Viongozi wetu na unafiki wa usuluhishi nje ya nchi.

Oltung'anyi

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
285
250
Baadhi ya viongozi wetu wakubwa wamekuwa wasuluhishi wa migogoro kadhaa nje ya Tanzania. Mingi ni ile itokanayo na migogoro baada ya uchaguzi.

Raisi Kikwete alisha alikwa Kenya kusuluhisha mgogoro mkubwa uliotokana na uchaguzi mkuu. Hali kadhalika, raisi mstaafu, Benjamini Mkapa, naye ameshiriki katika usuluhishi wa migogoro ya aina hii.

Tanzania imekuwa ikitoa wanajeshi wake kwenda kushiriki katika harakati mbali mbali za kiusalama katika nchi zenye machafuko hususani yatokanayo na kugombania madara.

Ninachojiuliza hapa ni kuwa, ni kwa nini mambo ambayo viongozi wetu wanayashughulikia katika nchi nyingine ndio hayo yanayotokea nchini kwetu huku wasuluhishi hao wakihusika kwa namna moja ama nyingine kwenye matatizo hayo hayo wanayoyatatua nchi nyingine?. Hili haliniingi akilini kabisa. Tanzania ilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa hususani kwenye swala hili la kidemokrasia la uchaguzi, lakini hali ni tofauti kabisa.

Wasuluhishi wengine wanabaki wakimya pamoja na kuwa na sifa kuuuuubwa ya usuluhishi wa migogoro nje ya nchi. Sina hakika kama Raisi Mstaafu Benjamin Mkapa alizungumza lolote kuhusiana na hali ya utata iliyojitokeza kwa Jk kutangazwa mshindi.

Tanzania ilitakiwa iwe mfano wa kuigwa na haikupaswa kuwa na migogoro ya uchaguzi inayowahusisha wasuluhishi wanaoheshimika katika utatuzi wa migogoro ya aina hii nje ya Tanzania. Ni aibu, ni jambo la kushangaza, na haliingii akilini kabisa.

Huu ni unafiki mkubwa kabisa. Ni aibu kwao, ni aibu kwa Tanzania.
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,698
2,000
Ni kutaka kujionyesha kwamba kwao hawana matatizo.
Kikwete aliumbuka siku Chadema walipotoka nje ya ukumbi siku analifungua bunge. Siri ilikuwa wazi kuwa kumbe hata yeye ni mchakachuaji!
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,320
1,195
Baadhi ya viongozi wetu wakubwa wamekuwa wasuluhishi wa migogoro kadhaa nje ya Tanzania. Mingi ni ile itokanayo na migogoro baada ya uchaguzi.

Raisi Kikwete alisha alikwa Kenya kusuluhisha mgogoro mkubwa uliotokana na uchaguzi mkuu. Hali kadhalika, raisi mstaafu, Benjamini Mkapa, naye ameshiriki katika usuluhishi wa migogoro ya aina hii.

Tanzania imekuwa ikitoa wanajeshi wake kwenda kushiriki katika harakati mbali mbali za kiusalama katika nchi zenye machafuko hususani yatokanayo na kugombania madara.

Ninachojiuliza hapa ni kuwa, ni kwa nini mambo ambayo viongozi wetu wanayashughulikia katika nchi nyingine ndio hayo yanayotokea nchini kwetu huku wasuluhishi hao wakihusika kwa namna moja ama nyingine kwenye matatizo hayo hayo wanayoyatatua nchi nyingine?. Hili haliniingi akilini kabisa. Tanzania ilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa hususani kwenye swala hili la kidemokrasia la uchaguzi, lakini hali ni tofauti kabisa.

Wasuluhishi wengine wanabaki wakimya pamoja na kuwa na sifa kuuuuubwa ya usuluhishi wa migogoro nje ya nchi. Sina hakika kama Raisi Mstaafu Benjamin Mkapa alizungumza lolote kuhusiana na hali ya utata iliyojitokeza kwa Jk kutangazwa mshindi.

Tanzania ilitakiwa iwe mfano wa kuigwa na haikupaswa kuwa na migogoro ya uchaguzi inayowahusisha wasuluhishi wanaoheshimika katika utatuzi wa migogoro ya aina hii nje ya Tanzania. Ni aibu, ni jambo la kushangaza, na haliingii akilini kabisa.

Huu ni unafiki mkubwa kabisa. Ni aibu kwao, ni aibu kwa Tanzania.

Wasuluhishe nini sasa wakati hakuna mgogoro wa uchaguzi ?. Ni uroho wa madaraka wa wachache ambao wameshindwa uchaguzi wa kidemokrasia kwa njia ya kura, ndio wanao jifanya kuwa nchi iko kwenye mgogoro wa uchaguzi, kumbe hakuna lolote. Na janja yao imeshtukiwa, wamekuwa wadogo kama piliton
 
Kwani kikwete na wewe mna akili ya kuona yaliyo nyumbani kwenu? kama hakuna mgogoro mbona alitoa comment ya "watakwenda watarudi?"
 
Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,374
2,000
Baadhi ya viongozi wetu wakubwa wamekuwa wasuluhishi wa migogoro kadhaa nje ya Tanzania. Mingi ni ile itokanayo na migogoro baada ya uchaguzi.

Raisi Kikwete alisha alikwa Kenya kusuluhisha mgogoro mkubwa uliotokana na uchaguzi mkuu. Hali kadhalika, raisi mstaafu, Benjamini Mkapa, naye ameshiriki katika usuluhishi wa migogoro ya aina hii.

Tanzania imekuwa ikitoa wanajeshi wake kwenda kushiriki katika harakati mbali mbali za kiusalama katika nchi zenye machafuko hususani yatokanayo na kugombania madara.

Ninachojiuliza hapa ni kuwa, ni kwa nini mambo ambayo viongozi wetu wanayashughulikia katika nchi nyingine ndio hayo yanayotokea nchini kwetu huku wasuluhishi hao wakihusika kwa namna moja ama nyingine kwenye matatizo hayo hayo wanayoyatatua nchi nyingine?. Hili haliniingi akilini kabisa. Tanzania ilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa hususani kwenye swala hili la kidemokrasia la uchaguzi, lakini hali ni tofauti kabisa.

Wasuluhishi wengine wanabaki wakimya pamoja na kuwa na sifa kuuuuubwa ya usuluhishi wa migogoro nje ya nchi. Sina hakika kama Raisi Mstaafu Benjamin Mkapa alizungumza lolote kuhusiana na hali ya utata iliyojitokeza kwa Jk kutangazwa mshindi.

Tanzania ilitakiwa iwe mfano wa kuigwa na haikupaswa kuwa na migogoro ya uchaguzi inayowahusisha wasuluhishi wanaoheshimika katika utatuzi wa migogoro ya aina hii nje ya Tanzania. Ni aibu, ni jambo la kushangaza, na haliingii akilini kabisa.

Huu ni unafiki mkubwa kabisa. Ni aibu kwao, ni aibu kwa Tanzania.

Ninyi watu munanishangaza! Nyimbo wanayoimba Mkapa na wenzake ni “ushindi lazima, mapinduzi daima”. Kwao ni kuwa hakuna mgogoro, hakuna matatizo. Huwa wametoa onyo mapema na hakuna anayelalamika kwa Tendwa kwa kauli hizo.

Huwa tunawaona mataahira, wanapopofanya kweli, wakati mchezo umekwisha ,tunakuja, oh,oh, ahh, foul.

Lakini, jamaa wanacheka, wanatukumbusha,” hivi ninyi hamkuamini kuwa tulishawaambia kuwa ushindi ni lazima, ninyi ni wasindikizaji tu?”

CCM wanajuwa wanawaongoza nani!!!!

See how smart (negatively) these guys are! They have just snatched the Katiba mpya, mabadiliko ya katiba issue, they are on a driving seat now.

Tuendelezeni longo longo na kupongezana!
Tuendelezeni longolongo na kuwa disorganized!
Tuendelezeni longo longo na siasa maji taka!

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo woteeee!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom