Takbir!?
Neno vita lina tafsiri moja tuu...! Ugomvi.. Penye vita hapana patano, hapana amani... Penye vita pana uharibifu wa mali na roho, majeruhi, ulemavu na vifo... Vita vinaharibu na kusambaratisha... Vita sio kitu chema! Vita sio kitu cha kujivunia... Vita ni uasi na kisasi... Vita ni ubabe na unyama...
Neno takatifu linatokana na neno utakatifu... Yaani njema, safi isiyo na mawaa, nzuri ya kutukuka... Isiyoangamiza inayoleta uhai... Yaani utakatifu ni jambo jema tena la kheri kabisa... Mikono ya mtakatifu ni safi na hainuki damu na mauaji kama mikono ya bwana vita! Penye utakatifu pana neema, hapana baya wala kisasi! Pana amani hapana taharuki.....
Mkanganyiko mkubwa unatokea pale unapotaka kuchanganya haya maneno mawili... Halafu yalete tafsiri isiyotatiza! VITA TAKATIFU...!
Misahafu ya dini zetu zote imeandika sana habari hizi... Habari za vita takatifu... Mapigano makubwa yaliyoangamiza roho nyingi na ushindi dhidi ya walioshindwa
Vita takatifu ni vita ya kiimani wema dhidi ya ubaya... Dhuluma dhidi ya usawa.. SHETANI dhidi ya MUNGU! vita takatifu ni vita ya imani kwenye ulimwengu wa roho... Sio vita ya macho..... Vita ya macho na kubeba silaha nzito sio vita takatifu... Vita takatifu silaha yake ni imani... Imani kuu kwa hakika.. Na ni vita inayopiganwa na WAAMINI dhidi ya .... WASIOAMINI.....
Kwanini sasa kuwe na vita inayoangamiza miili ya wanadamu, kuijeruhi, kuitia ulemavu na hata kuiangamiza? Kwanini iwepo vita inayoharibu mali na ustawi wa jamii ya nyama na damu? Na kwanini vita kama hiyo iitwe TAKATIFU? Utakatifu wake uko wapi?
Ulimwengu wa roho ndio injini kuu ya nishati inayoendesha ulimwengu unaoonekana kwa macho... Na ulimwengu huu wa roho ni timilifu... Hauna kasoro... Utimilifu wa ulimwengu wa roho ndio utakatifu.... Sasa ni katikati ya utimilifu huo wa roho na utakatifu wake... Ndio hutokea nguvu kinyume inayojaribu kuyumbisha ama kuangamiza roho timilifu katika utakatifu wake!
Hapa ndio tafsiri ya vita takatifu inapokuja... Vita ya kiimani iliyoanzia mapigano kwenye ulimwengu wa roho bila damu, bila... viasili vya mwili uharibikao...
kila roho inayoangamia kwenye vita takatifu ni ishara na ushindi kwa upande mmoja.... Na roho zote tarajiwa zinapoondoshwa kwenye mwili wa damu na nyama vita hukoma na kuanza kutafuta patano la amani mezani kwa njia ya mazungumzo... Bila silaha tena.....! Suluhu ya vita yoyote huishia kupatanishwa mezani... Na hapa ndio nguvu ya utimilifu wa ulimwengu wa roho katika dhana ya utakatifu inapojidhihiri....
Hivyo wapendwa vita takatifu kwa kigezo cha dini ni maneno yaliyopotoshwa ama kutumiwa na kaliba fulani hapa duniani kukidhi matakwa ya viumbe fulani
View attachment 799385