Vipi Mishahara kwa watumishi wa umma?

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Aslam alekhum wanajamvi.

Hivi karibuni kumezuka tetesi nyingi sana kuhusiana na serikali yetu kuchelewesha Mishahara.

Ningependa kujua ukweli wa hili jambo kupitia watumishi wa UMMA mliopo humu.

Nafikiri Tar 25 ya mwisho wa Mwezi mishahara inatakiwa iwe kwenye account za wahusika.
 
mshahara kwa baathi imetoka ila ikiwa pungufu, my friend anafanya halmashauri kapata with less by 110,000/=
 
Inasemekana hadi sasa wafanyakazi wa umma hawajapata mishahara yao wanalia. Sisi tulio katika private sekta tunashajizoelea tunasubiri tarehe 30 tuchekelee ila tetesi ni kuwa serikali iko hoi bin taaban.
 
Habari ni kwamba hazina imelipa mishahara jana 28/11. Leo ndio itaingia kwenye akaunti. At least kwa hapa nilipo.
 
Wana JF, sie wazee wa fuko la babu wategemea baba Ridhi mishahara imetoka, sasa tuache kazi maofisini tukimbilie POMBE, SIGARA na POOL maana ndio kazi tunazoziweza hizo. Angalieni salio!!!

Nawasilisha
 
Kaka kheri yenu, huku chuo kikuu cha kata cha morogoro hatujapata kitu, tunaambiwa eti mchakato unaendelea, sijui wanataka nasi tukawakamue wanavyuo rushwa ndo mambo yaende, maana wenzetu maaskari, madaktari na mahakimu wanawakamua wateja wao lakini bado kimango kimetoka mapemaaa, mi nashindwa kuelewa je serikali inatudharau sisi au viongozi wetu ni wazembe, ngoja tukae kama kamati.
 
Mpaka hapa umeshaisha woote, hamna kitu,ni hela ya kula tu hiyo.ni kugawana mshahara na serikali,nusu kodi(direct&indirect tax) nusu ndo inaingia tumboni.
 
Wana JF, sie wazee wa fuko la babu wategemea baba Ridhi mishahara imetoka, sasa tuache kazi maofisini tukimbilie POMBE, SIGARA na POOL maana ndio kazi tunazoziweza hizo. Angalieni salio!!!

Nawasilisha

kuna maza fulani nilimuona anatoka kwenye ATM ya NMB amenuna. natamani ningekuwa na namba yake nimjuze.
 
ni kwamba hizo pungufu ni serikali yenyewe imepiga panga au inakuwaje? au ni wizi?

Il Gambino.

Haya si kweli kabisa, serikali imelipa wafanyakazi wake kama kawaida ila kulikuwa na matatizo ya kiufundi kwenye computer za hazina.
 
Habari ni kwamba hazina imelipa mishahara jana 28/11. Leo ndio itaingia kwenye akaunti. At least kwa hapa nilipo.
Nadhani aliyekupa hii habari hajakuelewesha vizuri, hazina walilipa mishahara kabla hata ya tarehe25 tatizo inasemekana kuna mvutano na BOT wao Hazina wanalipa bila kujua kama wana pesa za kutosha BOT, Kwa taarifa yako inasemekana Serikali ina nakisi ya zaidi ya Billion400 pale BOT(-400Bn) na inasemekana kuna makubaliano ya BOT na Serikali kwamba nakisi haitakiwi izidi Billion600, na BOT wakiruhusu tu kutoa mishahara kama walivyo agizwa na Hazina nakisi itakuwa zaidi ya Billion700 kitu ambacho mpaka wafadhili wanaweza kuingilia kati. Kama unabisha subiri serikali ilipe mishahara alafu watafute watu wenye data za Ballance ya serikali watakuambia. Watu hawaelewi ni kwanini mfumuko wa bei unapanda kila kukicha ishu ni kwamba inadaiwa serikali imeshaanza kamchezo ka kuprint noti.

Tafakari na uchukue hatua
 
Haya si kweli kabisa, serikali imelipa wafanyakazi wake kama kawaida ila kulikuwa na matatizo ya kiufundi kwenye computer za hazina.

Mkuu kwa hiyo mishahara ya wafanya kazi wengine itakuwa imeliwa na virus eti?
 
kwani kipindi cha mr. clean, mzee ruhsa na mchonga watu walikuwa wanapata mshahara tarehe ngapi vile?
 
Inasemekana hadi sasa wafanyakazi wa umma hawajapata mishahara yao wanalia. Sisi tulio katika private sekta tunashajizoelea tunasubiri tarehe 30 tuchekelee ila tetesi ni kuwa serikali iko hoi bin taaban.
Eti na wewe ni great thinker!
 
Nadhani aliyekupa hii habari hajakuelewesha vizuri, hazina walilipa mishahara kabla hata ya tarehe25 tatizo inasemekana kuna mvutano na BOT wao Hazina wanalipa bila kujua kama wana pesa za kutosha BOT, Kwa taarifa yako inasemekana Serikali ina nakisi ya zaidi ya Billion400 pale BOT(-400Bn) na inasemekana kuna makubaliano ya BOT na Serikali kwamba nakisi haitakiwi izidi Billion600, na BOT wakiruhusu tu kutoa mishahara kama walivyo agizwa na Hazina nakisi itakuwa zaidi ya Billion700 kitu ambacho mpaka wafadhili wanaweza kuingilia kati. Kama unabisha subiri serikali ilipe mishahara alafu watafute watu wenye data za Ballance ya serikali watakuambia. Watu hawaelewi ni kwanini mfumuko wa bei unapanda kila kukicha ishu ni kwamba inadaiwa serikali imeshaanza kamchezo ka kuprint noti.

Tafakari na uchukue hatua

Ohoo wanaprint vipi noti,au unamaanisha hela fake?na wanazisambazaje? sijakuelewa kidogo hapo mkuu,unaweza kufafanua kidogo?
 
Back
Top Bottom