Hii mada ni ngumu sana kwa kuwa inahusu ujuzi wa kisheria na ilmu kubwa sana.Nimeuliza swali as per heading... Vita takatifu ni ninini hiki? Kisha nikajaribu kuweka uchambuzi wa kufanunua.... Inawezekana kabisa nimetumia lugha ngumu isiyoeleweka na isiyo na hitimisho.. Lakini nia ni kuamsha mjadala.... Kwakuwa hata nyie hapa hii kitu mnaweza kushindwa kabisa kuipa tafsiri sahihi bila kuacha maswali
Labda nifafanue kidogo:
Hapa duniani kuna vitu viwili ambavyo vinapinzana.[emoji116]
Binadamu na MUNGU.
Kama unaamini kuna dini lazima utaamini kuna vitabu vya dini.
Binadamu baada ya kuletwa hapa duniani yaani zama za Adam na Hawa, wao waliambiwa tokeni huku hali ya kuwa mumefukuzwa na nendeni duniani na huko tutawaleteeni mwongozo na atakaeufuata atasalimika na atakaeuacha atakuwa kadhulumu nafsi yake.
Sasa basi kipindi hicho hakukuwa na mambo ya siasa bali kulikuwa na miongozo ya vitabu vya dini pekee na wasimamizi walikuwa mitume na manabii.
Tukiigeukia historia,vita takatifu ya kwanza kabisa ilipiganwa mbinguni kati ya malaika na majini baada ya wao kupuuza mwongozo wa MUNGU na mwishowe wakafutwa wote na akabakia mmoja ambae yeye akawa chanzo cha uzawa wa hawa waliopo sasa.
Vita ya pili naweza kusema ilikuwa baina ya Nuhu ambae yeye kwake aliiona ni ngumu kwa yeye kupigana na akaomba msaada kutoka mbinguni na MUNGU akashusha maji na ikawafuta watu wote isipokuwa wachache tu walioingia kwenye jahazi.
Vita nyingine ni.
Luti
Nabii issa na waislaeli ambao walikuwa hawamtaki kabisa.
Musa.
Daudi hao wote walipigana hivyo vita vitakatifu...nk.
Sasa basi wanaoweza kuvisimamia hivi vita takatifu ni wale ambao wanaona utawala Fulani una udhalimu na kwaiyo wao wanaruhusiwa kufanya hivyo vita kisheria ya dini ili kuuondoa huo utawala.
MF:
MUNGU alimtuma Nabii Musa kwenda kupambana na firauni na jeshi lake japo na wao walikuwa wanapinga kama tupingavyo sisi lakini ilitakiwa lazima afanye hivyo.
Sisi karne hii wasimamizi wa vita takatifu ni viongozi wetu wa dini hata kama sisi wengi wao tunapinga na hatutaki..
Wao wataangalia kisheria japo wengine hawapendi na watachukia ila wao watachukuwa maamuzi ya kupigana na tukumbuke kuwa hizi siasa zimetokana na vitabu vya dini na watawala wamebadilisha na kuweka ya kwao.
Dini imekuja kutenganisha haki na baatil.
Tatizo lililopo:
Ni kuwa dini inatakiwa iwe moja ili imuabudu MUNGU mmoja hapo ndipo lilipo tatizo..nani asikilizwe na nani asisikilizwe.
Cha msingi ni sisi kusoma sana ili kujua na dini ipi ipo sawasawa na tusiingize ushabiki wala matashi ya kidunia.