Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Mna laana nyie vijana wa hotpot na blue band! Mgambo wenyewe wakiwa tight mnajinyea! Maandamano yanatangazwa kila siku hamuendi kisa mnaogopa mabomu ya machozi na virungu. HALAFU MNABWABWAJA TU HUMU JUKWAANI BAADA YA KULA NA KUSHIBA WALI NA MAHARAGE NYUMBANI KWA SHEMEJI YAKO UNAKOISHI!
we lofa tulia unadhani unavyolelewa Na shemeji yako basi wote tuko hivyo. Tuliza kijambio hicho
 
Wengi wa wanajeshi wetu baada ya vita walikufa kwa kukosa matunzo,Maana walitakiwa kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani walipaswa wapimwe ili kujua kama wameadhirika na Post-traumatic stress disorder (PTSD)Tatizo ambalo huwapata wanajeshi wengi wakiwa vitani au baada ya kutoka vitani.Baada ya vita wanajeshi wetu waliruhusiwa kurudi nyumbani bila kufanyiwa uchunguzi wa PTSD hivyo wanajeshi wengi walienda kuzua balaa kubwa kwa raia wema huko mitaani na kuna watu wengi sana waliadhirika sana na ujio wa hawa wanajeshi na hatimaye kusababisha wanajeshi wengi kuleta hali ya uvunjifu wa amani,Unywaji wa Pombe kupindukia,Ugomvi mbalimbali ambao wakati mwingine ulisababisha vifo kwa wanajeshi wetu hao!!!Binafsi nailaumu sana serikali yetu kwa kutotilia maanani maisha ya wanajeshi wetu hasa waliopigana katika vita vya kagera,Wengi wamekufa kwa msongo wa mawazo na bila msaada wowote.Na wengine walio hai sasa hivi hata ukiambiwa alipigana vita vya Kagera waweza kukataa maana ana hali mbaya kupindukia hawana mbele wala nyuma.Kinyume na nchi zingine wanajeshi wastaafu wanatunzwa vizuri na wanaheshimika.
Kweli mkuu..
 
Kamanda hongera nimesoma hii post mpaka machozi yamenitoka hongera umalitendea vyema taifa hongera sana
 
we jamaa umemsahau brigedia James Luhanga ambaye aliongoza kikosi cha Mizinga
 
Nakuunga mkono kabisa kwa hili la kuandila vitabu na kusimulia ni nini kilikuwa kinatokea uwanja wa vita..

Binafsi nadhani kuna haja ya kutafuta hata waigizaji mahiri wakapewa haya masimulizi wakayafanya kama script za kuandaa MOVIE. Nchi zote zilizoendelea huitumia sana hii..WHY NOT TANZANIA???
Kama naona CHUCK NORRIS wa Tanzania
 
Mkuu Echolima.asante kwa simulizi hii.murua. nilikuwa mdogo kipindi hicho lakini kishindo cha vita nilikisia...

Mkuu JokaKuu kuna kitabu nilikisoma kinaitwa "Kuanguka.kwa Fashisti Iddi amini" cha TPH nadhani. Chonde chonde mwenhe nacho au anayejua kinakopatikana ...kilisimulia vizuri sana.

RIP mashujaa waliotutoka.
Echolima

Hii ni kazi nzuri sana kwetu sote. Hatupaswi kuisahau historia yetu.

Ili kufanikisha uandikwaji na uchapaji wa kitabu najitolea kuifanya kazi ya Professional Typesetting and Graphic Design.

Watunzi na wachapishaji wengi wa vitabu siku hizi wamekuwa hawazingatii muonekano bora zaidi wa vitabu vyao, hivyo huishia kupata mapato duni yanayowakatisha tamaa.

Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi katika kubaini, kutambua, kukuza na kuimarisha soko la wasomaji. Kwa kuwa mbinu za kukabiliana na changamoto hizi zote ninazijua, niko tayari kufanya kazi na wewe pia katika hili, kwa manufaa yetu na taifa pia. Tukifanya kazi nzuri ninaamini kwamba Serikali inaweza kutuunga mkono na kukifanya kitabu hiki kuwa sehemu ya vitabu ambavyo vinaweza kuchukuliwa kama mojawapo ya vitabu vya somo la historia kwa shule za sekondari.

Licha ya kuwa mwanaharakati mwanamapinduzi, mimi pia ni mjasiriamali kwenye sekta ya ubunifu.

Trust me. I know what I am saying. You are looking at the goose that is about to lay its famous golden eggs.
RIP Kaka Sijui kama uliweza kutimiza lengo lako?
 
Habari nzuri sana hii. ni Historia MURUA. Nasi tukiwa Praimari wakati huo tuliimba:
Mashujaa twawaimba ni ndugu yetu Twalipo,
na Ndugu Simba Marwa (pia Mayunga),
na ndugu wanajeshi wote Twawapongeza
Kushika usukani mpaka Mwisho.
Chorus: Solo: Waliongoza
Wote: Vikosi mbalimbali
Solo: Kwa ushujaaa
Wote: hadi kuleta ushindi
Solo: Twashukuru
Wote: Kukomboa nchi yetu
Kwa Kumshinda ADUI,
Kwa hivi sasa Uganda,
Imekuwa nchi Huyu,
Tunawashukuru sana, Wana wa nchi..
 
140 Reactions
Reply
Back
Top Bottom