Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kwa kweli kama kuna kitu kinanikera hapa nchini kwetu hususani Dar ni matumizi ya kipoza hewa au a.c sijui ni ulimbekeni wetu au ni nini unakuta unaingia mahali a.c imewashwa utafikiri uko Makambako baridi mpaka unatafuta sweta na hii karibu kila ofisi unayoingia sasa usilogwe uende kwenye harusi ambazo kumbi zake zina a.c ni lazima utaondoka mgonjwa na hiyo baridi, kwa nini tunatesana hivi?
Unakuta nje kuna nyuzi joto zaidi ya 30° lkn ndani kuna ac inapoza mpaka nyuzi 18° sasa hii ni balaa na ni hatari hata kwa afya!
Kuna siku nilibahatika kuingia Ukumbi wa Bunge nilijuta kwa maana hata kutoka nje huwezi mpaka Bunge liishe nilipigwa na a.c na nikasema sirudii tena, sasa ni kwa nini hawawaambii wageni kabla hawajaingia kwamba waje na makoti?