Vipi awe ni wa kwako?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Angali yuko mtini,
Vipi huyo awe wako?
Waninunia mtani.

Nakuuliza kwanini,
Huyo ndege awe wako,
Alama yako nini?

Vipi nisimtamani,
Asiye mkononi mwako?
Wakati yuko mtini.

Ulimtia machoni,
Mara kawa ni wa kwako,
Kwa ubavu gani?

Watuzuia kwa nini,
Wengine na wangaliko,
Sikubali asilani!

Manati i mkononi,
Nikitungua si wako,
Ugomvi wa nini!?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
ujumbe umemfikia...
ha ha haha..
wapo watu wakiona ndege tu basi wa kwao...
 
1. naona wavuka mmpaka, yangu kuyajongea,
kama angekuwa paka, mie nisingeongea,
sasa naona shaka, kwa ndege kuingilia,
lazima awe wangu, wewe huwezi fikia

2.
nasema ndiye wangu, wako bado kutokea,
taswiraye kama yangu, hayo si ya kusemea,
hata kama ni yawa chungu, kweli utaipokea,
lazima awe wangu, wewe huwezi fikia.

3.
manatiyo maridadi, kuachia wachelea,
kama wangoja miadi, mie ndo ninajisevia,
utafyonza bila idadi, kwa ndege yule kumlilia
lazima awe wangu, wewe huwezi fikia

j4.
ifunze kwao wajuzi, waliofuzu kuwinda,
hata ikiwa chamazi, bora usile makinda,
bila kujali miezi, bali wanachokufunda
lazima awe wangu, wewe huwezi fikia
 
Nyie niachieni.
1.Nyie mwacheni wangu kimwana
Namjua mie marefu kwa mapana.
Kuwepo kwangu ni dhamana
Mwacheni wangu mie kanizowea.

2. Uroho tu huo wakusumbueni.
Mwajua nimemtoa msambweni
Au sababu mushajua mijini.
Mwacheni wangu vipi kumtamani.

3. nawe bana dogo hutosheki
Kila ukionacho wadhani keki
Nasema sasa huyu hatafuniki
Mtachoka tu kwa kunicheki.

4. kumbe ndo janja yenu
Heshima jamani huyu si wakwenu
Mnikubali tu mie shemeji yenu.
Hazitaki faranga wala vibisa wenu

5. Munisome tu kama gazeti
Si muda tawapa cheti
Niwapo nae nyie muvutane mashati.
Hauziki na wala hamumupati
 
wakijiji sikate tama, kama bado yu mtini,
nenda naye kwa mama, na umuweke zizini,
mgombea talalama, mwishowe ataamini,
ndege akiwa mtini, si wako usijisifu!

ndege akiwa mtini, nani adai wa kwake,
akivutia moyoni, tungua miguu yake,
muache swahiliani, wamjua kwani mke,
ndege akiwa mtini, si wako usijisifu!

mgombea na mipaka, lini uliiweka,
usitake shida kaka, ndege simfanye paka,
mchukue ka wataka, ila najua hakika,
ndege akiwa mtini, si wako usijisifu!

Wakijiji nakuonya, ndege pia namtaka,
we endelea nyonya, utakuta nimepika,
na hakika utafonya, utanichukia kaka,
ndege akiwa mtini, si wako usijisifu!
 
1.
Wa kijiji kaufyata, kweli kusikilizia,
Kaona ni heri bata, kuliko wa kuwindia,
Bora acheze karata, siyo hivi kuamia
lazima awe wangu, wewe huwezi fikia

2.
Sijasikia mswazi, katika ulotaka
Japo sasa u muwazi, vya wenzio kuvitaka,
Mwisho utatoa vazi, haibayo iwe taka
lazima awe wangu, wewe huwezi fikia

3.
Sijakusikia ebi, kwa hayo ulonena,
Maoni kama ya bibi, ya sasa nayo wakana,
Nakuapia yarabi, yu wangu hatanikana
lazima awe wangu, wewe huwezi fikia

4.
mwisho nawapeni somo, mlioshika manati,
wekeni sasa ukomo, kwani hamna bahati,
ndege kwenu hayumo, yu kwangu anachati
lazima awe wangu, nyie hamwezi fikia
 
Mgombea mgombea, jinalo lajieleza,
kamwe hutaki sikia, unabishana na giza,
ndege juu ametulia, we wataka mkimbiza,
kama ndege ni wakwako, mbona bado yu mtini!??

Utaziba masikio, somo langu husikii,
tavunja hata vioo, pumzi sikupatii,
ndege tamkaba koo, mawe simzuilii,
kama ndege ni wakwako, mbona bado yu mtini!??

utapiga tararira, ndege hunaye chatini,
utajikunjia sura, ndege bado yu mtini,
mpaka niipate dira, manati sishushi chini,
kama ndege ni wakwako, mbona bado yu mtini!??

labda kwa kumalizia, sote tukae kimya,
ndege tutamnyatia, tudake wake mkia,
yule atamchukua, ndege ni wake hakika,
kama ndege ni wakwako, mbona bado yu mtini!??
 
1.
Kweli ndege ndiye wangu, japokuwa yu mtini,
Huwezi mjua wangu, japo ndiwe mfitini,
Heri ufate machangu, usijekuwa haini,
Hakika ndege yu wangu, tayari nimesaini.

2.
Sasa iache kalamu, kwani wapoteza wino,
Mwenye ndege kulaumu, kweli huna maono,
Kama ingekuwa swaumu, njaa ngekupa kibano,
Hakika ndege yu wangu, tayari nimesaini.

3.
Madamu si ramadhani, sasa wadhani utani,
Na ukujie mtihani, ukweli utabaini,
Ndege sasa kibindoni, mgombea tamwamini
Hakika ndege yu wangu, tayari nimesaini.

4.
Angalia sijekuwa, ndani ya kumi na nane,
Waweza kuwa jibuwa, uje tamani mwingine,
Siku zitakutibua, slimu uione nene,
Hakika ndege yu wangu, tayari nimesaini.
 
Hongereni wakuu,

Hii kwa mtazamo wangu ingekua hadithi ya kisiasa ingependeza sana.

Mfano,(post ya kwanza) Mwanakijiji anataka uongozi lakini kutokea upinzani lakini tayari wenye madaraka yaani ccm wanadai wao kuongoza milele kama wafanyavyo sasa.Anawaambia uongozi ni wa yoyote tu mwenye ridhaa ya wananchi (wanawakirishwa na ndege kwenye shairi),sasa manza inaanzia hapo anadai nia na hari (manati) anayo ya kupata hicho anacho taka huyo ndege (uongozi).

Post ya pili,anapata na mashabiki pia kwamba watamwezesha na kwamba wenyewe (ccm) habari wamepata kwamba sasa kazi ipo.

Post ya tatu,Mwanakijiji anajitutumua na kuleta mbwembwe mbele ya wapambe kwamba anaweza.

Post ya nne,Duh!wenyewe wanamjibu mwanakijiji,kwamba asijisumbue uongozi ni wao siku nyingi na hilo halina shaka kwanza yeye Mwanakijiji uongozi (ndege) wala hafanani nao ila wao tu "wagombea".Tena wanamwambia ,kweli nia ya uongozi unayo ila wewe bado mwanafunzi nenda kajifunze tena kwao.

Salale,kumbe Mwanakijiji hayuko pekeyake anayetaka kua na huyo ndege,wako wengine,Bwn.Mswahili pia anasema wamwachie yeye kwani sio yeye mwanakijiji wala mgombea anayestahiri huyo ndege yeye pekee yake ndio mahususi.Anadai yeye sikunyingi ndege wake yeye ila wao tu wanamtolea macho,basi wamuaachie huo ungozi yeye kwani ndio anafaa,kwanza mfano yeye Mwkjj,kapelekwa shule na yeye Mswahili kwa kutumia ndege huyo huyo asione gele.

Inakua kama hari sio shwari kati ya Mgombea na Bwn. mswahili inavyoonekana wanatoka kwenye chama kimoja,ila sasa kuna mgongano wa kimaslai na mawazo pia wanagombana wenyewe kwa wenyewe.Ila inaonekana mgomea ananguvu kweli kweli chamani huko,anamwambia Bwn.mswahili asithubutu kutaka kisichokua chake na huyo Mwkjj bora yeye aendelee kuandika habari tu magazetini na kwenye wavuti.
Pia nawapuuza wote wale wanaoshangilia na kushabikia yasio wahusu,mfano Bwn Abi,mwawado na bwn bosi.

Bwn.Abi hakubari anadai yeye pia anaweza kumpata ndege na,yeye mgombea sio lolote ,basi kamavipi wakae wote wasubiri nani ndege (sasa hapa ndege ,watakua wananchi) atamchagua.

Lakini mwisho wa yote mgombea hakubarivijana wamshinde anawaambia,wanyamaze tu kwani wanapika makelele na kupoteza nguvu zao kwa jambo ambalo yeye anajua ni la kwake na wao ni wadokozi tu wanataka kuvamia mambo yasio wahusu.kwani wao bado vijana hawaju wakitakacho,kesho kesho kutwa wataacha uongozi kwenda fata jambo lingine vision ikapote.

Huo ni mtazamo wangu tu wa kifasihi kutokana na beti za wahusika,hazihusiani na chochote kama hicho kwenye maana harisi ya tungo za wenyewe hao .
Ni hadithi tu nimeipata hapo hapo
 
Hongereni wakuu,

..........................

Huo ni mtazamo wangu tu wa kifasihi kutokana na beti za wahusika,hazihusiani na chochote kama hicho kwenye maana harisi ya tungo za wenyewe hao .
Ni hadithi tu nimeipata hapo hapo

nashukuru mkuu kwa uchambuzi wako makini.

huo ndio utamu wa lugha! mtu anaona mashairi kumbe maudhui ya ndani usipime. tunashukuru umesaidia kufikisha ujumbe
 
Kaka umeiva..wacha nifike nyumbani kwanza nikutumie majibu! UMEIVA VIBAYA...
 
Hongereni wakuu,

Hii kwa mtazamo wangu ingekua hadithi ya kisiasa ingependeza sana.

Mfano,(post ya kwanza) Mwanakijiji anataka uongozi lakini kutokea upinzani lakini tayari wenye madaraka yaani ccm wanadai wao kuongoza milele kama wafanyavyo sasa.Anawaambia uongozi ni wa yoyote tu mwenye ridhaa ya wananchi (wanawakirishwa na ndege kwenye shairi),sasa manza inaanzia hapo anadai nia na hari (manati) anayo ya kupata hicho anacho taka huyo ndege (uongozi).

Post ya pili,anapata na mashabiki pia kwamba watamwezesha na kwamba wenyewe (ccm) habari wamepata kwamba sasa kazi ipo.

Post ya tatu,Mwanakijiji anajitutumua na kuleta mbwembwe mbele ya wapambe kwamba anaweza.

Post ya nne,Duh!wenyewe wanamjibu mwanakijiji,kwamba asijisumbue uongozi ni wao siku nyingi na hilo halina shaka kwanza yeye Mwanakijiji uongozi (ndege) wala hafanani nao ila wao tu "wagombea".Tena wanamwambia ,kweli nia ya uongozi unayo ila wewe bado mwanafunzi nenda kajifunze tena kwao.

Salale,kumbe Mwanakijiji hayuko pekeyake anayetaka kua na huyo ndege,wako wengine,Bwn.Mswahili pia anasema wamwachie yeye kwani sio yeye mwanakijiji wala mgombea anayestahiri huyo ndege yeye pekee yake ndio mahususi.Anadai yeye sikunyingi ndege wake yeye ila wao tu wanamtolea macho,basi wamuaachie huo ungozi yeye kwani ndio anafaa,kwanza mfano yeye Mwkjj,kapelekwa shule na yeye Mswahili kwa kutumia ndege huyo huyo asione gele.

Inakua kama hari sio shwari kati ya Mgombea na Bwn. mswahili inavyoonekana wanatoka kwenye chama kimoja,ila sasa kuna mgongano wa kimaslai na mawazo pia wanagombana wenyewe kwa wenyewe.Ila inaonekana mgomea ananguvu kweli kweli chamani huko,anamwambia Bwn.mswahili asithubutu kutaka kisichokua chake na huyo Mwkjj bora yeye aendelee kuandika habari tu magazetini na kwenye wavuti.
Pia nawapuuza wote wale wanaoshangilia na kushabikia yasio wahusu,mfano Bwn Abi,mwawado na bwn bosi.

Bwn.Abi hakubari anadai yeye pia anaweza kumpata ndege na,yeye mgombea sio lolote ,basi kamavipi wakae wote wasubiri nani ndege (sasa hapa ndege ,watakua wananchi) atamchagua.

Lakini mwisho wa yote mgombea hakubarivijana wamshinde anawaambia,wanyamaze tu kwani wanapika makelele na kupoteza nguvu zao kwa jambo ambalo yeye anajua ni la kwake na wao ni wadokozi tu wanataka kuvamia mambo yasio wahusu.kwani wao bado vijana hawaju wakitakacho,kesho kesho kutwa wataacha uongozi kwenda fata jambo lingine vision ikapote.

Huo ni mtazamo wangu tu wa kifasihi kutokana na beti za wahusika,hazihusiani na chochote kama hicho kwenye maana harisi ya tungo za wenyewe hao .
Ni hadithi tu nimeipata hapo hapo

kazi kwli kweli.Mbona sheikh Yahya ayumo humu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom