Oltung'anyi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 284
- 196
Baadhi ya viongozi wetu wakubwa wamekuwa wasuluhishi wa migogoro kadhaa nje ya Tanzania. Mingi ni ile itokanayo na migogoro baada ya uchaguzi.
Raisi Kikwete alisha alikwa Kenya kusuluhisha mgogoro mkubwa uliotokana na uchaguzi mkuu. Hali kadhalika, raisi mstaafu, Benjamini Mkapa, naye ameshiriki katika usuluhishi wa migogoro ya aina hii.
Tanzania imekuwa ikitoa wanajeshi wake kwenda kushiriki katika harakati mbali mbali za kiusalama katika nchi zenye machafuko hususani yatokanayo na kugombania madara.
Ninachojiuliza hapa ni kuwa, ni kwa nini mambo ambayo viongozi wetu wanayashughulikia katika nchi nyingine ndio hayo yanayotokea nchini kwetu huku wasuluhishi hao wakihusika kwa namna moja ama nyingine kwenye matatizo hayo hayo wanayoyatatua nchi nyingine?. Hili haliniingi akilini kabisa. Tanzania ilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa hususani kwenye swala hili la kidemokrasia la uchaguzi, lakini hali ni tofauti kabisa.
Wasuluhishi wengine wanabaki wakimya pamoja na kuwa na sifa kuuuuubwa ya usuluhishi wa migogoro nje ya nchi. Sina hakika kama Raisi Mstaafu Benjamin Mkapa alizungumza lolote kuhusiana na hali ya utata iliyojitokeza kwa Jk kutangazwa mshindi.
Tanzania ilitakiwa iwe mfano wa kuigwa na haikupaswa kuwa na migogoro ya uchaguzi inayowahusisha wasuluhishi wanaoheshimika katika utatuzi wa migogoro ya aina hii nje ya Tanzania. Ni aibu, ni jambo la kushangaza, na haliingii akilini kabisa.
Huu ni unafiki mkubwa kabisa. Ni aibu kwao, ni aibu kwa Tanzania.