Vipi Yanga leo Taifa?

Vipi Yanga leo Taifa?

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Leo yanga anashuka dimbani katika kuendelea kuikamilisha raundi ya kwanza ya Ligi Tanzania Bara.

Jana watani wao wameshindwa kuvumilia matokeo wakaamua kumalizia hasira zao kwenye mali ya umma.sasa je Yanga na nyinyi yakiwakuta leo ya kufungwa au kutoa droo mtakua kama wale wanywa viroba wa Msimbazi?
Je kuna nafasi za kutosha kweli leo uwanjani maana simba walitoroka zoo wakaja kungoa viti wakidai eti wanahasira.

Yote ya yote nawaombea mfungwe ili ile timu yetu ya wananchi Mbeya city izidi kuwapoteza.

VIVA MBEYA CITY FC
KUTOKA LIGI DARAJA LA KWANZA MPAKA UBINGWA LIGI KUU
 
Young Africans leo itashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kucheza na maafande wa jeshi la kujenga Taifa nchini timu ya JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom mzunguko wa 12.
Mara baada ya ushindi wa pili mfululizo wa mabao 3-0 dhidi ya Rhino Rangers na Mgambo Shooting kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kimeendelea kuimarika na safu ya ulinzi ikicheza michezo miwili pasipo kuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Mpaka sasa Young Africans inashika nafasi ya tatu ikiwa na ponti 22 pointi 1 nyuma ya timu zinaongoza mbili za Azam FC na Mbeya City zote zikiwa na pointi 23 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Young Africans inahitaji pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa leo dhidi ya JKT Ruvu ili iweze kujikita kileleni na kukalia kiti cha uongozi wa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 25 ambazo zitaweza kufikiwa na timu mbili tu za Azam FC na Mbeya City ambazo zitachezwa mwishoni mwa wiki.
Timu iliingia kambini juzi jioni katika hostel zilizopo makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa vijana wa Jagwani kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi na kupata pointi tatu muhimu.
Katika mchezo wa leo Young Africans itakosa huduma ya wachezaji wake David Luhende na Nizar Khalfani ambao ni majeruhi huku kiungo Haruna Niyonzima akiukosa mchezo huo kutokana na kuwa nchini Rwanda alipokwenda kushugulikia matatizo ya kifamilia.
Wapenzi, washabiki na wanchama wa Young Africans leo wanaombwa kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia vijana katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu. (Source: YANGA KUIVAA JKT RUVU TAIFA)
 
km wewe mbeya city habari ya yanga ya nini?
 
azam fc leo chanel ten na tbc 2 dont miss it dudez..
 
i hate yanga kutoka moyoni
 
Mwee nakosa maamuzi!
Yanga timu yangu na mbeya mkoa wangu!
Sijui nifanye kama mwigamba? Niisaliti tu yanga
 
Yanga na simba zinarudisha maendeleo ya soka kwa kiwango kikubwa sana bongo!
 
Kwani umekatazwa kuizungumzia Mbeya city?
 
Back
Top Bottom