ASFC DRAW: Simba, Yanga, Azam zapangwa na Vibonde

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Droo ya mashindano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) imepangwa leo Novemba 29, 2023 ambapo Vigogo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Yanga na Azam wamepewa vibonde katika hatua ya kusaka tiketi ya 32 bora.

Katika droo hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64, Mabingwa watetezi Yanga SC wamepangwa dhidi ya Haulung ya daraja la kwanza wakati Simba wakiwakaribisha Tembo FC ambao ni Mabingwa wa Ligi ya Mkoa wa Tabora huku Azam wakiwa wenyeji wa Alliance kutoka Mwanza.

DROO KAMILI YA RAUNDI YA PILI (Mechi zitaanza kuchezwa kati ya Desemba 15 na 17)

Yanga SC vs Haulung FC
Simba SC vs Tembo FC
Azam FC vs Alliance FC
Singida Foutain Gate vs Arusha City,
KMC vs ACA Eagle,
Dodoma Jiji vs Magereza FC,
JKT Tanzania vs Kurugenzi FC,
Kagera Sugar vs Dar City,
Geita Gold vs Singida Cluster,
Namungo vs Hollywood FC,
Tabora United vs Monduli Coffe (Arusha),
Coastal Union vs Greenland FC,
Ihefu FC vs Rospa FC,
Tanzania Prisons vs TRA Kilimanjaro,
Mtibwa Sugar vs Nyakagwe,
Mashujaa FC vs Mbuga FC
 
Yes, myama Tembo ni kibonde mbele ya mnyama Simba. Huko mbugani tembo huliwa na simba hususan watoto wa tembo wanaonewa. Sidhani kama simba wana ubavu wa kumvaa tembo aliyekomaa. Nahisi simba wetu wamepangwa na watoto wa tembo.
 
Tembo hafui dafu kwa Simba, hata Simba akiwa simba shoga.
Simba watampiga mtu goli 6
 
Back
Top Bottom