Visa vya Wanawake wa Wrong Number

Saad30

JF-Expert Member
May 26, 2020
1,815
3,637
Salamu wakuu.

Asee leo nina mzuka wa kutoa stori ya wrong number.

Asee katika miaka yangu ya ujana sina kazi ila najishughurisha tu na mitikasi ya mtaani, sasa sku moja nimechil geto nikasema wacha nikosee number mara mbili ilienda kwa machizi na kuwambia wrong number sasa mara ya tatu ikaenda kwa manzi.

Nikamuuliza asee vanessa umepata hiyo hela ya nauli alivyojibu hela gani na nauli ya kwenda wapi basi akawa kaingia kwenye mtego.

Nikamwambia basi samahani nilikuwa namtumia sister alikuwa anaenda kwenye kongamano ya mtoto Yesu.

Akaniambia wewe kaka muongo sana na umekosea namba. Akakata simu nikamtumia 25k palepale.

Dakika tano nyingi akauliza wewe ndio umetuma hii hela 25k nikamjibu ndiyo.

Basi story zikaanza kumbe mtoto anaitwa PENDO yupo mkoani jiji la mbeya...story zilinoga sana na siku ikapita.

Kama wiki hivi likaja jambo la kutumiana picha. MBEYA MBEYA MBEYA 😂😂😂😂 daah alinikata sana yule manzi hakuwa na smartphone ila akatumia akili moja kuniambia nimtue email yangu basi ikawa poa sana.

Kama siku kadhaa akaniambia naenda kukutumia picha mpenzi nikamuliza wapi akajibu internet cafe.

Asee nikaona picha za manzi duuh kweli yule ni pendo staki kuwasema vibaya sisters wa mbeya ila yule kweli alikuwa ni pendo na upendo ukaishia baada ya kuona picha.

Huyu mwingine ni story ndefu sana nina mwaka wa 9 sjawahi kumuona kamaliza Olevel, Alevel, university na sasa kazalishwa..HONGERENI SISTERS WA KICHAGA MARANGU MMENISHIKA AKILI.

wrong number wako ilikuwaje mkuu?
 
Back
Top Bottom