vipi kuhusu hili

wakuu naombeni mnijuze tofauti kati ya haya maneno, hayati na marehemu.

HAYATI, ni mtu alokufa lakini ambae akitajwa hutajwa kwa wema na anaekumbukwa kwa wema, wake na mara nyingi watu hawa wanaoitwa hayati uhai wao walikua na umaarufu fulani.

MAREHEMU, ni mtu yeyote alokwishakufa siku nyingi zilizopita.
 
shukrani mkuu kwa kudadavua
 
wakuu naombeni mnijuze tofauti kati ya haya maneno, hayati na marehemu.

Hayati-hutumika kumtaja mtu aliyefariki kwa kukumbuka mambo mema/mazuri aliyofanya. Mathalan Hayati Julius Nyerere, hayati Abeid Karume etc.
Marehemu-hutumika kumuombea mtu yeyote aliyefariki dunia, siku nyingi au hata siku chache zilizopita. Marehemu-kutokana na neno rehemu. Yaani unaomba arehemiwe.

Mtu yeyote anaweza kuwa hayati, na kamwe hayati sio cheo kama wajinga wanavyozusha.
Kwa hiyo hata ukisema hayati marehemu Julius Nyerere bado uko sahihi.
 
Hayati ni neno la Kiarabu, likiwa na maana aliye hai....!

Waswahili tunalitumia kwa namna mbili, kwa wale wasio hai, likitamkwa kabla ya jina lina maanisha huyo mtu hana uhai.

Mfano kuna huu msemo wa Kiswahili: Si hayati si mamati, (si mzima si mgonjwa)

Neno Marehemu, linatokana na neno Rehma, likimaanisha Huyo mfu amerehemewa.
 
Hayati ni neno la Kiarabu, likiwa na maana aliye hai....!

Waswahili tunalitumia kwa namna mbili, kwa wale wasio hai, likitamkwa kabla ya jina lina maanisha huyo mtu hana uhai.

Mfano kuna huu msemo wa Kiswahili: Si hayati si mamati, (si mzima si mgonjwa)

Neno Marehemu ni neno la kiarabu likitamkwa marhum kwa maana mrehemewa, linatokana na neno Rehma, likimaanisha Huyo mfu amerehemewa.

Swadakta
Swadakta.
 
Back
Top Bottom