Vipuli vya Sikio la kati

OCC Doctors

Senior Member
Jul 20, 2018
104
151
Kwenye sikio la kati kuna vipuli vitatu (ossicles) ambavyo hupitisha mitetemo ya hewa kutoka sikio la nje hadi sikio la ndani ili kuchakatwa kama sauti.

Kipuli cha kwanza ni 'Malleus' mfupa mdogo wa umbo la nyundo husambaza mitetemo ya sauti hadi kwenye kipuli cha pili kiitwacho 'Incus', ni mfupa wenye umbo la chungu hupitisha mitetemo ya sauti hadi kwenye kipuli cha tatu kiitwacho 'Stapes'.

Stapes ni kipuli cha tatu chenye umbo la kipago katika sikio la kati, kisha husafirisha mitetemo hiyo hadi kwenye majimaji ya sikio la ndani (inner ear fluid).

Insta-ReflectorsAS.jpg
 
Mie sijaelewa huu uzi unahusu nn au ni mambo ya mashine au mitambo?
Sikio la binaadamu limegawika sehemu kuu tatu, sehemu ya nje, sehemu ya kati na sehemu ya ndani.

Uzi huu unahusu mchakato wa kusafirisha mitetemo ya hewa sehemu ya kati ya sikio kwenda sehemu ya ndani ya sikio.
 
Ahaa hapo nimeelewa
...sema huu uzi hautopata wachangiaji wengi labda ungeweka mada inayohusiana na kupigana miti
 
Kwanini mada hizo zinapendwa?
Wabongo wengi wanapenda udaku, kula na kupigana miti maana maisha yenyewe ni stress tu viongozi wanagawana hela huku wananchi wa chini wanalia na kusaga meno sasa hakuna namna inabidi watu waendelee kujifariji kwa starehe tu maana kuwaza kutoboa ni ngumu
 
Ooh sawa sawa. Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom