Vipi anakutesa? Tumia pesa!

Kazi kweli kweli.

Kuna jamaa yangu alikuwa ni mtu wa kubadili sana mabinti, kiukweli jamaa alikuwa anachukua mabinti wakali sana(wazuri) kwa kale katabia kake kakanifanya nitake kujua nini siri ya yeye kumilikini mabinti wazuri, ujana kweli unamambo mengi kila ukionacho wataka kujua, wakati huo nilikuwa katika mahusiano na binti fulani lakini penzi letu kila kukicha vibwanga, maumivu, vituko, lawama,migogoro, ndiyo yalikuwa sehemu ya maisha yetu basi.


Hivyo ilinipelekea kujiona kama kunakitu kinapungua katika mahusiano yetu, kila nilipokuwa naangalia kwa jamaa yangu jinsi anavyotoka na mabinti warembo sikuwahi kusikia akinisimlia wala kunipa lawama za mahusiano kama nilivyokuwa nikimhadithia, nikaanza kutaka kujua mbona iko hivyo kwangu, katika hizo harakati zangu za kumpeleleza kuna maswali kadhaa aliniuliza kutaka kujua chanzo cha kuumizwa na mapenzi basi katika majibu yangu ilionekana kwamba nina mkono wa birika( ubahili), akanimbia kitu kimoja kwamba mwanamke siku zote natakuthamini na kukuona wa maana kama unakitu, ndiyo maana unaona kwangu wanajipanga na kushoboka japo sio mzuri wa sura, ila pesa inanifanya niitwe handsome.

Akaniambia raha ya baby;
(1)Azawadiwe vinono
(2)Asuguliwe mgongo
(3)Mabusu sio kipigo
(4)Kisha tumia pesa.


Ilinichukua muda sana kuamini alichoniambia kwa kuwa nilikuwa naamini katika mapenzi ya kweli pesa sio kitu, na haina nafasi kusimamia mapenzi ili yawepo, kumbe nilikuwa na waza kinyume baada ya kudungua kwamba yule binti niliekuwa nae japo alikuwa anaonekana mwenye upendo kwangu lakini kuna kitu alikosa(pesa) hivyo ikamfanya atafute mtu wa kumwezesha pembeni.



Hatima ya mahusiano yale ikawa kuachana, nikasema ngoja aende kwa vile nilishaijua kununi yahawa watoto wazuri nikutumia pesa, sio shida sana nitampata mwingine nitatumia pesa, nikachukua muda kukaa alone huku nikiendelea kumfuatilia alichokua anakifanya yule jamaa yangu ndiyo siri ya kumiliki mabinti wazuri na kutokuumizwa na mapenzi, muda mwigi jamaa alipokuwa akienda kwenye mihadi yake nilikuwa naongoza nae tu, huko nilikuwa naishia kuitwa shemeji na wale watoto warembo na kunifisia kwa jamaa yangu kwamba rafiki yako mpole mara "Oooohhh ni hb" lol nilikuwa nachukia kimoyo moyo.


Ukafika muda wa kufanya maamuzi baada ya kuchoshwa na upweke na kuitwa shemeji, nikawa nimempata binti mmoja mzuri, nikarudi kutumia ile kanuni nikiamini hapa sitaumia tena, safari ya mapenzi ikanzia hapo nikawamtoaji mzuri sana nisiende kinyume na kanuni kila akitakacho binti nikawanamnunulia nguo,simu na vitu vingine sio tabu tena kwangu ikawa nikawaida tu kugharamia. Sipati kusimlia wala kuvimaliza vyote nilivyo toa.


Kizaza kukaja siku moja wakati nimelala na yule binti usiku, ilikuwa yapata saa nane usiku kwa vile yeye alikuwa amechoka na alikuwa ndani ya usingizi mzito sanaa, nikasema ngoja nichukue simu yake nianze kuchunguza, maana sikuwa nakawaida ya kumkagua kagua simu yake, nilichokikuta sikuamini usiku ule massage za wanaume tofauti tofauti kibao nyingine za mizinga, kualikana mitoko ni wazi sikuwa mwenyewe yani nitabu kiukweli nilishikwa na pressure ghafla hasira zikanijaa amani ikatoweka usiku ule, ugomvi ukazuka kati yetu baada kumuuliza, nilimbana akakili kosa, kutokana na hasira nilibamiza ile simu ukutani ikawa nyang'anyang'a nikampa makofi kadhaa na mapenzi yetu yakaishia usiku huo huo...


Mpaka leo najiuliza nini siri ya mapenzi ya kweli na kumfanya binti akupende??

Mwenye mapenzi ya kweli anatawaliwa na tamaa ya pesa.

Unaempatia pesa anatamani kuwa na wanaume wengi zaidi yako watakao mpatia pesa.

Au ukimpenda mtu basi usimchunguze ndiyo inaweza kuwa siri ya mapenzi????

Yule binti wa askofu ndo ushamtosa mkuu Phlagiey
 
Last edited by a moderator:
Yeroo

Ukitaka ustaajabu ya Musa kisha ukiyaona ya Firauni uzimie tazama kometi za wadada ndio utaona kuwa ni waongo

Watajidai eti "pesa sio kila kitu" wakati mioyo yao iko kwenye "pakee"

Hawa wadada bana ......!!


are u sure?
 
hahahaaaaa muraaaaa ulipata presha ya kupanda au kushuka?
Utofauti wenu na huyo jamaa yako ni kuwa mwenzio hakutaka ishu za kuwekeza while weye uliwekeza....
poleeeeee..... hahahaaaaa kwaiyo kuna nafasi iko wazi nikusaidie kuweka bandiko jf?
 
hahahaaaaa muraaaaa ulipata presha ya kupanda au kushuka?
Utofauti wenu na huyo jamaa yako ni kuwa mwenzio hakutaka ishu za kuwekeza while weye uliwekeza....
poleeeeee..... hahahaaaaa kwaiyo kuna nafasi iko wazi nikusaidie kuweka bandiko jf?
Unacheka kisha unanipa pole

Unamajungu wewe mtoto!!!

Nilipata presha ya kuteleza.

Wa humu jf ndiyo..... mmmmmhhhhh!!!!!!! Nitakuja na kisa chao kesho kutwa.
 
Yeroo

Ukitaka ustaajabu ya Musa kisha ukiyaona ya Firauni uzimie tazama kometi za wadada ndio utaona kuwa ni waongo

Watajidai eti "pesa sio kila kitu" wakati mioyo yao iko kwenye "pakee"

Hawa wadada bana ......!!
Money and love are two sides of the same coin....
 
Back
Top Bottom