Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Meneja wa hospitali ya Alshifa hapo jana kwa niaba ya hospitali chache ambazo hazijasitisha huduma ameiita siku hiyo kuwa ni vita dhidi ya hospitali hiyo ni baada ya jeshi la Israel bila haya kuzizingira hospitali kadhaa kwa vifaru na kuzuia huduma zote kuendelea.
Baada ya hapo hospitali hizo zilianza kupigwa kwa makombora kutoka ndege za kivita na kusababisha vifo vya watu wengi.
Upande wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa amewahi kusema Gaza imegeuka kuwa ni kaburi la watoto baada ya kuona jinsi watoto wanavyouliwa wazi wazi ja jeshi la Israel.
Yenyewe UN imeshapoteza wafanyakazi wake zaidi ya 100 ambayo ndio idadi kubwa kuwahi kulikumba shirika hilo katika mzozo wowote mmoja duniani.
Mashirika ya habari nayo yameshapoteza waandishi wao wa habari mahiri tangu kuanza kwa vita hivyo wengi wakiwa wameuliwa kwa makusudi kwani huwa wamevaa vizibao vyao vya kuwajulisha shughuli yao.
Hasira hizo za IDF ni matokeo ya kutofikiwa kwa malengo yake zaidi ya mwezi tangu vita na wapalestina vianze huko Gaza. Hakuna mateka hata mmoja aliyeokolewa na Hamas bado wako hai wanapigana kwa nguvu.