Visa vya mapenzi visivyosahaulika

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Nikiwa nimemaliza kidato cha nne miaka ya 2000's kweusi nikawa nimechill tu home hakuna ishu hakuna mpango, mjini hakuna mashamba. Kwa hiyo nikawa busy na mapenzi na by that time nilikua nimemzimia kwa binti mmoja hivi anakaa mtaa wa tatu tokea home.

Tulikuwa tunapendana sana yaani hata Mitume wangeingilia kati tusingeachana. Sasa binti alikua yuko kidato cha tatu na anasoma shule ya kutwa na kwao hua yupo yeye, wazazi na beki tatu tu, binti nikamzoesha michezo hii ya mapenzi akawa amezoea hadi ikafikia kipindi sasa tukawa tunafanya mapenzi nyumbani kwao bila woga.

Siku moja binti akawa amewahi kutoka shuleni, akanipitia home tukaenda kwao, tukajifungia chumbani kwake, na beki tatu wao hakuaga na shida kwa sababu tulikua tunamtoa toa sana vishilingi, beki tatu mwenyewe hajui kiswahili vizuri wamemtoa vijiji vya ujima huko hivyo nyumba ilikuwa yetu. Sasa hii siku tuko chumbani kwa binti tukasikia kama kikundi cha watu kimeingia ndani.

Kumbe walikua ni baba ake na binti, mama yaake, mashangazi na wana ukoo, wazazi walienda kuwapokea wana ukoo kutoka vijijini wamekuja mjini kwenye sherehe ya ndugu yao mwingine.

Sitokuja kuisahau hii siku, kwanza ilikua mchana na sio muda sahii wa kutoka shule, binti ametoka tu nje wazazi wake wote wakamvaa kwanini ametoroka shule, baba yake akamwambia akachume fimbo huo ujinga hautaki ndani ya nyumba yake. Mind you mie niko chumbani kwake na yote yanayoendelea nayasikia.

Ghafla nikaanza kuona kwamba wezi walioiba sokoni hua wanakufa vipi. Israel mtoa roho huwa anakuja na marungu ya namna gani. Lakin pia nikaona kwamba motoni kunafananaje. So kuokoa nafsi ikabidi nizame chini ya uvungu. Malaika wa haki ni kwamba walisimama mlangoni pale sio baba sio mama sio mashangazi waliokuja chumba cha binti yao. Binti akawa na kazi ya kuja kunichungulia na kuongea maneno kama mwehu.

Wakuu nilikaa chini ya uvungu kwa muda wa siku mbili, binti alikua ananiletea maandazi na maji na wali kiasi halafu kesho yake akaenda shule akanifungia ndani.

Nilivyotoka ilikua ni miujiza maana ukoo ule uliaga ukaondoka nyumba ikawa huru, kule home walinitafuta sehem zote bara na visiwani sikupatikanika wakajua wanga wamenichukua msukule. Nilivyorudi wakafanya party ila siri hiyo nilikuja kuwaambia miaka mingi mbele.

Kisa cha pili.

Nikiwa chuo, miaka ya elfu mbili kweupe hapa, J.K Rais enzi izo wanachuo tunashinda kwenye ma bar japo boom ilo enzi izo sio sawa na la sasa.

Nikiwa chuo nilikua nimepanga gheto mwenyewe, chumba cha jirani kulikua na ndugu yangu wa dhati kabisa, huyu bwana alikua ni wale wanaopenda kufa yaanI akimpenda mtu anakua hadi anakera. Sasa ndugu yangu huyu alikua anampenda mwanafunzi kidato cha nne enzi izo na ka binti kalikua nako kanamuelewa ndugu yangu na enzi izo hapa bongo ukisema wewe ni mwanachuo nchi nzima wanakuogopa sababu la saba walikua ni wengi kila kona.

Siku moja akafanya risk kubwa sana alimuita huyu mwanafunzi akampanga kwamba ukitoka shule kesho pitia hapo kwake, so kabinti kakatii kesho yake kakawa kamefika. Kuja kustuka ni saa tatu usiku, binti anakaa mbali akagoma kuondoka akasema ataenda kesho ila ata tunga uongo tu kwao. Kumbe huku nyuma wazazi wa huyu binti walishamtafuta binti yao kwa marafiki zake wote na kwa ndugu wakamkosa.

Binti kesho amewasha tu simu, akapigiwa na dingi yake basi dingi likampa vitisho ambavyo likasema 'ukirudi nyumbani nakuchinja kwa msumeno', Binti ikabidi aogope na hapo ndio matatizo yalipo anzia. Kuanzia siku hio jamaa akaanza kuishi na binti na ndugu yangu nae mshamba akajua amesusiwa sasa muda wa kujipigia atakavyo, huku nyuma msako ukatengamaa binti akajulikana yuko wapi. Usiku mmoja tukashangaa mamwera hawa hapa wameizunguka nyumba yote na tena tuka kamatwa nyumba nzima ila sie wakatuachia siku ile ile. Mshikaji wangu na binti wakaenda ndani. Jamaa akapewa kesi ya kutembea na mwanafunzi, kumtorosha and so. miaka 30 hio hapo. Na amekamatwa redhanded.

Kilichotokea jamaa ilibidi kule kijijin kwao wauze ng'ombe zote na mashamba kuja kutembeza mrungula huku town ndio mambo kusettle na kesi haikufika kwa ponsio pilato ila jamaa akatengwa na wana ukoo na miezi michache mbele yule binti akaolewa na mtu mwingine na ndugu yangu akarudi zake kijijini.

Visa ni vingi, nimechoka kuandika ila nitakua navishusha vingine huku nikisaidizana na nyinyi, leteni visa vyenu au mlivyowahi kuvishuhudia
 
Nikiwa nimemaliza kidato cha nne miaka ya 2000's kweusi nikawa nimechill tu home hakuna ishu hakuna mpango, mjini hakuna mashamba. So nikawa bize na mapenzi na by that time nilikua nimefall kinyama kwa binti mmoja iv anakaa mtaa wa tatu tokea home.
Bro wewe ni nomaaa aiseee upo nondoo...
 
Kuna demu nilikuwa napiga, alishakuja kulala kwangu mara kadhaa.

Nilikuwa nikitaka kumtia namtuma bodaboda ninaejuana nae anamfata anamleta geto.

Siku nimetoka safari, ilikuwa usiku na mkuyenge ulikuwa unahitaji, kama kawaida yangu nikamtuma boda wangu akamchukue yule dem, ilikuwa majira ya saa 4 usiku, lakini mpaka saa tano unusu boda hajafika na yule manzi, nikipiga simu ya yule manzi haipatikani, yule boda haipokelewi, nikajua huenda yule boda anamkaza yule demu, fasta tu nikachukua boda mpaka mazingira anayoishi yule duu, nikaenda hadi dirishani nasikiliza, nikawa nasikia kama miguno, hasira zikanipanda nikamuita yule demu kwa nguvu, nikazunguka hadi mlangoni.

Ile nakaribia tu mlangoni, mlango ukafunguliwa likatoka libraza tolu flani, nikaona hii ni hatari ikabidi nigeuze nianze kutoka mkuku, lile lijamaa lilirusha kitu kama rungu, kama sio mchi wa kinu, likanipiga begani, nilianguka, nikajitahidi kukimbia mpaka geto, hapo hadi ndala niliziacha palepale, geto pekupeku na pensi na tshirt, kesho nakuja kupata stori kwa yule boda kuwa kumbe jana yake lilimtaitisha, boda akajitetea sana ndo likamuacha, kumbe alikuwa mke wa lile jamaa.

Demu akaja kuniona geto nikamwambia aende tu kwa mumewe mana nilitaka kufa kwa ajili yake.

Niliuguza bega miezi mitatu.
 
Kuna demu nilikuwa napiga, alishakuja kulala kwangu mara kadhaa.

Nilikuwa nikitaka kumtia namtuma bodaboda ninaejuana nae anamfata anamleta geto.

Siku nimetoka safari, ilikuwa usiku na mb.oo ilikuwa Inahitaji, kama kawaida yangu nikamtuma boda wangu akamchukue yule dem, ilikuwa majira ya saa 4 usiku, lakini mpaka saa tano unusu boda hajafika na yule manzi, nikipiga simu ya yule manzi haipatikani, yule boda haipokelewi, nikajua huenda yule boda anamkaza yule demu, fasta tu nikachukua boda mpaka mazingira anayoishi yule duu, nikaenda hadi dirishani nasikiliza, nikawa nasikia kama miguno, hasira zikanipanda nikamuita yule demu kwa nguvu, nikazunguka hadi mlangoni.

Ile nakaribia tu mlangoni, mlango ukafunguliwa likatoka libraza tolu flani, nikaona hii ni hatari ikabidi nigeuze nianze kutoka mkuku, lile lijamaa lilirusha kitu kama rungu, kama sio mchi wa kinu, likanipiga begani, nilianguka, nikajitahidi kukimbia mpaka geto, hapo hadi ndala niliziacha palepale, geto pekupeku na pensi na tshirt, kesho nakuja kupata stori kwa yule boda kuwa kumbe jana yake nilimtaitisha, boda akajitetea sana ndo likamuacha, kumbe alikuwa mke wa lile jamaa.

Demu akaja kuniona geto nikamwambia aende tu kwa mumewe mana nilitaka kufa kwa ajili yake.

Niliuguza bega miezi mitatu.
Hahahaha nimecheka sana

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom