayo endapo wataendelea kugombea ili tuyakomboe baadhi ya majimbo

9. Rejea comment alizotoa Z Madabida juu ya muswada wa marekebisho ya sheria ya Pharmacy Council wakati ukijadiliwa bungeni.
ebu tafuta majadiliano ya bunge, kisha yalete hapa ili watu tupate fursa ya kuchambua kila neno na kujua ukweli,

ningependa kushauri watanzania tutoe taarifa za uhalifu kwenye vyombo vinavyohusika TFDA,TBS,FCC, Baraza la wafamasia na polisi ili tupunguze makosa ya jinai yakiwemo uuzaji wa dawa bandia. kuna baadhi yetu maeneo tunayoishi kuna viwanda vya kutengeneza dawa vilivyojengwa ndani ya nyumba za watu, tuwataje ili washughulikiwe.hii ni moja ya tabia ya wapangaji wa kichina/kihindi, ndio maana china adhabu yao ni kunyonga tu ili kuwapunguza wahalifu. Hakuna nchi yoyote duniani iliyofanikiwa kudhibiti makosa ya jinai bila wananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu

Binafsi kabisa, naomba nimpongeze huyu mchangiaji ambaye kwa kweli amejitahidi kujibu kitaalamu na kiutu uzima katika hoja zote ambaye mtoa mada aliamua, kwa utashi wake kabisa, kuleta mada ambayo kimsingi inaonekana kama hana ufahamu wa kiundani zaidi, na anatumia hisia zake zisizo na ushahidi katika kuleta uchochezi usio kuwa na kichwa wala miguu.

Naomba niseme tena kwamba mabadiliko ya sheria yaliyofanywa mwaka jana novemba, yalifanywa katika kulenga uboreshaji wa sekta ya dawa hapa nchini, mpaka katika kumfikia mlaji wa mwisho kabisa. Naamini kabisa wafamasia wenyewe walishirikishwa kikamilifu katika mabadiliko hayo, na waliona yanafaa kufanywa kisheria.

Baraza la Famasi kupewa majukumu ya kusimamia taaluma ya Famasi na usimamizi wa shughuli zinazohusiana na taaluma hiyo sio kitu kigeni hapa ulimwenguni. Nakushauri wewe mtoa mada fanya utafiti, hata wa kwenye internet uone nchi zingine zinafanyaje.

Mimi binafsi naamini kabisa kuna uhusiano mzuri sana kati ya vyombo hivi viwili, na ndio maana kuna baadhi ya kazi ambazo Baraza na TFDA wanafanya kazi kwa pamoja mpaka sasa hivi, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Issue za ulaji ni stories za vijiweji tu, na naamini mtoa mada anajua kabisa huna haja ya kusema jambo hadharani bila kuwa na taarifa za kitafiti. Nenda Uganda pale uone jinsi mifumo ilivyokuwa, ambapo chama cha wafamasia ndio wanacontrol taaluma na pia wanataka kusimamia maduka. Sasa pressure groups like such organisation inawezaje kupewa dhamana hiyo? Ndio sasa hivi serikali yao inaanza kuamka.

Kingine nikusaidie kwa sababu hujasoma sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi kisheria. Kuna maduka ya dawa moto (yaani Pharmacies) na Maduka ya dawa muhimu (yaani ADDO), kwa hiyo hata ulivyoainisha kwamba Baraza linasimamia maduka ya dawa baridi, inaonesha uko mbali kiasi gani na mabadiliko ya sheria ya Famasi.

Pia katika suala la kaguzi, jumatano katika taarifa za habari za ITV na Channel Ten, nilishuhudia kaguzi iliyofanyika katika mkoa wa dar-es-salaam mzima, ambao kiukweli umeonesha mafanikio makubwa kwani maduka mengi yalifungwa yaliyokuwa yamekiuka taratibu, kanuni na miongozo iliyopo. Data ipo pale Baraza kama utahitaji.

Kwa vile mtoa mada amehisiwa kuwa ni mfamasia, na hata kama si mfamasia, mi napenda kumwambia kwamba chombo chochote cha serikali hakifanyi kazi kwa mitandao. Wafamasia wana chama ambacho ni Pharmaceutical Society of Tanzania (PST). Kama unadhani unataka kuisaidia jamii, naomba upitie chombo hichi kinachotambulika na serikali ili kufikisha maoni yako yaliyokuwa na evidence. La sivyo, mi binafsi, ninadhani unataka kuleta chuki kati hivi vyombo vyetu viwili.

Mimi nimalizie kwa kusema kwamba , taaluma ya Famasi sio ya taaluma ya kubeza. Pamoja na kwamba kuna changamoto nyingi zinazoikumba, ikiwemo uchache wa wanataaluma hiyo, na utumikaji wa taaluma yenyewe katika sekta ya afya, naomba nikiri kwamba Vyombo hivi Pharmacy Council na TFDA wanafanya kazi nzuri katika usimamizi wa shughuli zinazohusu taaluma (Baraza) na ubora, ufanisi na usalama wa dawa(TFDA). Wanatakiwa waangaliwe kwa jicho la pekee na Wizara ya Afya ili kuyapa nguvu zaidi kirasilimali, ili malengo yaliyoanishwa kwenye sheria zao yaweze kufikiwa kwa kiasi kikubwa zaidi, na ili wananchi akiwemo mtoa mada mwenyewe, wapate huduma bora zaidi ya dawa.

Kwenye kila mabadiliko ya kitu chochote, hapakosi uvumi na majungu, wanataaluma wa famasi msiyumbishwe, na msirudishwe nyuma mlikotoka.

Cheeers

Safi sana Silumbe....tena kuna looser mmoja hapo juu amesema eti wafamasia ni vilaza...hahahaa..aende asome hiyo miaka minne aone shughuli yake..lol
 
1. Ni vizuri kwa mtoa uzi siku nyingine anapotoa mada nzito kama hii awe amesoma hizo sheria zizilizoiunda TFDA na Pharmacy Council na azielewe, na ajenge mada yake kwa kutumia ufahamu sahihi wa sheria hizo, vinginevyo itakuwa na hisia tu au mawazo yake ambayo kwa kweli hayaendani na kilichomo kwenye sheria hizo zinazoainisha majukumu ya Taasisi hizo za Serikali. Kama hatuajisoma ni vizuri tukasema hivyo na tukaomba kuleimishwa kuliko kusema tusichokielewa vizuri.

2. Nakubaliana naye kuhusu upungufu wa wafanyakazi PC, na si hilo bali hata wakiongezwa pale walipo hapatoshi kabisa kwani ofisi ni za makontainer na ni chache. Napendekeza waongezewe watenda kazi na vitendela kazi ikiwemo ofisi,magari n.k. Kwa taaarifa yenu Ofisi ambazo PC wapo sasa ndio zilizokuwa za TFDA zamani kabla hawajajengewa uwezo na Serikali Kuu na kujenga Ghorofa lao walipo sasa. Kwa kuwa majukumu ya PC yameainishwa kisheria, sasa ni wakati muafaka wa kuwajengea uwezo....

3. Ninawasihi Chama Cha Wafamasia (PST) kiendelee kuifahamisha fani ya famasia kwenye jamii kwani watu wengi wakiwemo wengine hapa jamvini hawaielewi kabisa...kwani ikifikia mtu anasema hata kutumia computer hawajui na wao ni vilaza kweli inashtusha! Binafsi sidhani kwamba huo ni uhalisia, ila inawezekana watu wa kawaida hawaelewi au hajawahi kuona Pharmacist akitumia uwezo wake wote katika fani yake. PST fanyeni kazi yenu ya kuelimisha jamii juu ya mada mbalimbali zinazohusiana na dawa.
 
Pharmacy body ni wabinafsi!! Wamewatenga wafamasia wenye diploma wasiwe na mandate ya kusimamia pharmacy japo kwa maoni yangu wana uwezo Huo. Acheni keki ya taifa iliwe na wote! Ni hayo tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom