Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,408
Hamjambo!
1. Ni wazi vita imekolea kwa kiwango cha juu kabisa
2. Propaganda za tafuta pesa zilishamiri huku watu wakifikiri pesa ndio utu wa mwanadamu.
3. Sisi watibeli Pesa ni karatasi tuu. Yaani kuwa kwako na pesa hakutufanyi tukuone wa maana kuliko watu wengine.
4. Propaganda ya tafuta pesa ilikuwa imeshamiri zaidi kwenye mambo ya kijamii hasa mahusiano ya kimapenzi kule MMU lakini mambo yanaenda kubadilika na kuingia kwenye siasa.
5. Kila kitu tafuta pesa. Ukisema hivi wee tafuta pesa. Kwamba watu kwenye akili yao waweze tuu pesa na mali kuliko kitu chochote au jambo lolote lile.
6. Matokeo yake watu wakifikiri kuhusu pesa tuu yaani kutanguliza pesa tu vilio na milio, mauaji na maombolezo yanaanza kusikika. Watu wanaanza kusema mambo ya UTU.
7. Hivi ndugu zangu, Lini . Nauliza tangu Lini Uchu wa pesa na UTU vikawa sehemu moja. Tangu Lini?
8. Tafuta pesa tupo hapo. Kwa njia yoyote uwe na pesa. Tupo hapo!
9. Watu wanang'ang'ania Madaraka, vyeo kwa sababu ya pesa. Mnawalaumu nini? Si mlisema wenyewe watu watafute pesa. Wakizitafuta mbona mnalalamika?
10. Watu walipwa pesa wakaue watu wengine. Mnawalaumu. Mnalaumu nini? Si mnataka watu watafute pesa. Hayo ndio matokeo ya kupenda pesa na kuchagua pesa kuliko UTU.
11. Watu wanaamua mpaka kuwa machawa, mashoga, kubwa mario, kuuza madawa kwa sababu ya kauli ileile. Tafuta pesa weee! Niliwahi kuandika hapa miaka kadhaa. Nikatukanwa. Silaumu kwa wanaofanya hayo kwa sababu sio kila mtu anakarama ya kuona matokeo ya mbeleni.
12. Watu lazima wahamasishe UTU, HAKI, UPENDO. Hayo mambo ndio msingi wa familia, jamii na taifa.
Unahamasisha pesa alafu utegemee UTU, HAKI NA UPENDO umelogwa wewe. Hujui usemalo na uombalo
13. Nakuhakikishia kwa asilimia mia moja. Yote yanayoendelea nchi hii ni matokeo ya roho ya kupenda Fedha na mali. Na wala hakuna sababu nyingine yoyote ile.
14. Mafundisho yaliyokuwa sahihi ni kuhamasisha;
a) Fanya kazi yoyote halali. Ridhika na unachokipata.
Heshima ya mtu haijengw kwenye pesa.
b) Utu ni bora kuliko mali na utajiri.
c) Heshima ya mtu ni anapofanya matendo mema.
d) Kujifunza kwa watu wanaofanya kazi zinazoonekana na kujulikana.
15. Mitandaoni pesa. Ukienda kwa wachungaji wanahubiri pesa.
Ukirudi nyumbani wazazi wanalia na pesa. Ukiyatoa kafara upate pesa yanaanza kulialia. Unalia nini sasa?
16. Hakunga uhuru kwa wapenda pesa weka akilini hiyo.
Hakunaga haki kwa wapenda pesa weka na hiyo.
Hakunaga upendo kwa wapenda Pesa chukua hiyo.
17. Ni mwendo wa nifanye nini unipe pesa. Hawajali kama ni halali au haramu. Muhimu kwao ni pesa. Hayo mengine hayawahusu.
18. Nyie mbadilishe Katiba ili nini? Ili miradi yangu, michongo yangu, na mitego yangu ya pesa niliyoiweka isinipe pesa. Thubutu yake! Haiwezekaniki. Mkiweza tupigane atakayeshinda haya.
Ndicho kinachoendelea hivi leo.
19. Hakunaga maridhiano kwa wapenda fedha. Hayapo hayo. Maridhiano yatakayogusa maslahi ya pesa yatazuiwa na hayatofanyika wala kufanikiwa. Ndivyo fikra za wapenda pesa zinavyofanya kazi hivyo.
20. Tume ya uchaguzi ibadilishwe ili? Wapenda fedha na wale wazee wa tafuta pesa lazima swali hilo likiulizwa waangalie je ikibadilishwa itaathiri mfumo wa mapato yao? Hilo kwao ndio muhimu.
21. Wapenda fedha usiwaambie mambo ya haki sijui upendo. Utakuwa kama kituko, kioja na wataona umerukwa na akili.
22. Wakati fulani nilienda kununua kahaba maeneo fulani. Nilipofika pale nikiwa kwa mbali nikiwa na chagua nikavutiwa na mada mrembo mwenye nyamanyama na kaumbo fulani hivi.
23. Nilipofika wakawa wananing'ang'ania kama mpira wa kona. Hatimaye nikakachukua kale kadada. Tulipofika ndani nilikatambua kanaitwa Tina kama kifupi cha Chtistina.
24. Huduma ile ilikuwa ya kulipia,, elfu 30 hivi kwa mshindo mmoja. Na hapo hakuna mambo mengi. Yaani huvui nguo zote. Heheee! Taikon unaenda wapi huku. Ujue unajidhalilisha. Haya mambo ni faradha. Tulia!
25. Yule dada nikamwambia mimi sijajakufanya mambo hayo kwa leo. Akaniambia akiwa ananitathmini usoni, umekuja kufanyaje sasa, wewe ni askari, nikamwambia hapana. Akasema kwa hasira usinipoteze muda.
26. Nikamwambia nitatumia dakika kumi kuongea na wewe tuu alafu nitakupa elfu 30 yako.
27. Hapo nikamwona ameshusha hasira zake kwa kushusha pumzi. Akaniangalia kwa macho ya udadisi yenye hofu asiyoijua.
28. Nikatoa elfu 30 nikampa. Akaipokea akawa ameishika mkononi.
29. Nikamuuliza kwa nini anafanya kazi ile. Akaeleza weee kwa kirefu sana. Lakini sababu kubwa aliyokiri ni kupenda pesa na uvivu wa kufanya kazi. Kwani nilipomwambia mtu akikupa mtaji ukaacha kazi hiyo akasema hawezi kuacha kwa sababu hataki stress za biashara. Zaidi anasema aliwahi kujaribu biashara zikamshinda. Hata hivyo kwa sasa anasaluni ipo Tabata ambayo ndio anatumia kuzugia kama sehemu ya shughuli ya kuzalishia kipato.
30. Nilipomwambia natafuta mke wa kuoa. Na nahisi yeye atafaa akacheka sana. Huwezi akasema kwa kunisifia kwamba mimi ni kijana mzuri ambaye yeye angejivunia lakini tatizo yeye anapenda pesa na ameathirika na jambo hilo. Kwamba nikiwa naye atakosa pesa za wanaume wengine.
31. Nilishangaa sana. Akasema ataishia kuniumiza na zaidi kunidhalilisha.
32. Baadaye nilimwomba tuombe. Tukaomba. Hazikuwa dakika 10 tena. Saa ambayo iikuwa mule ndani ilionyesha tumedisha dakika kumi na tano yaani tumezungumza kwa dakika 25.
33. Baadaye akaniambia chukua tuu hela yako akiwa analia. Alikuwa analia kwa kwikwi. Nikawa nambembeleza. Nikimwambia asijali wala asijihukumu sana. Ila. Pia asijiendekeze kwenye kujikosea heshima na utu wake.
34. Aliniomba namba. Sikuwa nimetembea na simu. Nikamwambia nitarudi wakati mwingine. Akajua nimemnyima kwani inakuwaje sijakariri namba yake. Sikumpa!
35. Baada ya mwezi kuisha nilirudi palepale wanapojiuza. Sikumkuta ila moja ya makahaba wenzake alimpigia nikiwa pale. Alinikumbuka. Alifurahi kuona nilirejea kwaajili yake. Akanisihi nichukue namba yake kwa huyo rafiki yake ambaye nilimtambia kwa jina moja P.
36. Tina aliacha ukahaba, aliamua kuwa msusi wa saluni na baadaye kuwa Fundi cherehani.
37. Mara pili tulionana mwaka 2019 huu mara ya kwanza ikiwa 2018. Mwaka mmoja baadaye.
38. Nilifurahi kumwona Tina akiwa katika hali ile. Hakuwa na nguo fupi tena. Hakuwa na Manyonyo nje tena. Alibakiwa na tattoo moja niliyoiona kwenye shingo yake. Yenye jina Angela. Alinifahmisha huyo ni Mamaake.
39. Sio tuu mabadiliko ya kimwili niliyoyashuhidia kwake. Bali pia mabadiliko ya kiakili, kimtazamo, kiroho na kihisia.
Alikuwa Tina mpya. Mtibeli aliyezaliwa katika hali ya uovu na kujidhalilisha.
40. Nakumbuka aliniambia, maisha yake sasa yanafuraha. Anasema Bob kwa sababu alipojua jina langu alipenda kuniita Bob.
Akasema, pesa sio kila kitu. Ninaishi maisha ya kawaida hata wakati mwingine sina hata mia lakini moyo wangu unafuraha na amani.
41. Tina aliolewa Mwaka 2021. Alinialika na nilienda nikiwa na mchumba wangu wakati huo ambao sasa ni mke wangu.
42. Ninafurahi kuona maisha ya Tina yakiwa yafuraha na mabadiliko changa.
43. Kwa mtazamo wa Tina kipindi kile kamwe isingewezekana kuolewa na kijana aliyenaye Leo. Ameolewa na kijana wa kawaida kabisa ambaye anaishi maisha ya kawaida na kufanya shughuli za kawaida za uzalishaji mali.
44. Nataka kusema Ukishaanza kuipenda fedha na kuitanguliza kuliko kitu au jambo lolote maisha yako utaenda kuyaharibu na sio yako tuu bali hata maisha ya watu wengine.
45. Utaumiza wengine bila kujali. Utageuka kuwa bad monster.
45. Pesa ni muhimu lakini kamwe usiiweke kipaombele chako. Pesa isikae nafasi ya UTU.
46. Kwa sababu pesa ikikaa nafasi ya utu matokeo yake ni mabaya na makubwa sana ndani ya familia, jamii na taifa.
Yule Mtibeli hana la ziada. Nawatakia siku njema yenye baraka.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam