Virusi vya Corona: Zanzibar Yapokea Mashine Yenye Uwezo wa Kupima Watu 288 kwa Siku

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Zanzibar imepokea mashine moja yenye uwezo wa kupima sampuli 288 kwa saa 24. Mashine nyingine mbili zilizoagizwa zitafika nchini humo muda wowote kuanzia sasa.

Zanzibar iliazimia kuwa na Maabara ya kisasa ya kupima COVID19 nchini humo ili wasiwe wanatuma sampuli kwenye maabara zilizoko Dar es Salaam.

Mara ya mwisho kwenye taarifa yao Zanzibar walitangaza kuwa na visa 134, na vifo 5.

======

1589549887643.png
IMG-20200515-WA0028.jpg
 
Mimi naomba kuzijua hizo mashine kwa picha maana nasikiaga tu watu wanapimwa corona na sijui wanapimajwe.
 
Mimi nashauri kabla hazijaanza kazi na zenyewe zipimwe kwanza kama hazina maambukizi...
 
Zanzibar imepokea mashine ya kupimia ugonjwa wa homa kali ya mapafu, Corona, kufuatia agizo la Rais Dk Ali Mohamed Shein kwa Wizara ya Afya kufanikisha upatikanaji wa mashine za kupimia ndani ya miezi mitatu.

Mashine zingine mbili zinatarajiwa kupokelea wakati wowote, na zitafungwa visiwani Unguja na Pemba, imesema taarifa kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Mashine hii iliyopokelewa leo, inauwezo wa kutoa majibu ndani ya saa nane kwa vipimo vya watu 96.

"…hivyo kwa saa 24, ina uwezo wa kutoa majibu ya vipimo 288," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kupokewa kwa mashine hii kunakuja wakati ambapo vipimo vya COVID-19 vimesimama kutolewa Tanzania bara kupisha uchunguzi katika maabara ya taifa.

Uchunguzi huu ulikuja baada ya Rais John Magufuli kutilia shaka utendaji kazi wa vifaa na wataalamu wa maabara hiyo ambapo alidai pamekuwa na utoaji wa majibu 'positive' mengi kuliko kawaida katika maabara hiyo.

Zanzibar pia wamekuwa wakitumia maabara hiyo.

Shirika la afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika na kituo cha kupambana na kuzuia maradhi kilicho chini ya Umoja wa Afrika (Africa CDC) hata hivyo walitupilia mbali madai haya ya Magufuli.

Walisema vifaa pamoja na wataalamu walioko katika maabara ya Tanzania wana ufanisi kama ule ule walionao wataalamu na vifaa vinavyotumika kote barani Afrika.

Jana Alhamisi, Africa CDC iliitaka Tanzania kutoa takwimu mpya za mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini humo.

Mkurugenzi wa Africa CDC, Dkt John Nkengasong amesema kuwa kituo chake kwa kutumia takwimu hizo kipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia msaada wa kitaalamu na kiufundi unaohitajika.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Mkurugenzi wa Africa CDC Dkt John Nkengasong amesema kituo chake kipo tayari kushirikiana na Tanzania.
"Hili ni janga kubwa kwa bara (Afrika) lote na dunia kwa ujumla… hivyo ni kwa faida ya Tanzania kutoa takwimu kwa wakati ili tufahamu mapungufu yapo wapi na tuwasiadie kadri itakavyohitajika," alisema Dkt Nkengasong katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao.

Mara ya mwisho kwa Zanzibar kutangaza takwimu mpya ilikuwa ni Jumatano ya wiki ilopita Mei 7. Huku Tanzania Bara ikitoa takwimu za mwisho Aprili 29.

Mpaka sasa taarifa rasmi zinaonesha kuwa kwa ujumla wake Tanzania kuna wagonjwa wa Corona 509, waliopona 183 na waliofariki kutokana na maradhi hayo ni 21.
--------- BBC Swahili ---------
 
Na Bara bado wanang’aa macho huku wakiendelea kuficha idadi ya wagonjwa wapya kwa wiki ya pili.
Hivi mkuu unajua uliuliziwa sana hapa...
Alafu umekuja kisimposimpo tu bila taarifa..

Ulikua wapi!??
 
Inapendeza kujua je wale ambao wanapima watu 1000 au 2000 kwa siku, wamefanikiwa ktk kuutolomeza ugonjwa?
 
Sasa naanza kuamini iwapo Zanzibar ingekuwa ni nchi Huru badala ya kuwa Koloni la Nchi isiyojulikana ya Tanganyika, huenda ingepiga hatua kubwa sana Kiuchumi, Kisiasa na pia Kijamii.

Wazanzibar wana umoja, ni Wazalendo wa kweli kwa Nchi yao, Viongozi wao wanawajali sana Wapiga kura wao, nk. Nimefurahi walivyo jiongeza. Huku Bara ni bla bla tu na porojo nyingi! Haiwezekani mpaka leo eti mashine ya kupimia hizo sampuli iko Dar tu.

Hongereni Wazanzibari, Hongera sana Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein! Wewe ni Rais wa kweli! Ulijiandaa na kuandaliwa! Ni mtu usiye na makuu! I wish ungekuwa ni Rais wa Tanzania.
 
Nilikuwa chato Mkuu nabangaiza ila hapo kuja kisimposimpo tu nimetabasamu kwani ulitaka nitoe taarifa kama ipi na wapi? 😂😂😂

Hivi mkuu unajua uliuliziwa sana hapa...
Alafu umekuja kisimposimpo tu bila taarifa..

Ulikua wapi!??
 
Naunga mkono hoja Mkuu, hii coronavirus imeonyesha ukomavu mkubwa wa Zenj kufanya maamuzi muafaka kwa wananchi wao ukilinganisha na Bara kulikojaa UNAFIKI.

Sasa naanza kuamini iwapo Zanzibar ingekuwa ni nchi Huru badala ya kuwa Koloni la Nchi isiyojulikana ya Tanganyika, huenda ingepiga hatua kubwa sana Kiuchumi, Kisiasa na pia Kijamii.

Wazanzibar wana umoja, ni Wazalendo wa kweli kwa Nchi yao, Viongozi wao wanawajali sana Wapiga kura wao, nk. Nimefurahi walivyo jiongeza. Huku Bara ni bla bla tu na porojo nyingi! Haiwezekani mpaka leo eti mashine ya kupimia hizo sampuli iko Dar tu.

Hongereni Wazanzibari, Hongera sana Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein! Wewe ni Rais wa kweli! Ulijiandaa na kuandaliwa! Ni mtu usiye na makuu! I wish ungekuwa ni Rais wa Tanzania.
 
Nilikuwa chato Mkuu nabangaiza ila hapo kuja kisimposimpo tu nimetabasamu kwani ulitaka nitoe taarifa kama ipi na wapi? 😂😂😂

Popote tu. Ulitafutwa sana. Tunataka utuambie ulikua wapi... Kama ulitekwa au la!?

Alafu saivi umepunguza moto wako. Sio wewe tunae kujua.

Tuambie nini kilikukuta. Hata kama umeamua kuunga juhudi sio mbaya.
 
Zanzibar imepokea mashine ya kupimia ugonjwa wa homa kali ya mapafu, Corona, kufuatia agizo la Rais Dk Ali Mohamed Shein kwa Wizara ya Afya kufanikisha upatikanaji wa mashine za kupimia ndani ya miezi mitatu.

Mashine zingine mbili zinatarajiwa kupokelea wakati wowote, na zitafungwa visiwani Unguja na Pemba, imesema taarifa kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Mashine hii iliyopokelewa leo, inauwezo wa kutoa majibu ndani ya saa nane kwa vipimo vya watu 96.

"…hivyo kwa saa 24, ina uwezo wa kutoa majibu ya vipimo 288," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kupokewa kwa mashine hii kunakuja wakati ambapo vipimo vya COVID-19 vimesimama kutolewa Tanzania bara kupisha uchunguzi katika maabara ya taifa.

Uchunguzi huu ulikuja baada ya Rais John Magufuli kutilia shaka utendaji kazi wa vifaa na wataalamu wa maabara hiyo ambapo alidai pamekuwa na utoaji wa majibu 'positive' mengi kuliko kawaida katika maabara hiyo.

Zanzibar pia wamekuwa wakitumia maabara hiyo.

Shirika la afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika na kituo cha kupambana na kuzuia maradhi kilicho chini ya Umoja wa Afrika (Africa CDC) hata hivyo walitupilia mbali madai haya ya Magufuli.

Walisema vifaa pamoja na wataalamu walioko katika maabara ya Tanzania wana ufanisi kama ule ule walionao wataalamu na vifaa vinavyotumika kote barani Afrika.

Jana Alhamisi, Africa CDC iliitaka Tanzania kutoa takwimu mpya za mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini humo.

Mkurugenzi wa Africa CDC, Dkt John Nkengasong amesema kuwa kituo chake kwa kutumia takwimu hizo kipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia msaada wa kitaalamu na kiufundi unaohitajika.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Mkurugenzi wa Africa CDC Dkt John Nkengasong amesema kituo chake kipo tayari kushirikiana na Tanzania.
"Hili ni janga kubwa kwa bara (Afrika) lote na dunia kwa ujumla… hivyo ni kwa faida ya Tanzania kutoa takwimu kwa wakati ili tufahamu mapungufu yapo wapi na tuwasiadie kadri itakavyohitajika," alisema Dkt Nkengasong katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao.

Mara ya mwisho kwa Zanzibar kutangaza takwimu mpya ilikuwa ni Jumatano ya wiki ilopita Mei 7. Huku Tanzania Bara ikitoa takwimu za mwisho Aprili 29.

Mpaka sasa taarifa rasmi zinaonesha kuwa kwa ujumla wake Tanzania kuna wagonjwa wa Corona 509, waliopona 183 na waliofariki kutokana na maradhi hayo ni 21.
--------- BBC Swahili ---------
ni habari njema, mungu ibariki zanzibbar. Udumu muungano
 
Back
Top Bottom