Vipaji,Umaarufu na watoto wetu.....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,847
Kuanzia Marekani mpaka hapa TZ inaonekana
umaarufu 'huharibu' watoto vibaya mno....

ndo maana ni kawaida kusikia watu maarufu wakikataza
watoto wao kujishughulisha na sanaa au michezo au kazi za kuwapa umaarufu wakati
bado wadoogo....

sasa wakati kila mtu anazungumza ya Kanumba na Lulu nilikuwa sijui kuwa

Lulu kumbe alikuwa maarufu toka mtoto kwa kutangaza ITV...

na nikikumbuka watoto wengine weengi walioshindwa kusoma
na kuingia kwenye matatizo kwa kuwa maarufu toka utotoni....

nauliza swali hili kwa wana jf....mtoto wako kama ana kipaji

cha kutangaza tv au kuigiza filam au kuimba nyimbo.....utamruhusu

'aoneshe kipaji chake'?

wewe swala la madhara ya umaarufu kwa watoto na hata teenagers umalichukuliaje?????
 
Mtoto wangu hata awe na kipaji vipi, lazima aende kusoma.

Akisha soma nikajua ana elimu ya kutosha, hapo sasa yeye ndo ataamua kufanya nini, huo ni uchaguzi wake.
 
Mtoto wangu hata awe na kipaji vipi, lazima aende kusoma.

Akisha soma nikajua ana elimu ya kutosha, hapo sasa yeye ndo ataamua kufanya nini, huo ni uchaguzi wake.

lakini vipaji vingine vinatakiwa
kuendelezwa tangia utotoni
mfano mpira
unasemaje hapo?
 
The Boss kwa kweli kuna kujiuliza maswali mara mbili mbili
Je nikimruhusu madhara yake yatakuwa ni nini
na je masuala ya elimu itakuwaje
je atazingatia tena elimu akishapata huo umaarufu au akiwa anafanya kazi akiwa mdogo
na je anaelewa madhara ya kuwa maarufu akiwa mdogo
Hapo ndipo wazazi wengi tunajiuliza maswali hayo na uamuzi utakaoupata ndio unakuambia hapo yes unaweza kumruhusu mtoto wako au hapana
 
lakini vipaji vingine vinatakiwa
kuendelezwa tangia utotoni
mfano mpira
unasemaje hapo?
Si naye mmoja yeye anaitwa messi hahaha, lakini usiombe mama yake amemzungushia walimu, yani anaenda kucheza tena anapewa time saa flani awe karudi.
 
The Boss bado sana hatujajua namna ya kuhandle issue za watoto ambao wana hivyo vipaji wakiwa wadogo
Bado hatujaweza kuviendeleza na hakuna shule maalum za kufanya hayo mambo na kuwaweka katika misingi ya kuwa pamoja na kipaji chako elimu nyingine iendelee
At least kungekuw ana namna ya kuwafanya watoto waendeleze vipaji vyao na huku wakiwa wanaendelea na elimu ya kawaida hapo sawa
huku unaweza kumwachia aendelee na kipaji chake ukajikuta hata muda wa kupata elimu ya kawaida hakuna na anaishia kupata umaarufu ambao utamcost baadae bila kujua kuwa kipaji chake kinatakiw akuendana na elimu
 
hata huko kwenye nchi zenye shule maalum
watoto wanaharibika

je zingekuwepo shule hizo hapa TZ..wewe ungewaruhusu wako?
 
Mi sioni ubaya, but mzazi anatakiwa kua makini na kumsaidia mtoto kuishi utoto wake wote. Sio mtoto wa miaka 13 unampa uhuru wa mtu mzima just because she makes money out of her talent. Guide the kid, inculcate your values and teach her the tricks of life, step by step, just like for all other children. It would be unfair not to promote the gift he/she has.
 
Mchakato wa Kukuza Kipaji cha mtoto ni sahihi ukaanzia katika mazingira ya wazazi tu nyumbani na wanafamilia wachache, shuleni na kanisani / msikitini/sinagogini/jamatin n.k. Kipaji kikianza kukuzwa kupitia umma(public) mtoto anaanza kuwa katika mazingira hatarishi (exposed to vulnerable environment and she/he will be a victim of all shits) Mapakashume yatamnyemelea ili wapate kipato, mafataki yatatoa udenda, wenye wivu watapanga yao.

Nionavyo mimi ni bora kumwacha mtoto akue na vipaji vyake kwa hatua. Maendeleo yeyote katika kila sekta huwa ni "of spiral nature" yaani unaendelea kwa kwenda mbele hatua mbili unakosea na kurudi nyuma kwa hatua moja au mbli hizo hizo au hata tatu, unaanza tena kwa kujisahihisha na kwenda mbele tena. hiyo ndiyo kanuni ya maendeleo.

Hivyo mtoto anapopambana na umaarufu mapema analewa sifa, anajiamini kupita kiasi, anashindwa kuhimili sifa hizo, ata sema ndiyo kwenye kila kitu maana anataka umaarufu wake usipotee. Anataka Cheeap popularity. Yeye hajui kama anaharibikiwa uwezo wake wa kupambanua masuala ni mdogo maskini.
 
Mi nafikiri tatizo c mtoto kupewa nafasi ya kuendeleza kipaji chake bali ni uangalizi wa wazazi/walezi. Kuna baadhi ya wazazi/walezi ambao wanakuwa na ile mitizamo ya kikale pindi anapoambiwa mambo mabaya anayoyafanya mwanae/bintie, huwa wanaona watoto wao wanaonewa wivu n.k huwa wanawatetea na hivyo kuchangia kuharibika kwao.

Pia inategemea aina ya kipaji na njia za kukiendeleza, kipaji kinatakiwa kuendelezwa kwa awamu kulingana na umri wa mhusika, mtoto anatakiwa kuchukuliwa kwa nafasi yake ni c kumchukulia kwa ujumla, cc hatuna mfumo wa namna hii hivyo kila mwenye kipaji awe mtoto au m2 mzima yupo kwenye kandi moja na sheria ya pori ndo inatumika mwenye ubavu/ushawishi ndo ataendelea kuwepo.
Kila wakati ukiangalia au kusikiliza mahojiano ya wasanii chipukizi ambao wengi ni<18 wanapoulizwa wanaowawezesha wengi wanakuwa wanajisimamia wenyewe au kutumia marafiki ,hivyo iwapo mzazi/mlezi hujampa msaada(kimawazo/kifedha) mwanao ili atoke usidhani utaweza kumshauri/kumwongoza akishatoka.
 
aaaa!yaan nntakiendeleza na kama kinaonekqna akiwa mdogo nntampa kila aina ya support akifanyie kazi.napenda sana vipaji na vivalue sana
 
Unaweza ukamruhusu mtoto ku-EXPLORE ki/vipaji vyake
huku ukim-limit kwa kiasi fulani badala ya kumu-EXPOSE all the way.

Ulaya (naongea from experience) . . .watoto huwa wanaenda shule kama kawaida huku pembeni (muda wa ziada) wakijifunza/hangaika na hivyo tunavyoweza kuita vipaji. Kama ni kupiga chombo cha mziki, kucheza michezo ya athletic, kuimba, kucheza mziki vinakua ni "SIDE" things mpaka baadae mtoto anapokomaa. Binafsi niliruhusiwa kujifunza kila nilichoonekana napenda/naweza (kuimba, kupiga kinanda, kupika, kufuma, kushona, kuandika,michezo kidogo n.k) bila ya kuvipa hivyo vitu kipaumbele. Darasa lilitangulia ndo na hayo yakafuata. Sasa hivi nikiamua kujikita kwenye kuimba sijui kuandika siwezi angukia pua maana sikusukumizwa huko kwenye umaarafu ila niliruhusiwa kujiweka sawa ili nikomae.

Tatizo linatokea pale mzazi anapoamua kumtumia mtoto kama kitega uchumi hata pale ambapo mtoto anakua bado sana. Kwahiyo ni vizuri kugundua na kuendeleza vipaji vya watoto wangali wadogo ila sio kuvitumia wakati bado hawajakomaa vyakutosha.
 
The Boss na wana jf wote mliochangia hii hoja nzuri sana nami nimejifunza mambo muhimu, kwangu mm nadhani elimu ni msingi wa kila jambo ktk dunia ya leo, ni bora adumaze hicho kipaji ili apate elimu kwani naadhani itakuwa ni namna pia ya kukiendeleza hicho kipaji kwa manufaa/mafanikio makubwa zaidi, na bila elimu anaweza kuneemesha wengine bila yeye kutabua...
 
aaaa!yaan nntakiendeleza na kama kinaonekqna akiwa mdogo nntampa kila aina ya support akifanyie kazi.napenda sana vipaji na vivalue sana

je madhara ya umaarufu kwa watoto unayazungumziaje?
 
The Boss na wana jf wote mliochangia hii hoja nzuri sana nami nimejifunza mambo muhimu, kwangu mm nadhani elimu ni msingi wa kila jambo ktk dunia ya leo, ni bora adumaze hicho kipaji ili apate elimu kwani naadhani itakuwa ni namna pia ya kukiendeleza hicho kipaji kwa manufaa/mafanikio makubwa zaidi, na bila elimu anaweza kuneemesha wengine bila yeye kutabua...

kama hana uwezo wa kusoma sana je?
 
Unaweza ukamruhusu mtoto ku-EXPLORE ki/vipaji vyake
huku ukim-limit kwa kiasi fulani badala ya kumu-EXPOSE all the way.

Ulaya (naongea from experience) . . .watoto huwa wanaenda shule kama kawaida huku pembeni (muda wa ziada) wakijifunza/hangaika na hivyo tunavyoweza kuita vipaji. Kama ni kupiga chombo cha mziki, kucheza michezo ya athletic, kuimba, kucheza mziki vinakua ni "SIDE" things mpaka baadae mtoto anapokomaa. Binafsi niliruhusiwa kujifunza kila nilichoonekana napenda/naweza (kuimba, kupiga kinanda, kupika, kufuma, kushona, kuandika,michezo kidogo n.k) bila ya kuvipa hivyo vitu kipaumbele. Darasa lilitangulia ndo na hayo yakafuata. Sasa hivi nikiamua kujikita kwenye kuimba sijui kuandika siwezi angukia pua maana sikusukumizwa huko kwenye umaarafu ila niliruhusiwa kujiweka sawa ili nikomae.

Tatizo linatokea pale mzazi anapoamua kumtumia mtoto kama kitega uchumi hata pale ambapo mtoto anakua bado sana. Kwahiyo ni vizuri kugundua na kuendeleza vipaji vya watoto wangali wadogo ila sio kuvitumia wakati bado hawajakomaa vyakutosha.

niko curious kujua ni nchi gani hiyo ulikulia...
but kwa TZ huoni bora mzazi akamkazania mtoto wake shule zaidi?
 
Kukuza kipaji ni kitu kingine na umaarufu ki kitu kingine.

Kama mtoto atasaidiwa kukuza kipaji bila kujituka ametumbukia kwenye umaarufu basi atasaidiwa.

Lakini mambo ya mtoto wa miaka 8 ana fans all over the country kila anakopita watu wanamtolea macho, na wengine hata kutamani asaini sijui nini zao HAPANA, hata kama itamfanya awe milionea, NO.

Umaarufu katika umri mdogo ni mzigo kwa mtoto na wachache sana wameweza kutoka watu na akili zao timamu, siwezi fanya majaribio hayo kwa mtoto wangu lol
 
Back
Top Bottom