Vipi vilikua kipaumbele chako wakati unachagua mchumba/mke?

Optimists

JF-Expert Member
Oct 17, 2021
278
686
Vipi je priority yako Ilikua ni elimu, matako makubwa, uzuri wa sura, financial status, mweusi, mnene mrefu? au ulijishtukia tu umeoa?

Nimepata mchumba, Bado nafiikiria kama nitamuoa, japo asilimia zimefika kama 67% nasubiri zifike 85% nimuweke ndani, Tabia kwa miezi 3 hii anaridisha, mcha Mungu sana, Binti hajawai kuguswa kabisaa Lakini sura ni wakawaida tu, siyo wale akipita mbele yako lazima ugeuke hapana, age miaka 23 ninavyomuona hata nikimuoa sitapata competition saana kutoka kwa wazambuli/ mende, Hana makuu nilimwambia nimenunua shamba hekali moja twede tukalime akaniambia sawa aina shida, ni Binti wa kasulu vijijini huko, kwao wako 11 yeye ni wa Mwisho, madada 6 wameshaolewa woote, Binti hajui burger Wala Pizza, japo amekaa dar miaka 4, hapajui kitambaa cheupe, Lambo Wala tiptop. Yupo tayari kuishi sehemu yoyote Tanzania, namuona kama ni mke niliekua namsubiri aisee ni wakati wa kuoa Sasa.

Vipi kipindi unaoa ulizingatia nini? Au unapotaka kuoa umeweka vigezo gani? Je tatizo la ndoa kuvurugika inategemeana na vijana kuweka masharti wakati wa kuoa/ kuolewa? Nina jamaa yangu yeye standard alizoziweka yeye ni uzuri, alitaka mabinti wale wa show off, Sasa hivi analia tu, amekosa amani Kabisa, kuanzia wafanyakazi wenzie mpaka maboss wanamtaka mke wake alafu jamaa life yake ni kama ya kuunga tu, Hana amani.
 
Hayanaga mwongozo mkuu. Ukishapenda sawasawa hata ulikuwa na vigezo vyako unaviona siyo vya muhimu kivile...ukija kushtuka muda wa kampeni umeshaisha jimbo limeshachukuliwa na mgombea keshaapishwa upo unaonja joto ya jiwe...

Kwangu mimi kigezo kikubwa kilikuwa ni akili na emotional intelligence. Binti aliye vizuri upstairs na ambaye ana emotional intelligence kubwa kama Mama E basi mi kwishnei. Mengine tutajuana huko mbele ya safari 😁
 
Screenshot_20240322_212547_WhatsApp.jpg

Am done
 
Hayanaga mwongozo mkuu. Ukishapenda sawasawa hata ulikuwa na vigezo vyako unaviona siyo vya muhimu kivile...ukija kushtuka muda wa kampeni umeshaisha jimbo limeshachululiwa na mgombea keshaapishwa upo unaonja joto ya jiwe...

Kwangu mimi kigezo kikubwa kilikuwa ni akili na emotional intelligence. Binti aliye vizuri upstairs na ambaye ana emotional intelligence kubwa kama Mama E basi mi kwishnei haijalishi kama ni kama ni pisi kali ama la!
Kweli sana comments Bora kwangu kwa siku ya Leo, barikiwa sura sio kigezo kwako?
 
Back
Top Bottom