Vipi NMB, mbona App yenu inazingua?

Vipi NMB, mbona App yenu inazingua?

ministrant

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
1,257
Reaction score
2,307
Tokea siku ya juzi kuna changamoto kwenye app yenu ya NMB mkononi, kutoa pesa ni shida na nimekuta nimeandikiwa deni ndani ya account yangu yaani (-Kisha kiasi ninachodaiwa) jambo ambalo sijawahi kuliona hapo kabla.

Nimetuma pesa juzi na imerudishwa jana ila nikitaka kununua umeme pia haiwezekani. Kuweni makini na mifumo yenu na kama mmezidiwa ni busara kuomba msaada
 
Nmb wamenikosesha dili baada ya kutuma fedha kupitia app na haikumfikia mlengwa
 
Walisababisha nikashindwa kutoa pesa ya kunywa bia. Jana nimelala nipo soba kabisa wapuuzi sana hawa...🤨
downloadfile-1.png
 
Tokea siku ya juzi kuna changamoto kwenye app yenu ya NMB mkononi, kutoa pesa ni shida na nimekuta nimeandikiwa deni ndani ya account yangu yaani (-Kisha kiasi ninachodaiwa) jambo ambalo sijawahi kuliona hapo kabla.

Nimetuma pesa juzi na imerudishwa jana ila nikitaka kununua umeme pia haiwezekani. Kuweni makini na mifumo yenu na kama mmezidiwa ni busara kuomba msaada
Kwenye UMEME tokeni haiji kwa sms ila ukienda sehemu ya pata tokeni kwenye menu ya Luku ndo unaona tokeni kwa hiyo inabdi uweke umeme umeshikilia sehemu ya tokeni.

Mimi nimelipa king'amuzi mara mbili moja imekubali moja imegoma ila fedha imekatwa naomba bank statement sipati siku ya tatu leo.
 
Yaani imekuwa shida kweli! Nilifanya malipo siku 3 ziluzopita, pesa haikufika, kwangu inaonesha imetoka ila ipo kwenye process.
 
Back
Top Bottom