Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Halafu kuna jamaa anaitwa Kichuguu nae alitoa historia yake ya Vita ya Kagera naona maelezo yake yako humu copy and paste anyway labda ni coincdence am not accusing..!!!!!
Kama unaweza kuona kuna habari ambazo mimi mwenyenywe nilikuwepo na kuna habari kutoka vyanzo vingine ambavyo mimi sikuwepo mfano kasese mimi sikupita huko habari zingine toka vikosi vingine nimezipata toka kwa jamaa zangu ambao tulikuwa nao vitani lakini vikosi tofauti Mfano lt Emmanuel Nyangasa alipitia Mbarara lt juma Ramadhani alipitia masaka na mimi mwenyewe ambao tuanzia Mtukula na kuendelea sehemu pili utanielewa vizuri nitaambatanisha na picha nyingi tu zangu mwenyewe na za wengine maana tulibahatika kuwa na mwandishi wa habari kwenye platoon.Najua sana kutakuwa na challenge nyingi sana maana hapa ni kwa GREAT-THINKERS.
 
Halafu kuna jamaa anaitwa Kichuguu nae alitoa historia yake ya Vita ya Kagera naona maelezo yake yako humu copy and paste anyway labda ni coincdence am not accusing..!!!!!

Usituchafulie uzi wewe!

Basi we kila ukitoa pua yako ni kuchafua mazingira tu!

Hivi wewe huna wazee kwenu!?
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Usituchafulie uzi wewe!

Basi we kila ukitoa pua yako ni kuchafua mazingira tu!

Hivi wewe huna wazee kwenu!?

Mwenyewe mwenye uzi amenielewa vzur sana na hata sasa nimemwelewa ila kama wewe unataka tuchafuane mimi na wewe niko tayari.
 
Kama unaweza kuona kuna habari ambazo mimi mwenyenywe nilikuwepo na kuna habari kutoka vingine ambavyo mimi sikuwepo mfano kasese mimi sikupita huko habari zingine toka vikosi vingine nimezipata toka kwa jamaa zangu ambao tulikuwa nao vitani lakini vikosi tofauti Mfano lt Emmanuel Nyangasa alipitia Mbarara lt juma Ramadhani alipitia masaka na mimi mwenyewe ambao tuanzia Mtukula na kuendelea sehemu pili utanielewa vizuri nitaambatanisha na picha nyingi tu zangu mwenyewe na za wengine maana tulibahatika kuwa na mwandishi wa habari kwenye platoon.Najua sana kutakuwa na challenge nyingi sana maana hapa ni kwa GREAT-THINKERS.

Asante sana Echolima nimekupata vzur sasa mwanzoni nilidhani unaandika kile ulichoshuhudia tu ndio maana nkasema inafanana na ya Kichuguu nadhani utakua umepitia uzi wake pia. Shukran kwa Historia nzuri.
 
Nshimanyi na wengine wengi sana wametajwa kwenye sehemu ya pili ya historia hii vuta subira nitaitoa mda si mrefu.

Mkuu naisubiri kwa hamu sana hiyo sehemu ya pili maana tuliozaliwa baada ya ile vita wengi hatujui kilichotokea on the ground zaidi ya hear says...

Safi sana mkuu kwa kuja na huu uzi....
 
echolimo,

..kuna vitabu 3 kuhusu vita vya Kagera.

..kuna kimoja kimeandikwa na waingereza waandishi wa habari.

..halafu kingine kimeandikwa nadhani na Lt.Col.Ngatuni.

..kitabu cha tatu nimesahau kimeandikwa na nani, sijakiona muda mrefu, lakini nakitafuta sana. kimeandikwa kwa kiswahili na kiko very detailed kwa kumbukumbu zangu. unaweza kunikumbusha kuhusu kitabu hicho na wapi naweza kukipata??

..tafadhali, tafadhali, andika kitabu au hata vitabu kuhusu hii vita. mlifanya kazi KUBWA sana and I dont think it has been adequately documented.

..wale majenarali wote walioongoza vita walitakiwa waandike experiences zao kuhusu vita ile. zaidi, walitakiwa wawe wanazunguka ktk vyuo mbalimbali vya kijeshi kutoa mihadhara.

..andikeni hata operation za Seychelles, Comoro[nadhani walikwenda mara mbili], Msumbiji, na Zimbabwe.

NB:

..ambush ya Lukaya, maandilizi yake, washiriki wake, etc etc, inaweza kuwa kitabu peke yake.

cc:mad:gobore, Moshe Dayan, Shwari, Jasusi, Mzee Mwanakijiji
Nakuunga mkono kabisa kwa hili la kuandila vitabu na kusimulia ni nini kilikuwa kinatokea uwanja wa vita..

Binafsi nadhani kuna haja ya kutafuta hata waigizaji mahiri wakapewa haya masimulizi wakayafanya kama script za kuandaa MOVIE. Nchi zote zilizoendelea huitumia sana hii..WHY NOT TANZANIA???
 
Mkuu Echolima

Nimewahi kusikia mwenye moja ya masimulizi ya kama sio Mayunga basi ni Msuguri, kuwa aliwahi kufyatua kombora kutoka kwenye kifaru alichokuwa nacho na akalenga tundu la mtutu wa kifaru cha adui wa Uganda, kwamba jamaa alikua na shabaha ya hatari ni za kweli au maneno ya watu??

Vipi suala la kuwaacha wale wanajeshi wa Uganda pale Mtukula wajifie wenyewe kwa kukosa msaada na baadaye watu wa OAU wakapelekwa kuwaona ilikuwa ni war strategy ya uwanja wa vita au ilifanywa na Mwalimu kwa malengo ya kisiasa kuuonesha ulimwengu kuwa Uganda ni wavamizi??

Suala jingine linaloniacha hoi ni kwa nini siku mbili tatu kabla ya vita Idd Amin alionekana ikulu ya Dar es Salaam akiwa na mazungumzo mazito na Mwalimu na wakanywa mpaka "kahawa" pamoja??, Hii kivita imekaaje??, Kwa nini asinge mnaniliu tu huku huku mpaka kupeleka nchi vitani??

Mwisho kabisa naona umezungumzia vita ya ardhini na majeshi ya angani kidogo sana vipi majeshi ya maji?? Ina maana wakati huo tulikua wachovu sana kwa upande wa majeshi maji?? maana kwa Uganda ilivyo ilikua ni rahisi kuivamia kupitia ziwa Victoria kwa kupitia Musoma, Mwanza na Kagera kuliko kuzunguka koote huko...

Shukrani sana...
 
Last edited by a moderator:
Echolima,

Umetaja basi la Lupondije umenikumbusha mbali sana mimi binafsi nimeishalipanda sana.

Zamani tulikuwa tunatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na basi Kauma au Tanganyika basi, ukifika Mwanza kwenda Magu au Nyanguge, unapanda Lupondije basi, teh teh teh.

Naomba nikuulize kitu kama kilikuwa cha kweli, wakati mnatoka vitani, mlikuja na vifaa vingi sana radio/tv/friji/magari/vyombo/ ni kweli mliwapora raia wa Uganda.

Nakumbuka mlivyokuwa mnagawa biskuti kwa raia barabarani.

CC; Jasusi, gombesugu, Prof. Ngongo,
 
Last edited by a moderator:
Lt. ni kweli mmoja wa makamanda Marwa ama Msuguri, katika kuonyesha madhuni na kusudi la vita, aliwaambia wapiganaji kuwa ni bora wote "wapiganaji" wavuke daraja la mto kagera na ikiwezekana livunjwe(libomolewe) ili askari yoyote asirudi nyuma hadi vita iishe!
 
Mkuu Echolima,

Zile biskuti mlizokuwa mnakula vitani zilikuwa za nini mbona zilikuwa ngumu sana.

Na yale maharage ya kopo, pamoja na nyama ya kopo, zilikuwa zinatoka wapi.

Naomba unipe darsa kaka.
 
Last edited by a moderator:
Mara nyingi sana Jeshini huwa na kitu kinaitwa DRY RATION Wakati huo hata sasa naamini kipo kinagawiwa wakati wa dharura yoyote- kwa wakati ule kulikuwa na maji ya machungwa ORANGE Na Biscut nyingine zilikuwa zinatoka humu humu nchini zingine zilikuwa zinatoka nje vile vile na Nyama zilikuwa zingine zinatoka pale KAWE Kuhusu zile nyama au Biscut zilikuwa na nini mimi naamini zilikuwa za kawaida sana na wakati ule uchakachuaji haukuwepo hivyo vyakula hivyo vilifaa sana,Wengi wanaamini kuwa vyakula vya jeshini vimewekewa vitu ambavyo huwafanya wawe wajasiri kama simba hiyo si kweli kabisa.mimi najua wale walimu wa siasa Jeshini ndiyo waliokuwa wanawapandisha MORI askari kiasi cha wao wenyewe kuamua kwenda Front-line bila wasi-wasi.Mimi nakumbuka sana tarehe 06-11-1978 Baba Nape(MZEE MOSES)Katutangazia kuwa wamepata habari na wana uhakika kabisa kuwa Majeshi ya Amin hayana vifaa vizuri wao wanazo silaha za kizamani sisi tuna BM wao hawana lakini baada ya sisi kwenda mbele tulikuja kugundua kuwa kumbe amin alikuwa na vifaa Bora kuliko sisi alikuwa na Vifaru T-54 na T-55 pamoja na mizinga, BTR APCs, BM-21 Grad MRLs artillery, wakati sisi tulikuwa na T-34 na Vifaa vingine ambavyo ukilinganisha na wao vilikuwa duni.Hivyo watu wa Propaganda ni mhimu sana Mstari wa mbele.
Mkuu Echolima,

Zile biskuti mlizokuwa mnakula vitani zilikuwa za nini mbona zilikuwa ngumu sana.

Na yale maharage ya kopo, pamoja na nyama ya kopo, zilikuwa zinatoka wapi.

Naomba unipe darsa kaka.
 
Last edited by a moderator:
Kwangu mimi kiingereza ni lugha ya kigeni simtaalaamu kama wewe au wengine pamoja na kwamba naweza kuandika historia hii kwa kiingereza najua naweza sehemu kukosea,labda kwa faida yako nimesoma Marekani kwa mwaka mmoja Israel miaka mitatu na iliyokuwa USSR UKRANE Mwaka mmoja hivyo kuchapia kwa kiingereza naweza kukosea tu maana si lugha ya mama.
Echolima,

..dont put ur self down.

..ukifika wakati wa kuandika kitabu tafuta mtaalamu wa lugha na mtaalamu wa histori wakupe kampani.

..hata publisher wako anaweza kukusaidia kumpata mtaalamu akakifanyia mapitio kitabu chako.

..kuna jamaa alishiriki kwenye shambulio lililomuua Osama Bin Laden ameandika kitabu kwa msaada wa mwandishi mwingine.

..sasa hebu fikiria just that raid mtu anaandika kitabu, sembuse nyinyi mliopigana vita ya karibu mwaka mzima??

..majuzi nimeona paper inayohusu jaribio la Rwanda kujaribu kumpindua Raisi Kabila Snr wa Congo. Jaribio hilo lilizimwa kwa msaada wa majeshi ya Angola, na Zimbabwe. sasa pande zote tatu zimeandika kuhusu tukio hilo.

cc: Pasco, Jasusi, Kichuguu, Moshe Dayan
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom