Visa na mkasa vya wavuta bange wa zamani; ni dhahiri bangi ya siku hizi haina madhara

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Kuna watu bangi zimewapa maisha lakini kuna wengine zimewaharibia maisha yao yote!
Bangi za zamani zilikuwa mbaya sana! pafu moja tu inamkaa mtu miaka saba! ni tofauti sana na hii iliyochakachuliwa siku hizi.
Kisa cha abdallah mibange

Huko Kateshi,
Aliwahi kuwepo bwana mmoja mvuta bangi kwelikweli, alijulikana kwa jina la Abdallah- Mibange, huyo bwana pia hakuwa na lelemama juu ya kula,alikuwa anakula kilo moja peke akesana, mke wake alikuwa akimpikia ugali kilo nzima ya unga peke ake na habakishi, Abdallah mibange alifanikiwa kupata kazi ya ulinzi kwenye moja ya mashamba ya wazungu, alikuwa ni mkatili sana, ng'ombe za wafugaji zilizoonekana kuingia shamba la mzungu alikuwa anazifyeka na mapanga,watu walimuogoba sana abdallah mipange!
Basi Abdallah mibange aliwahi anzisha ujenzi wa nyumba yake vyumba viwili, ile nyumba alianza kwa kujenga boma, alivyomaliza kabla ya kuweka bati yeye akaanza na tailizi, ikakaa kama mwaka mzima hv, bdae akaweka milango na madirisha, ikakaa tena miaka miwili ndipo badae akaezeka nyumba yake kwa mabati ya madebe ya mafuta (korie).

Abdallah Mibange pia alikuwa haendi kwenye misiba, siku moja msiba ukatokea kwa jilani yake, abdallah mibange hakwenda msibani zaidi zaidi akaenda kuvuta bangi bdae akarudi akasimama nje ya nyumba yake akaanza kuwaita wale watu pale msibani, nyie waseng3 mtakufa sana na uchawi wenu: kwakuwa walisha mzoea Wakamwacha tu akatukana wee bdae akalala.

Mke wa abdallah mipange baada ya kuchoshwa na visa vya mmewe! akafikilia labda wakimtisha kumfunga jera atabadilika, akaandaa mtego wakamkamata, lakini mkewe akaongea na hakimu asimfunge; alitaka alipishwe faini tu halafu yeye mkewe atalipia ili mmewe asifungwe lengo likiwa ni kumtisha tu ili abadili tabia yake.
Siku ya hukumu ikafika, Abdallah akiwa kizimbani kusomewa hukumu.
HAKIMU akaita; Abdallah khalifani......! Mtuhumiwa Abdallah akaitikia!.."Sema Muniyoo!!, HAKIMU akarudia tena; Abdallah Khalifan; Mtuhumiwa akitikia tena; sema mk*ndu muniyo!!(muniyo kwa Kinyaturu maanake ni ile sehemu ya kutolea haja kubwa) BASI HAKIMU pale pale AKAMHUKUMU Abdallah mabange kwenda jela miaka 3,
Baada ya kutoka jela abdallah mibange hakubadilika akaendelea na ukorofi wake;
siku moja akapita kituo cha polisi Kateshi akakuta wamepanda maua, naye akapanda bangi kwenye yale maua polisi hawakumuona.
basi akawa kila siku akipita pale anaimba " Polisi wanakamata bange na wanalima bange!..miezi ikasogea wimbo wake ukiwa huohuo, polisi walimsikia lakini hawakujali wakajua kachanganyikiwa!. baada ya bangi kustawi polisi ndo wakagundua kuna bangi kwenye maua yao! wakahisi ni yuleyule abdallah mibange anaeimba kila siku.Basi wakamsubilia.

Abdallah mibange siku akapita polisi wakamuona wakamuita, Abdallah Njoo!...tuambie hii ni nini?..Abdallah mibange akawajibu ...MULIVYOKUWA MNAPANDA MLIFIKILI MATAKO?...huyo akaondoka zake....
nahisi hizi bangi zinatofautiana
 
Kweli bangi za siku hizi hazina madhara...siyo kwa stori hii
 
Bangi ni bangi tu sema labda mitindo ya uvutaji ndio inaweza kutofautiana huyu analikoka hivi mwingine analipuliza vile ili mradi tafrani. Bibi yangu mzaa mama alikuwa anajifukiza bangi anapoumwa kichwa anaweka chetezo chake chini, anajifunika kanga mwili mzima akitoka hapo jicho jekundu na kichwa kimepona.
 
Back
Top Bottom