VIP Lounge na AC ya kuzidi

VIP Lounge na AC ya kuzidi

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
Naingia pub moja Kinondoni, sehemu ambayo wao huita VIP, au Lounge. Ni pazuri, pako kiheshima na hakuna fujo kama sehemu zingine za bar hii. Hata kama una mazungumzo ya biashara ni mahali pazuri pa kuyafanyia.

Nafurahishwa na mandhari isipokuwa jamaa wameweka AC kubwa sana, baridi kama MAfinga vile. Wahudumu hawana wasiwasi, wao wamevaa makoti ya suti so wanajisikia poa, kazi kwetu sie tuliokuja na vipande vya nguo. Zaidi ya mara moja inatulazimu (mimi na wateja wengine) kwenda kwenye kiambaza nje ili walau tupate hewa nzito ya Mungu ambayo ina nafuu mara mia..

Jamaa yangu ananitonya kuwa eti wanafanya hivyo makusudi ili tusilewe haraka hivyo kukuza mauzo, namwomba msimamizi wa pale apunguze hiyo mashine ya hewa anakataa katakata. Loh...

Pamoja na uzuri wa sehemu ile si mahala ambapo natamani tena kurudi, bora niendelee kunywa dukani kwa mangi.

e225.jpg


cc: Kaizer, Baba V
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mphamvu si ungenistua tukaenda wote vipi pana totoza za kutosha?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mphamvu si ungenistua tukaenda wote vipi pana totoza za kutosha?

Kinondoni kwa dhambi tu hawajambo. We hata ukitaka yutong yenye injini kwa nyuma, wewe tu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom