Mzee23
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 1,742
- 3,673
Wakati Dunia inapata matumaini ya kudhibiti virusi vya korona baada ya kuidhinishwa chanjo kadhaa, hali ya sintofahamu imeukumba ulimwengu na Sayansi ya utafiti baada ya aina mpya ya virusi vya korona kugunduliwa nchini Uingereza ambayo inaambukiza kwa haraka zaidi ya aina ya kwanza hivyo kutia shaka kuwa hatua zilizopigwa kwenye kupata chanjo zikawa kazi bure!!
Kitaalamu aina hii mpya imetokea baada ya virusi vya korona kubadilika kutoka umbo la awali na kutoa kirusi chenye sehemu za mwili tofauti(new variant). Wataalam wanasema baadhi ya mabadiliko yaliyotokea ni pamoja na kujibadili sehemu inayotumika na kirusi kunasa katika seli ya binadamu, mbaya zaidi ni kuwa chanjo zilizopo zinafanya kazi kwa kuwezesha kinga ya mwili kushambulia sehemu hii ya kirusi inayonasana na seli ya binadamu!! Sasa kwa kubadili umbo hapo itabidi utafiti upya kufanyika kupata chanjo inayoweza kukabili umbo husika!!
Nchi nyingi za Ulaya na sasa India zimezuia usafiri kutoka Uingereza ili kujikinga na aina hii mpya ya virusi vya korona!
Mungu atusaidie sana!
Chanzo: BBC NEWS