Hivi karibuni Trump amepitisha sheria kwa baadhi ya nchi raia wake wakiingia Marekani waingie kwa Visa bond. Imewekwa bayana ni dola5000 naomba anayejua hii maana yake nini hasa.
Ni dhamana ya kifedha ili kuruhusiwa kuingia US,
Kuhakikisha kwamba unaondoka kihalali bila ku overstay,ni dhamana ya kifedha ambazo utarudishiwa kama utaondoka pale visa yako itakapokua imekwisha muda wake wa wewe kua ndani ya US.
Dhamana au deposit ya kifedha
Inatumika kwa muombaji wa visa au sponsor wake, kwa Tanzania pia inatumika unapomuajiri mgeni au hata kama mwajiriwa kutoka nje kwa familia yake
Nchi nyngi hasa za kiarabu wanatumia kwa makampuni yanayoajiri kutoka nje ndio maana wengi wanazuia passport za waajiriwa wao
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.