Vipindi vya redio vinaweza kuvunja ndoa. Please be carefull... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipindi vya redio vinaweza kuvunja ndoa. Please be carefull...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, Oct 28, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kuna mzozo mkubwa umeibuka katika ndoa fulani baada ya mdada mmoja kuwa na mazoea ya kupiga simu redioni kumtakia njozi njema mpenzi wake xxx (akimtaja kwa majina matatu)...

  Jamaa anayetajwa ni mume wa mtu, ambaye ameenda chuo kuongeza ilmu, na kumuacha mkewe akilea familia. katika hali ya kushangaza, kuna dada amejitokeza (na inahisiwa ni wmanachuo mwenzake), anapiga simu kwenye vipindi vya redio kadhaa hasa usiku, kumsalimu na kumtakia njozi njema jamaa huyo ambapo huyo dada ili kuwa specific amekuwa akitaja majina matatu, chuo anachosoma, na wakati mwingine koz anayosoma. Tena anaenda mbali zaidi na kutaja eneo jamaa anakoishi (namnukuu, ..."namtakia likizo njema na njozi njema huko .... aliko mapumzikoni nyumbani kwa sasa) wakati wa likizo.

  jamaa alishamwelewesha mkewe kuwa hajui kinachoendelea, lakini siku zinavyozidi kwenda, mgogoro unazidi kuongezeka, maana almost kila siku huyo dada lazime apige simu kwenye hata zaidi ya kituo kimoja cha redio, vipindi vya usiku.

  Imekuwa kero kwani sasa inajulikana kwa ndugu, jamaa na rafiki wa pande zote, ambao wamekuwa wakisikia salamu hizo au kuahdithiana. Jamaa kwa sasa anafanya taratibu za kupata namba za huyo dada kwenye vituo vya redio kadhaa, japo namba aliyopewa na kituo kimoja ilikuwa haipatikani kila alipopiga na amepeleka malalamiko tume ya mawasiliano, japo hajapata majibu...

  Kuna haja ya vituo vya redio na TV kuwa makini na haya mambo maana wasio na nia njema wanaweza kutumia hzi fursa vibaya...
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ah na huyo mkwewe nae awe muelewa mume yuko nae yeye huyo anaetuma salama atajijuuuuuuu atume mpaka akichoka atatulia.wanampa kichwa wakigombana..
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mkewe alijitahidi sana kumuelewa mwanzoni. Hata hivyo wakati ambapo mumewe amerudi chuoni, na kutokana na kuendelea kwa tabia hiyo ilianza kumfanya apoteze ujasiri. Pia ilichangiwa na kuulizwa mara kwa mara na ndugu na wazazi wake kuwa mbona mumewe anasalimiwa na mpenzi mwingine mara kwa mara, kuna tatizo katika ndoa yao?
   
 4. v

  valid statement JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Dah....hii kaliii.
   
 5. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Hivi, vituo vya redio vinaruhusiwa kutoa namba ya mtu bila ridhaa ya mhusika mwenyewe?? Na wanatumia vigezo gani kujiaminisha/kumuamini mlalamikaji kiasi cha kumgea namba ya mlalamikiwa bila consent yake?? Au aliwakubalia?
   
 6. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Jamaa asizuge, akumbuke visichana alivyovizuga hapo chuoni au huko alikopita!!
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii kesi ngumu..
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo sio kweli kwamba huyo kaka ni mpenzi wa huyo dada???
  Sitaki kuamini kwamba mtu anaweza akakurupuka tu na kumtumia mwanaume salamu za kimapenzi redioni bila kuwa na ukaribu wa aina yoyote. Na hizo details za huyo jamaa zote kazipata wapi nazo???

  Neway kwa vyovyote vile sikubaliani na kichwa chako cha habari...WATU NDIO WANAOWEZA KUVUNJA NDOA....tulieni na familia zenu huko!!
   
 9. ram

  ram JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,224
  Likes Received: 918
  Trophy Points: 280
  Lizy, yawezekana kbs sio wapenzi, mimi nadhan mdada amempenda huyo mkaka nadhan kaona njia rahis ya kufikisha ujumbe ni hiyo na pengine hajui kama ameoa na salamu zake zinasababisha timbwilwi. Km ni kweli basi mama awe muelewa tu manake hata kutrace no ya cm ya huyo dada ni ngumu coz anapiga redioni.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kama ni wapenda taarabu hiyo ndo zao..
  wanaita' kumrusha roho' huyo mwanamke.......
   
 11. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Sijaamini bado, kama angekuwa anamtaka basi asingeficha jina, angejitaja ili tongozo lake lifike directly na mhusika amjue anayemuadmire ni nani!!! Mfano wewe umempenda huyo jirani yako alafu uanze kumtongozea redioni bila kutaja jina, atajua kama ni wewe ram jirani yake?? As to that dude, anakijua kabisa hicho kidate chake na kama anao wengi ndo atahaha kumtambua ni yupi!!
   
Loading...