vipigo CCM! Jamani vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

vipigo CCM! Jamani vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msongoru, Sep 16, 2008.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sophia Simba, Janeth Kahama washambuliana kwa maneno

  2008-09-15 09:26:48
  Na Simon Mhina


  Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam kilichokutana wiki iliyopita, kiliahirishwa kwa muda baada ya kutokea mzozo kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi (UWT) jijini, Janeth Kahama.

  Janeth na Sophia wote wanawania nafasi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikishikiliwa na Anna Abdallah.

  Chanzo chetu ndani ya kikao hicho kimepasha kuwa kilichoibua mzozo huo ni malalamiko yaliyotolewa na Waziri Simba kwamba siku hizi hashirikishwi katika vikao vya UWT Mkoa wa Dar es Salaam, na malalamiko hayo kumgusa Kahama ambaye ndiye mwenyekiti.

  Chanzo chetu kimepasha kuwa Waziri Simba alitoa malalamiko hayo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita.

  Habari hizo zinasema baada ya Simba kuwasilisha malalamiko yake, Kahama alisimama kujitetea na kusema kuwa, Waziri huyo hapaswi kumlaumu mtu, kwa vile anajifanya ana shughuli nyingi kila wakati anapopelekewa taarifa za mwaliko wa vikao.

  Kutokana na majibu hayo, chanzo chetu kimetupasha kuwa Waziri Simba alikuja juu huku akimshambulia Kahama kwa maneno, kwamba ana wivu, yaani anamuonea wivu kutokana na nafasi yake.

  Habari hizo zinasema Kahama naye aliamua kujibu mapigo, huku akimrushia makombora mshindani wake kwamba Waziri huyo anatumia madaraka yake katika kampeni za kutaka achaguliwe uenyekiti wa Taifa wa UWT.

  ``Usifikiri uwaziri wako na kupata ofisi pale Ikulu vitakusaidia, huu ni uchaguzi wa Chama, heshimu taratibu za chama,`` chanzo chetu kilimnukuu Kahama.

  Habari zinasema kuwa Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu, alisimama na kumuomba Guninita asitishe hoja hiyo, kwa vile haiwahusu.

  Imeelezwa kuwa, baada ya Zungu kutoa hoja hiyo, Waziri Simba alimfuata huku akiwa ameweka vidole juu na kuanza kumsuta Mbunge huyo na kumfokea kwamba anajifanya ni mjanja wa CCM jijini Dar es Salaam.

  Habari hizo zinasema kuwa Zungu alipoona Simba amefuatwa kwenye kiti chake na kusimama mbele yake, aliamua kutoka haraka haraka na kuacha kikao.

  Habari hizo zinaendelea kueleza kuwa baada ya Zungu kuondoka katika kikao, Waziri Simba alielekea alipokuwa ameketi Kahama lakini wajumbe waliwatenganisha ili kuepusha mzozo zaidi.

  Akihojiwa na Nipashe jana, Guninita alikiri kupokea malalamiko toka kwa Waziri Simba kwamba hashirikishwi kwenye mambo ya UWT, jambo ambalo alisema analitafsiri kwamba ni njama za kumwangusha katika kinyang`anyiro hicho.

  Hata hivyo, alisema hicho kinachoitwa ugomvi siyo kilichosababisha kufungwa kwa mkutano.

  ``Unajua Waziri Simba alitoa malalamiko yake kwangu wakati mkutano wetu tayari ukiwa umemalizika, hapakuwa na ugomvi mkubwa kama unavyouliza, bali Mwenyekiti wa UWT Mkoa (Kahama) alikuwa akijaribu kutoa ufafanuzi,`` alisema Guninita.

  Alipoulizwa na Nipashe kuhusu kutoka katika kikao, Zungu alisema hakukimbia, bali muda wake wa kuondoka ulishafika.

  ``Mengine yaliyotokea huko nyuma sijui, lakini mimi nilishaondoka,`` alisema Zungu.

  Akihojiwa na Nipashe kuhusu kutembeza ubabe kikaoni, awali Waziri Sophia alikana kwamba hajawahi kuhudhuria kikao hicho.

  Hata hivyo, alipopigiwa simu mara ya pili, muda mfupi baada ya Guninita kukiri kupokea malalamiko kutoka kwake kikaoni, Simba alikiri kuwepo, lakini akahoji nani aliyevujisha habari za tukio hilo.

  ``Wewe sijui leo ni mtu wa ngapi kunipigia simu, watu wengi wamenipigia eti wanauliza kulikuwa na masumbwi kati yangu na Janeth. Sasa kwa nini mnaniuliza, huyo aliyeamua kuvujisha siri za kikao basi na awamalizie kilichoendelea,`` alisema.

  Kahama alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai ya vurumai hizo, alikata simu na hadi tunakwenda mitamboni jana, simu yake ya kiganjani ilikuwa imefungwa.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hatari hii jamani!! Kweli UFISADI mtamu...
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu mama kweli mambo mengi sana!Sophia Simba anajua kuna ulaji lazima agombee kwa vurugu!
  Politics Is A Dirty Game!
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sophia Simba ubabe utakufikisha pabaya, Uza sera mama siyo kugeuza kikao uwanja wa masumbwi! hao nipashe naona wamekustahi, ukweli ni kwamba makonde alirusha na wanaume walipo jaribu mzuia aliwasukumizia kuleee.....

  Ninalo shangaa jamani hivi ni ruksa waziri mwenye dahamana kurusha makonde mbele ya kadamnasi? hakuna 'ethics' hapo zilizo vunjwa?
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  Hii nayo kali ama kweli madaraka ni matamu!mtu waziri bado unataka tena uenyekiti!si ungeridhika tu na nafasi ya uaziri ili ufanye kazi zako kwa ufanisi!sasa UWT nako anataka!
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hizo ni tabia za kifisadi,hakuna lolote.
   
 7. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ndio hapo mtajua sophia SIMBA ni nani. she is very powerful woman in the system nawaaambieni
   
 8. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sophia Simba, Janeth Kahama washambuliana kwa maneno

  2008-09-15 09:26:48

  Na Simon Mhina
  • SOURCE: NIPASHE
   
 9. C

  Chief JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Labda hela za Zain wanaojenga ofisi kuu zao kwenye kiwanja cha UWT
   
 10. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nanukuu manenokatika gazeti liliandikuwa Bibie bi Sophia Simba alisema kwuwa ameambiwa na Rais kikwete agombanie hiyo nafasi ,hiyo ndiokauli yake sasa hapatujiulize nini kinaendelea na kuwachieni wachambuzi kwamuda huu mtafakari kauli yake bi simba .
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Hii mijitu sijui kama inajua kusoma nyakati.  .
   
 12. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapo ndiyo muone wenyewe hawa mawaziri wa JK! Amewachagua kwa kuzingatia nini!!!!
   
 13. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Bwana Black Jesus itakuwa msaada mkubwa kama ukiweka link ya hilo gazeti
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli, wanarudisha nyuma mapambano ya kujikomboa kwa mwanamke!
   
 15. M

  Masatu JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wanagombea mabwana tu hakuna lolote
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Akina mama mnatuangusha kwa kweli,mambo ya kususa susa tuu kila wakati hata hamkui.
   
 17. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wasiwasi wangu haya malengo ya milenia ya kuongeza idadi ya akina mama katika uongozi yakitia hali itakuwaje.
  Sijui....
   
 18. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  una ushahidi?au udaku tu
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kumbe hawakushambuliana na wka maneno tu. kwa mujibu wa magazeti ya leo, Kahama anasema kuwa alikabwa na kupigwa ngumi na Simba. Anasema hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba alikumbuka msalaba! Anasema hata wanaume wenye nguvu walijaribu kumshika Simba lakini walsihindwa kwa jinsi alivyogeuka mbogo
   
 20. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280


  Majina ya magazeti hayo!naomba jina la gazeti
   
Loading...