KIGENE
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,551
- 813
Kwenye miaka ya themanini ilitokea varangata la aina yake kwenye shule moja ya sekondari pale Morogoro mji kasoro bahari. Wanafunzi walifanya fujo wakaharibu majengo na vifaa kadhaa vya shule. Vagi lilianza hivi:
Walimu walitunga mitihani ya kumaliza mwaka, kumbe wanafunzi wakafanikiwa kuiba hiyo mitihani na kuanza kuikariri kwa kadri walivyoweza. Kwa hiyo kila mwanafunzi akajilisha kwa nafsi yake kwamba lazima safari hii atafaulu vizuri.
Kama ilivyo ada siku ya mtihani ikawadia, wanafunzi wakagawiwa karatasi za mitihani. Kwa mshangao wa wanafunzi wakakuta ule sio mtihani waliouiba! Wanafunzi wakapiga kelele na kusema 'walimu huu mtihani sio wenyewe.'
Wanafunzi baada ya kujua kuwa walimu walishtukia dili na kubadili mitihani wakasema afadhali lawama kuliko fedheha wakasusa mitihani na kuanzisha vurugu.