Visa nilivyoshuhudia kwa ndugu yangu Mtaalam wa Tiba za Asili

kuna muda mwanangu alipandisha homa, yan homa haisikii panadol ya maji wala ya kidonge, niliagizia hilo fusho, halaf uzurkwangu nimezungukwa na hio miti, miarobaini, mikunde pori, kivumbasi na majani ya mvuje, niliyachuma nikayachanganya kwa pamoja nikaweka maji nikafunika mvuke usitoke nikalibandika jikoni likachemka nikamuogeshea mtoto homa lilipungua na tukalala vzr tu

ndio nikaambiwa pia mavi ya tembo uchanganye na majani ya vitunguu swaum na majani ya mvuje yaliokaushwa unachoma moshi wake ukijifukiza tiba nzur sana ya homa isioshuka
Ni kweli ila kwenye mvuje na mavi ya tembo ukikosa mvuje ndio unachanganya majani ya vitunguu swaum na mavi ya tembo tiba nzuri sana
 
Uchawi upo aisee, miaka ya nyuma kidogo sitakuja kusahau siku niliopotea wakati sehemu niliokua naenda naijua kwa asilimia 100.

Nimetoka ubungo na daladala nimeshuka tegeta kwa ndevu kuelekea kwa mama mdogo nilikokuwa nakaa lakini cha kushangaza baada ya kushuka kwenye dala dala njia ya kuelekea home nikaisahau.
Nilizunguka karibia saa nzima naitafuta njia ya kwenda nakokaa baadae ufahamu ulivyorudi nikaona kama watu wananishangaa. Na maeneo niliokuwa nazunguka ni maeneo yale yale ya njia ya kuelekea ninakokaa.
Itakuwa ulikanyaga mdudu mbaya.
 
Kivumbasi
inapunguza tumbo hii
Unachemsha ikiwa mbichi unakunywa kama chai kila asubuhi na wakati wa kulala huku ukipunguza kiwango cha ulaji wako hii chapchap inajibu,
inapandisha nyota kwa kunywa na kuoga
Inavuta wateja katika biashara uoteshe mjani huu ndani ya ofisi yako
Huo mmea unatuliza mme haraka mno ukiusaga na kuichanganya na unga wa mchekea mtilie katika mlo wake au kwa chambia huko down

Unafukuza vitu vibaya ndani ya nyumba au ofisi yako ponda majani mabichi ya jani hilo kisha changanya na maji mwaga au dekia ndani mwako

Vilevile ni nzuri kwa watoto wasiotembea vizuri uikaushe ichome jivu lake chemsha na soda ya fanta orange na ndimu 7 mfushe mwanao na umuogeshee atatembea haraka na ataongea zaidi.

Jani hilo pia huandaliwa kama kinga ya nyumba au mwili huchukuliwa viza hutobolewa matundu matundu kisha hunyunyiziwa unga wa jani hili na kufungwa na kitambaa cheusi kisha huzikwa upande wa magharibi na mashariki mwa nyumba yako hakika hatui mbaya nyumbani kwako.

Baadhi ya matumizi yake kama dawa
Nitautumia kuogea.
 
Inaendelea.....SEHEMU YA SITA

Ndugu zangu nifafanue kidogo, nilikuwa siamini haya mambo hapo awali na jambo usipoliamini usilipinge bali tafuta ukweli wake kwa waliozama katika fani hiyo...naam ndivyo nilivyofanya na ndiyo maana nikawa karibu na nikawa ni mfano wa msaidizi au kwa lugha zao wanaita mwana maji na hapo ndipo nikajua mengi na sasa naamini sana uwepo wa nguvu hizi kwani pengine zingenitoa roho kama si Mungu mwenyewe.

Wakati yule kiumbe namfuata nilikuwa kama zezeta fulani au kama nipo kwenye ndoto ila naona kila kitu lakini mwili siwezi kujizuia hivyo nikafungua mlango na kumfuata huku yeye akiongoza mbele.

Kitendo cha kufungua mlango na kuuacha wazi ulirudi wenyewe na kujifunga kwa nguvu na hilo likaenda sambamba na mganga kupandisha ndani kwake na kutoka nje haraka huku akifuatwa na mkewe na ndipo walipokuja kunikuta nyuma ya uchochoro wa nyumba nikitembea kama zuzu! Hapo nikarudishwa na nilipokuja kuzinduka (nilipoteza fahamu) ndipo nikaambiwa nimeaguliwa sana ndiyo pona yangu lakini ilikuwa niende na maji na kwamba yule aliyekuja ni jini la kichawi limetumwa kunichukua mimi ili wakanipoteze na ameyafanya yote hayo chini ya uangalizi maalum wa wachawi wale wale wanaoona uchungu kuaguliwa kwa yule binti, alitakiwa aachwe afe!!

Nikauliza sasa mimi nahusika na nini na vita vyenu huu si uonevu?

Mganga akasema hapana, ni sahihi kufanyiwa haya wewe maana wameshindwa kuyatekeleza haya kwangu, kwa mke wangu na wanangu maana wamekula miti mingi, hivyo kwa namna yeyote wanatafuta mahali pa kuniliza, nijutie na nilie kwa kusaga meno na hapo ndipo ilipoonekana panapofaa ni kwako!! Na wewe ni mbishi ulipoingia tu nilikwambia nikutengeneze huku si kuzuri na ukikaa nyumba hii upo vitani ila ukanijibu urogwe una nini, si wangerogwa akina Bakhressa wewe urogwe kwa lipi.

Nikakosa cha kusema na kwa mara ya kwanza nikaandikiwa makombe na madawa yenye harufu mbaya mbaya kujifukiza na hapo ndipo nikawa sawa hata kichwa na uchovu vikaacha na ukapita mwezi mzima salama salmini.

Siku moja ni kama ilianza na shughuli mbaya mbaya tangu kulipokucha kwani alikuja dada mmoja amedhoofu sana lakini kwa macho anaonekana ni mzima, huyu alikuja akiwa na majonzi huku machozi yakimlenga! Akatusalimia na kukaribishwa kilingeni, akamwambia mganga unanikumbuka? Akajibiwa kwa mfumo wa swali, "naam si yule uliyechukuliwa mpenzi wako?

Dada akajibu; "ndiyo kaka, nilikuja nikakwambia nina rafiki yangu ananichukulia mtu wangu hali akijua kabisa hivyo nikataka tumuondoe na ukaniagiza jogoo jekundu, sanda na pweza mbichi, tukaenda kufanya kazi kaburini na yule pweza tukamzika huko....
Mganga akadakia; "vipi maendeleo je bado tuongeze nguvu? Maana sikukuona tena ni miezi sasa na nilikwambia uniambie maendeleo yake".

Dada akaendelea; "mh! Kwanza yule mtu ni ndugu yangu tumbo moja sema nilimleta kwangu baada ya kufeli masomo yake ya kidato cha nne hivyo baada ya kupata kazi na kuondoka kwangu nikaja kugundua anatembea na shemeji yake kwa ushahidi wa sms kabisa na nilipomuuliza ndugu yangu akaanza maneno ya kejeli! Iliniuma sana ndiyo nikaja kwako na nikakwambia ni rafiki ili unitendee jambo langu bila maswali mengi.

Mganga akadakia; "aisee!!

Dada akaendelea; "baada ya ile shughuli ndugu yangu akaanza kuumwa sana wazazi wakamaliza tiba za kizungu na kushauriwa tujaribu kienyeji, tumezaliwa sisi wawili tu hivyo ikawa kila msafara na mimi niwepo kwenye kuuguza na tulikwenda Pemba, Pangani na hata Turiani lakini kote huko ramli zilisema KIKULACHO KI NGUONI MWAKO bila kutaja nani adui ila walimuagua bila mafanikio yeyote...na sasa hivi yupo tu nyumbani hali mbaya amekwisha na mwili unanuka maana ana mapele yanatoka maji kama Pweza na kila akikaa ananyanyua mikono juu kumuomba Mungu amchukue kwani anateseka....nimeuza kila kitu na nimekonda hivi sababu ya mawazo na kujutia hivyo naomba tumlete kwako umuague apone.

Mganga akajibu kwa chuki; watu mbona mna matatizo? Yasingempata uliyoyataka ungesema mimi si mganga sasa leo hii unaleta kigeugeu! Siwezi kumuopoa nilisema tangu mwanzo kuwa atakaeweza kumuagua huyo ni atakaeweza kumpata pweza tuliyemzika...na sasa si ameshakuwa mchanga!! Haaguliki mama nenda kapumzike!!

Yule dada akaanza kulia kwa sauti huku akisema; "nisaidie ndugu yangu anakufa jamani umemuua ndugu yangu, huyo mpenzi wangu mwenyewe pia ametuacha sote na sasa hivi ameoa mwanamke mwengine...

Inaendelea....
Ushezi huu kisa mapenzi kaenda kuloga
 
Kwa upande mwingine huwa kama una uhakika mtu hajafa kifo cha halali huwa inatengenezwa dawa kabla ya arobaini ya marehemu hufukiwa kaburini marehemu mwenyewe mzimu wake utaamka kumaliza chain yote iliyohusika na huo utopolo, wanaumiza sana familia kwa chuki ndogo ndogo au ugomvi mdogo mdogo mwingine anajivunia kujua hiyo sanaa anasababisha kifo nna ndugu yangu alipishana kiswahili tu kuhusu mwanamke jamaa akakuendea Tanga ikawa siku moja anarudi nyumbani kwake alipopita watoto walikua wanaendelea na michezo yao mmoja kati ya wale watoto akarusha jiwe kawaida tu halikua na nguvu likampiga mguuni baada ya muda ule mguu ulianza kumsumbua taratibu ukaanza badilika rangi kuwa mweusi kama mtu alieungua wakahangaika sana kila wanapoenda wanaambiwa wamechelewa nikaja kukutana na mdogo wa marehemu akanielezea nikamwambia acha na mimi nione kuna nini jibu likawa lile lile kupishana kiswahili na huyo mtu akamsafiria na kweli muda ulikua umeenda kutengua kile kilichofanywa, tulikutana ndugu wa kiume hiyo siku hospital alikua anapata tiba ambayo walijua haiwezi saidia lolote tukakubaliana hadi hapo hamna namna ni kurudisha majibu upande wa pili wakanipa jukumu nikaomba kwa walimu tunashkuru kabla ya kumstiri ndugu yetu alianza kustiriwa mganga kisha yule alieenda kufanya ule ubaya.Kuna ubaya huwa hauvumiliki
Ikitokea mzimu umezidiwa nguvu na mtu kwenye hiyo chain nn kitatokea nicksonmoses
 
Mwaka 2014 huko wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya. Kuna Binti wa around miaka 16 au 17 alipakizwa na kaka yake kwenye baiskeli. Sasa wakati wa kushuka kwenye baiskeli aliteguka mguu, na hapo ndio alianza kuumwa huo mguu.

Ule mguu ulimsumbua sana. Walihangaika naye alikuja kufia Muhimbili.
 
Huwa hawapatani na mtu anayewaharibia kazi yao,kuna mchungaji wa kkkt alipangiwa hko kwetu sasa yeye ni mtu wa maombi na wachawi wakija kanisani anawaona anawatimua au akija kwako anakwambia nenda sehemu fulani toa hiki na kile kimewekwa nyumbani kwako bas bwana akawakosesha wachawi raha sasa mapambano yakaanza anakwambia usiku hawalali ni wanakesha wanaomba maana wachawi wamezunguka nyumba kila mtu anajaribu uwezo wake basi mda si mrefu wakamtorosha mtoto wake alikuwa anaingia form five baada ya mda akapatikana hajakaa mda wakakuta amejinyonga na ndo alikuwa anajiandaa kwenda form five ikabid mchungaji wetu wamwamishe tena,wachawi wakasherekea na kunywa bia maana walikuwa hawamtaki katukatu

noma
 
Back
Top Bottom