Viroja vya kuibiwa mtihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viroja vya kuibiwa mtihani

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by KIGENE, Feb 28, 2011.

 1. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,066
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Kwenye miaka ya themanini ilitokea varangata la aina yake kwenye shule moja ya sekondari pale Morogoro mji kasoro bahari. Wanafunzi walifanya fujo wakaharibu majengo na vifaa kadhaa vya shule. Vagi lilianza hivi:

  Walimu walitunga mitihani ya kumaliza mwaka, kumbe wanafunzi wakafanikiwa kuiba hiyo mitihani na kuanza kuikariri kwa kadri walivyoweza. Kwa hiyo kila mwanafunzi akajilisha kwa nafsi yake kwamba lazima safari hii atafaulu vizuri.

  Kama ilivyo ada siku ya mtihani ikawadia, wanafunzi wakagawiwa karatasi za mitihani. Kwa mshangao wa wanafunzi wakakuta ule sio mtihani waliouiba! Wanafunzi wakapiga kelele na kusema 'walimu huu mtihani sio wenyewe.'

  Wanafunzi baada ya kujua kuwa walimu walishtukia dili na kubadili mitihani wakasema afadhali lawama kuliko fedheha wakasusa mitihani na kuanzisha vurugu.
   
 2. N

  NUHWAHI Senior Member

  #2
  Jun 11, 2015
  Joined: Jan 23, 2014
  Messages: 109
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  hahahahahaaahahahahaaaa
   
 3. ncm

  ncm Member

  #3
  Jun 11, 2015
  Joined: Jun 8, 2015
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hadi raha! Matumizi mazuri ya akili.
   
 4. P

  Partyrobert Member

  #4
  Jun 11, 2015
  Joined: Apr 29, 2015
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hiyo kali bhana
   
 5. Idd Ninga

  Idd Ninga JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2015
  Joined: Nov 18, 2012
  Messages: 1,931
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  wanafunzi wana akili hawa,kama simu ya tochi.
   
 6. Gabmanu

  Gabmanu Senior Member

  #6
  Jun 12, 2015
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajanja... hao
   
 7. Analyse

  Analyse JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2015
  Joined: Jan 19, 2014
  Messages: 3,685
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Hata mm ningemind tu,kwann wabadilishe ghafla?
   
 8. ISO M.CodD

  ISO M.CodD JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2015
  Joined: Feb 17, 2013
  Messages: 2,641
  Likes Received: 835
  Trophy Points: 280
  Mtihani sio wenyewe! Loooh! Hahahahahhaahahhaah
   
 9. C

  Cassie johnson Member

  #9
  Jun 14, 2015
  Joined: Jun 7, 2015
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh! jaman hao walm naooo,c wangeacha ule ule tu
   
 10. m

  masanja the king. Member

  #10
  Jun 14, 2015
  Joined: May 16, 2015
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  theft is there forever
   
Loading...