Visomo hivi si dalili njema sana

Siamini visomo au maombi yatakuwa na matokeo yale ambayo wengi wanatarajia ndani ya muda mfupi. Lakini funzo kubwa ni kwamba kuna watu wengi sana wanalia mioyoni mwao kutokana na mengi yanayoendelea nchini. Kuanzia ukata mtaani, bomoa bomoa, kubanwa kwa uhuru wa kuongea na kukusanyika au kuandamana, mpaka tukio la Lissu kupigwa risasi.

Mambo haya sio madogo. Ktk hali ngumu ya maisha kama hii ungetegemea serikali ikupe moyo na sio ikupe sababu ya kuamini inahusika na kujeruhiwa kwa mtu. Maisha ya Lissu ni ya wanyonge walio wengi, ni ya kupigania wanaoonewa kuanzia vyuoni mpaka ktk migodi. Kushikamana kwa watanzania ktk hili kunaonyesha namna Tundu Lissu alivyoyaishi maisha ya wanyonge. Nadhani ni mmoja wa mawakili wanaoongoza kwa kufanya pro borno (kesi za bure) kwa ajili ya wanyonge.

Narudia kusema kwamba kuna funzo kwa vyombo vyetu vya dola. Kuna watu fulani ktk nchi lazima walindwe kutokana na ushawishi wao na mtaji wao kwa wananchi, lazima walindwe bila kujali kwamba wako vyama vya upinzani. Kwa kufanya hivyo unakuwa unailinda serikali iliyo madarakani dhidi ya chuki na hasira za wananchi. Serikali haiwezi kufanikiwa bila kuungwa mkono na wananchi.
 
Mshana, umenena kwa hekima sana. Ikiwa tutazoea kutumia nguvu na maguvu kwa kila jambo kuna siku wanaohisi kukandamizwavwatasema liwalo na liwe. Nahisi watawala wetu wamegeuka kuwa waumini wa maguvu, tuwaombee.

Vv
 
Mkuu mbona hueleweki???...Umesoma vizuri huu uzi??? Rudia kusoma then toa maoni yako.....
 

visomo huwa ni siri!!!

hata wakifa hatutawajua, mrema mbona iligoma?
 
Serikali haina dini, lakini wananchi wake wana dini, inashangaza serikali ambayo haiamini juu ya Imani inakataza watu wenye Imani kufanya mambo ya Kiimani.

Wanahofia nini hasa!
Kumbe huwa viongozi wanatudanganya....Kukataza maombi ya wananchi/raia kutokana na imani zao ni jambo la kushangaza kidogo...
 
kama wanavyofuatilia mitandao ya kijamii basi hili nalo wameliona na watatafuta muafaka
 
Kimsingi hicho kisomo ni njia ya kisaikolojia ya kumbaini MTU aliyetenda jambo fulani.Huyo mtu hubainika kwa kuonyesha hofu waziwazi na kufanya maamuzi ambayo ni kinyume na alivyokuwa akitenda awali,namaanisha kwamba inawezekana kuna jambo ktk jamii fulani huwa linatendwa Mara kwa mara, lakini ghafla hilo jambo linaonekana ni geni na hatari.
 
Kila binadamu anapenda kuthaminiwa na kuheshimiwa,atakapogundua kuwa anapuuzwa ktk mambo yake ya msingi huwa anareact.Sasa tujitahidi kuondoa hizo reactions ili maisha yaendelee.
 
Albadili haiwezi kufanya chochote,sasa hofu ni ya nini?Je now days serikali inaamini mambo haya?
 
Kwa vyovyote vile, nchi inaendeshwa kwa mapenzi ya Mungu.
Mungu ametajwa hata katika wimbo wetu wa Taifa, ili alibariki Taifa la Tanzania.

Hata rais wetu ametuomba mara kwa mara kumuombea katika kazi zake.
Sasa haya tunayoyaona ni kinyume na baraka za Mungu.
Watu wanaomba negative energy, Albadiri, tena kwa utashi wao, baada ya kuona giza litokanalo na dalili za umwagaji damu.
Mungu ainusuru nchi hii, watawala walione giza kama wananchi wanavyoliona, ili hatua stahiki zichukuliwe.
 
Wizi wa mali zipi za Taifa? Ni huu usanii unaoendelea kwenye masuala ya madini? Hapa kinachofanyika zaidi ni kutafuta sifa. Mpaka sasa, tangu tuanze kuambiwa kuna wizi wa mali za Taifa, ni nini tulichopata au kulipwa, zaidi ya sisi kuwalipa ili kukomboa ndege?

Watanzania tutumie akili kutenganisha hadaa na ukweli. Mambo madogo yanakuzwa sana kuwa makubwa na makubwa yanafunikwa. Halafu tunashangilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…