abdulkarim harub mzee
Member
- Jul 20, 2019
- 21
- 78
CHIMBUKO LA AL SHABAAB, VITA YA AL SHABAAB VS AHLUL SUNNA WAL JAMAA NA DHANA YA UGAIDI CHINI YA KIVULI CHA UISLAM
Naam Assalam Alaykum Warahmatullah Wabarakat, Katika nakala na machapisho yaliyopita nlieeleza kwa uchache dalili za kuenea kwa Ugaidi nchini Tanzania. Na pia kuna baadhi ya watu walinshauri kuwaelezea kwa kina dhana ya ugaidi katika bara letu pendwa la Africa. Namshukuru Mwenyezimungu kwa kunijalia kuendelea kutoa elimu yangu ndogo nliyopewa na Mwenyezimungu ili kuwaelimisha.
Al Shabaab iliaanza miaka ya 2004 amabapo lilikua ni kundi linalopambana na jeshi la Ethiopia lililokua nchini Somalia. Wasomali wengi waliwapenda saana kutokana na umahiri wao katika mapambano hayo na kuona kama Tumaini lao nchini Somalia. Al Shabaab waliendeleza mapambano yao kwa umaridad mkubwa saana na baadhi ya makabila na koo za nchini Somalia zikakubali Al Shabaab iendeshe uongozi katika himaya zao.
Taarifa za kua Al Shabaab wanashirikiana na Al Qaeda katika kipindi hiko zilizkuepo na watu walidhirika na hali kwa kua hawakuona dalili mbaya zozote za Al Shabaab kuwadhuru raia. Japo mataifa makubwa yaliyoona kua mbeleni kundi hili litaleta shida na kuonya watu wa Somalia, lakini wasomalia waliendelea kulipa umaarufu kundi la Al Shabaab. Kwa nini mataifa ya Nje yalishtukia mapema uhatari wa kundi hilo. Naam hili ni swali ambalo Wasomali hawakujiuliza kipindi ambapo Al Shabaab wanaanza harakati zao. Marekani na Urusi zilibaini kua wapiganaji wengi wa Al Shabaab ni wale ambao wanatokea AL Qaeda na wengine ni wale waliopigana katika vita za Afghanistan. Majemedari na manguli wa mapambano waliteuliwa kufundisha vijana hao wa Al Shabaab.
Al Shabaab likawa kundi ambalo lina wapambanaji wazuri wenye ustadi mzuri wa vita uliochangiwa na ukakamavu wa hali ya juu ukapelekea mpaka kua moja ya amakundi tishio nchini Somalia na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Basi kundi la Al Shabab baada ya kuleta amani nchini Somalia likajipatia umaarufu mkubwa baada ya kuwashinda wanajeshi wa Ethiopia na pia vilevile walionekana kama wanamgambo wa wanyonge.
KUANZA NA KUPUNGUA UMAARUFU WA AL SHABAB
Baada ya wanajeshi wa Ethiopia kudhibitiwa na wanamgambo wa Al Shabaab waliamua kurudi nchini kwao Ethiopia na Al Shabaab wakaonekana kama watetezi wa wanyonge. Baada ya ushindi huo Al Shabaab wakaendelea kuaminiwa na kuitwa katika koo mbalimbali za Wasomali ili wadumishe ulinz. Baada ya hapo Al Shabaab wakaanza kuleta sharia mbalimbali za Kiislam na hii ni baada ya kufanya mawasiliano na AL Qaeda kujenga mipango mbalimbali ya kufanya sharia za Uislam ziitawale Somalia yote. Idadi kubwa ya waislam walikuabaliana na hilo suala la kufanya Al Shabaab itumie sharia za Kiislam kutawala maeneo inayoyamiliki. Baadhi ya watu walikataa wazo hilo kwa kujua baadae mambo yanaweza kubadilika na ikajirudia ile hali ya Afghanistan.
Al Shabaab wakaendelea kusimamia sharia za kiislam na kuanza kukataza mambo ya kijamii mbalimbali mfano baadhi ya sherehe za wafugaji zailipigwa STOP. Unywaji wa pombe nao ukakatazwa hadharani huku waliogunduliwa kua walikua wanatumia vilevi walikua wanachapwa bakora 40 kama adhabu ya mlevi. Na pia wazinzi walichapwa bakora 100 na kama walikua katika ndoa zao basi waliuliwa kwa kupigwa mawe hadharani. Hii ilianza kuibua hisia tofauti baina ya Wasomali baadhi ambao hawakua katika miongozo thabiti ya dini.
Hali iliyokuja kushangaza wengi ni kupiga marufuku uzalishwaji na matumizi ya Mirungi. Hili ni zao ambalo Wasomali walikua wanatumia katika kila sehem. Mirungi ilikua inatumika kama dawa na pia vilevile lilikua kama zao la kibiashara. Hii ilipelekea Al Shabaab kuonekana kama inataka kutwala kidikteta na kutokana na kuwaua hadgarani watu waliokua wanapinga sera zao.
Hapo ndipo baadhi ya koo za Wasomali zilipoamua kupinga waziwazi utawala wa Al Shabaab na Wasufi wakaungana na kupelekea kuanzishwa kwa kundi lengine la Wasufi AHLUL SUNNA WAL JAMAA.
AHLUL SUNNA WAL JAMAA
ITAENDELEA