Vipimo vya mjao

Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,606
1,500
 1. Vipimo vya kimila
  Kabla ya kuundwa kwa vipimo sanifu vya kimataifa (SI) kulikuwa na vipimo mbalimbali vya mjao vilivyo tofauti kati ya nchi na nchi.

  Vipimo vya Kiingereza
  Hadi leo vipimo vya kiutamaduni vya Uingereza bado vinatumiwa katika nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza kama Marekani, Ufalme wa Maungano au Australia na hapo na pale kati ya watu wa nchi zilizokuwa koloni ya Uingereza.Kati ya vipimo hivi vya mjao ni fluid ounce, pint, quart, peck na bushel.

  Vipimo vya Uswahilini
  Waswahili wa kale kabla ya enzi ya ukoloni walikuwa na mfumo wa vipimo vyao, pia kwa mjao.

  Katika biashara walipima hasa mjao wa nafaka. Kipimo cha kimsingi kilikuwa pishi, Pishi 1 iligawiwa kwa visaga 2 au vibaba 4.

  Pishi 12 zilikuwa fara 1. Fara 5 au pishi 60 ziliitwa jizla 1, iliyoitwa pia mzo.[1]

  Pishi ililingana takriban na lita 2.5 - 3 lakini jinsi ilivyo katika mazingira ya kimila vipimo vilitofautiana kati ya mji na mji au soko na soko.[2]

  Marejeo
 2. Sehemu hii kuhusu vipimo vya Waswahili inafuata maelezo katika kamusi ya Velten, Suaheli Wörterbuch Teil I, Suaheli - Deutsch, Berlin 1910, uk 358 ("pima")
  Kamusi ya Kiswahili Sanifu inataja kibaba kuwa "kipimo cha ujazo cha takriban gramu 700", kwa hiyo pishi 1 = vibaba 4 = gramu 2800. Haisemi ni gramu za nini; mahindi huwa na gramu 800 kwa lita moja, unga huwa na gramu ~500 kwa lita. Sacleux katika kamusi yake (dictionnaire Swahili Francais, 1939) anataja pishi kuwa sawa na nusu galoni ya Kiingereza yaani takriban lita 2.25. Velten katika kamusi yake (Suaheli Wörterbuch I. Teil, 1910; "pima") anataja pishi kuwa na takriban lita 4 akirejea kibaba kuwa kama lita 1; hapa ni juu mno kwa sababu kibaba kipo chini ya lita 1
chanzo: Wikipedia ya Kiswahili, Kipimo cha mjao - Wikipedia, kamusi elezo huru
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom