Vita vya Kagera na Anguko la Idd Amini Dada.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
UTENZI WA VITA VYA KAGERA NA ANGUKO LA IDD AMINI DADA.


Amani iwe juu yenu ndugu wapendwa.
Vita vya Kagera ni moja katika ya vita maarufu katika historia ya Afrika na historia ya Tanzania..
Ni vita vilivyopiganwa baina ya Tanzania chini ya Mwalimu Julius Nyerere na Uganda chini ya Idd Amini Dada.
Vita ambacho vilipeleka utawala wa Idd Amini kuangauka na Uganda kuingia katika historia nyingine.
Leo nitajaribu kukimbushia kidogo na kwa mbali sana kuhusu baadhi ya mambo ambayo kupitia Mikono ya watanzania kwa vipawa vyao waliweza kuandika kuhusu vita hivi kwa Yale tunayoyajua.
Mnamo mwaka 1987 muandishi wa vitabu ndugu H. Muhanika akiandika kitabu chenye hisia Kali kabisa kuhusu vita hivi vya Kagera.
Henry Muhanika aliezaliwa mwaka 1949 katika kijiji cha Kamachumu mkoani kagera na alikuja kuandika kitabu kilichochambua mengi tusiyoyajua kuhusu vita hivi vya kagera.
Akiandika kitabu chenye jumla ya beti 1271 ambazo zilikuwa zikielezea chimbuko,chanzo na asili ya vita hivi.
Ndani ya kitabu hili,ametajwa mtu ambae ndie aliemshauri Idd Amini kuivamia Tanzania NA baadae kuangukia katika kipigo kizito cha mbwa mwizi ambacho kilimtoa kanga manyoya.
Ni utenzi ambao upo katika mfumo wa mashairi huru,kwani kanuni nyingi za Ushairi zimevunjwa Kama alivyosema mwenyewe mtunzi katika beti ya saba na Tisa:
Usije kuniambia
Sheria zake utenzi
Ulio safi utenzi
Yatakiwa mistari
Minne kila ubeti.



Mimi haya nayajua
Sitaki kuyafuata
Ukitaka hebu sema
Mtunzi huyu ni nanga
Mwenye mambo kubananga.


Kwa hiyo kama in mjuzi wa mashairi utagundua kuwa kanuni nyingi sana za Ushairi hapa ziliwekwa pembeni.
Ila siongelei aina ya utunzi wake sana maana tayari mtunzi alishatoa tahadhari toka mwanzo wa kitabu chake.
Ndani ya kitabu hili,mtunzi amejaribu kuelezea historia ya Idd amini Hadi kuja kuingia katika Jeshi.
Mtunzi kamuelezea namna Idd Amini alivyokuwa kiumbo,kiimani,kiitikadi, na hata kisiasa.

Mtunzi ameeleze Hadi ahadi alizota Idd Amino kwa mwananchi wa Uganda Mara baada ya mapinduzi ya kijeshi yalomng'oa madarakani Ndugu Obote.
Tazama kidogo ubeti wa 35 na 36,alisema:
Dada aliendelea
Mimi si mwanasiasa
Mimi kazi yangu hasa
Ni kupigana kisasa
Lakini tangia sasa
Nitashiriki siasa
Nipige nchi msasa.


36.Nitashiriki kwa muda
Usio mrefu sana
Na hali ikitulia
Kambini nitarejea.


Tumeona jinsi gani Amini alivyowaaminisha waganda kwamba yenye kaenda kusafisha tu nchi lakini hatokaa muda mrefu madarakani kwani atarejea tena jeshini na nchi kuongozwa na serikali ya kiraia.
Mtunzi ametaja sababu ya Idd Amini kutumia jina la "Dada" ,jina ambalo wengi hatulijui.
Twende ubeti wa 403 ,406 na 407-408:
403.sheria iliyotungwa
Kambini iliwambia
Ye yote anaetaka
Lazima mke mmoja
Wa pili akiingizwa
Yatakua ni makosa.


406.Siku na ilitokea
Yule anaehusika
Na kambi kuiongoza
Alitaka kuchunguza
Akiukae Sheria


407.Idd alipohojiwa
Maelezo kayatoa
Hakukawia kuapa
Anae mke mmoja.


408.Amini alieleza
Yule mke wa ziada
Nyumbani anae kaa
Si mke bali ni Dada.


Pia mtunzi wa utenzi huu ametoa sababu nyingine ya Amino.kumi wa Dada kuwa ni:
410.Mwingine alitokea
Maelezo akatoa
Kwamba jina katokana
Na lile la kwake baba
Kaidada aliitwa
Amini alifupisha
Uzembe ukimtuma.

Hapo mengi yametajwa ndani ya kitabu hili,ili kupata uhondo zaidi,nitafute na ukisome.

JINA KITABU-UTENZI WAVITA VYA KAGERA.
MTUNZI-Henry R. muhanika.

Imeandaliwa na Idd Ninga,Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Kabisa,rejea hapo katika ubeti wa 410 utaona jina lake halisi la Kaidada limetajwa
 
Back
Top Bottom