Vipi anakutesa? Tumia pesa!

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,452
2,000
..::Kazi kweli kweli::..

Kuna jamaa yangu alikuwa ni mtu wa kubadili sana mabinti, kiukweli jamaa alikuwa anachukua mabinti wakali sana(wazuri) kwa kale katabia kake kakanifanya nitake kujua nini siri ya yeye kumilikini mabinti wazuri, ujana kweli unamambo mengi kila ukionacho wataka kujua, wakati huo nilikuwa katika mahusiano na binti fulani lakini penzi letu kila kukicha vibwanga, maumivu, vituko, lawama,migogoro, ndiyo yalikuwa sehemu ya maisha yetu.

Hivyo ilinipelekea kujiona kama kunakitu kinapungua katika mahusiano yetu, kila nilipokuwa naangalia kwa jamaa yangu jinsi anavyotoka na mabinti warembo sikuwahi kusikia akinisimlia wala kunipa lawama za mahusiano kama nilivyokuwa nikimhadithia, nikaanza kutaka kujua mbona iko hivyo kwangu, katika hizo harakati zangu za kumpeleleza kuna maswali kadhaa aliniuliza kutaka kujua chanzo cha kuumizwa na mapenzi basi katika majibu yangu ilionekana kwamba nina mkono wa birika( ubahili), akanimbia kitu kimoja kwamba mwanamke siku zote natakuthamini na kukuona wa maana kama unakitu, ndiyo maana unaona kwangu wanajipanga na kushoboka japo sio mzuri wa sura, ila pesa inanifanya niitwe handsome.

Akaniambia raha ya baby;
(1)Azawadiwe vinono
(2)Asuguliwe mgongo
(3)Mabusu sio kipigo
(4)Kisha tumia pesa.

Ilinichukua muda sana kuamini alichoniambia kwa kuwa nilikuwa naamini katika mapenzi ya kweli pesa sio kitu, na haina nafasi kusimamia mapenzi ili yawepo, kumbe nilikuwa na waza kinyume baada ya kudungua kwamba yule binti niliekuwa nae japo alikuwa anaonekana mwenye upendo kwangu lakini kuna kitu alikosa(pesa) hivyo ikamfanya atafute mtu wa kumwezesha pembeni.

Hatima ya mahusiano yale ikawa kuachana, nikasema ngoja aende kwa vile nilishaijua kununi yahawa watoto wazuri nikutumia pesa, sio shida sana nitampata mwingine nitatumia pesa, nikachukua muda kukaa alone huku nikiendelea kumfuatilia alichokua anakifanya yule jamaa yangu kama ndiyo siri ya kumiliki mabinti wazuri na kutokuumizwa na mapenzi, muda mwigi jamaa alipokuwa akienda kwenye mihadi yake nilikuwa naongoza nae tu, huko nilikuwa naishia kuitwa shemeji na wale watoto warembo na kunifisia kwa jamaa yangu kwamba rafiki yako mpole mara "Oooohhh ni hb" lol nilikuwa nachukia kimoyo moyo.

Ukafika muda wa kufanya maamuzi baada ya kuchoshwa na upweke na kuitwa shemeji, nikawa nimempata binti mmoja mzuri, nikarudi kutumia ile kanuni nikiamini hapa sitaumia tena, safari ya mapenzi ikanzia hapo nikawamtoaji mzuri sana nisiende kinyume na kanuni kila akitakacho binti nikawanamnunulia nguo,simu na vitu vingine sio tabu tena kwangu ikawa nikawaida tu kugharamia. Sipati kusimlia wala kuvimaliza vyote nilivyo toa.

Kizaza kikaja siku moja wakati nimelala na yule binti usiku, ilikuwa yapata saa nane usiku kwa vile yeye alikuwa amechoka na alikuwa ndani ya usingizi mzito sanaa, nikasema ngoja nichukue simu yake nianze kuchunguza, maana sikuwa nakawaida ya kumkagua kagua simu yake, nilichokikuta sikuamini usiku ule massage za wanaume tofauti tofauti kibao nyingine za mizinga, kualikana mitoko ni wazi sikuwa mwenyewe yani nitabu kiukweli nilishikwa na pressure ghafla hasira zikanijaa amani ikatoweka usiku ule, ugomvi ukazuka kati yetu baada kumuuliza, nilimbana akakili kosa, kutokana na hasira nilibamiza ile simu ukutani ikawa nyang'anyang'a nikampa makofi kadhaa na mapenzi yetu yakaishia usiku huo huo...


Mpaka leo najiuliza nini siri ya mapenzi ya kweli na kumfanya binti akupende??

Mwenye mapenzi ya kweli anatawaliwa na tamaa ya pesa.

Unaempatia pesa anatamani kuwa na wanaume wengi zaidi yako watakao mpatia pesa.

Au ukimpenda mtu basi usimchunguze ndiyo inaweza kuwa siri ya mapenzi????
 

ChickMagnet

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,792
2,000
Acheni kujidanganya nyie..... Eti nipende tu na kuniheshimu! Sasa utakula na kuvaa hiyo heshima yake? Pesa ndo kila kitu! Asikwambie mtu.... Yaani ukiwa nazo hata huangaiki kutongoza ,wanakujaa tu wenyewe
 

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Mar 21, 2013
37,146
2,000
Acheni kujidanganya nyie..... Eti nipende tu na kuniheshimu! Sasa utakula na kuvaa hiyo heshima yake? Pesa ndo kila kitu! Asikwambie mtu.... Yaani ukiwa nazo hata huangaiki kutongoza ,wanakujaa tu wenyewe

money is not everything na hao wanaokuja watakuja kwa ajil ya pesa zako zikiisha unadhani watabakia

halaf kama wewe wajishugulisha huwez kukaa ubabaikie pesa ya mwanaume kuwa hana pesa
kinacho matter uwe na mtu mwenye vision na maisha
 

Asnam

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
4,258
1,225
moyo ndo kila kitu,ukikuongoza kwenye pesa basi ukiona wallet mapenzi yanafufuka,ukikuongoza kwingine ndo hivyo tena....mapenzi hayana formula
 

mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,470
2,000
Mapenzi ya kweli hayahusiani kabisa na mambo ya pesa, ukiona unapendwa kwa ajili ya pesa au kwa vile unajua kuhonga sana ujue hapo hakuna mapenz bali kinachopendwa ni hizo pesa zako na akija mwingine mwenye nazo zaidi yako au mtoaji zaidi yako lazma watakulia tu, na hata ikitokea ukamuoa mwanamke wa hivyo ujue siku ukizikosa na ndoa imekufa. Mimi mme wangu enzi za gf na bf mpaka uchumba sikuwa na pewa chochote na uwezo anao ila kupewa hela ilikuwa mpka niombe na penyewe ntaulizwa maswali mpka naweza kususa, so nilikuwa naomba only nnapokuwa na shida hasa, hela yake naifaidi sahz baada ya kuolewa
 

ChickMagnet

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,792
2,000
money is not everything na hao wanaokuja watakuja kwa ajil ya pesa zako zikiisha unadhani watabakia

halaf kama wewe wajishugulisha huwez kukaa ubabaikie pesa ya mwanaume kuwa hana pesa
kinacho matter uwe na mtu mwenye vision na maisha

nakataa mpaka kesho kutwa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom