Jamani tunashindwa kuwa serious hata kidogo inajulikana huu uprofesa wakujipa lakini bungeni anaitwa hivyo hivyo ajabu kabisa.Huko marekani uprofessor ni wa chuo kikuu hakuna uprofessor kwenye siasa. kama wewe ni professor wa chuo ikiwa mwanasiasa inaachana na title ya u professor kama akina Obama na Rice. Hapa kwetu mganga wa kienyeji anatumia jina prof. anatinga bungeni na bado anaonekana kuwa addressed kama professor! Ma dr. fake wanajulikana lakini bado wanaitwa ma dr katika taarifa rasmi za bunge na serikali! Najua ID yangu nikiongeza Prof. litapendeza sana yaani kuanzi sasa nami niitwe Prof. Kimbunga. Kama wewe mkuu kisha nione nani ataniuliza.
Umesahau dr. dr E Nchimbi.Labda tungekuwa tunawauliza kwenye mikutano ya kampeni, warsha. makongamano na vikaoni wateleze phd/thesis zao zimetusaidiaje kama taifa.DR. J.M Kikwete, DR G.Bilal, Eng. Stella Manyanya, DR Asharose Migiro, DR Mary Nagu, Eng. C. Chyzya, Prof. Maji Marefu, DR Shukuru Kawambwa, Prof I. Lipumba, DR. W.Slaa, Pof. Mark Mwanosya, DR. Hussein Mwinyi, Prof. Jumanne Maghembe, DR H. Mwakyembe.Hyo ni THELUTHI ya orodha ya viongozi wetu. Ndo hvyo, elimu tittle, but how it helped us. GOD KNOWS
Pia nilimuona lady wa kwanza wa nchi akisema "serikali ya dr dr dr dr........ ina nia njema ya kuleta maendeleo"Tupo ndani ya mfumo wa usanii, kwa hiyo hizo title ni za kisanii zaidi. Nakumbuka wakati tunaelekea uchaguzi mkuu 2010 mgombea mmoja alitunukiwa PHD 2 za fasta fasta ili kukidhi mahitaji ya wakati huo.
Pia vyombo vya habari vikaelezwa kuitaja hiyo title yaani Dr, katika kila wanchoongelea kumhusu.
Ukiangalia hazina tija, Dr, professor everywhere lakini matendo hayaendani na title zenyewe. Shame on Them.
Umesahau dr. dr E Nchimbi.Labda tungekuwa tunawauliza kwenye mikutano ya kampeni, warsha. makongamano na vikaoni wateleze phd/thesis zao zimetusaidiaje kama taifa.
Ni kweli hata mie naunga mkono kuwa wanataka kuwa "juu". Ndugu Bill Mwalimu Nyerere Alitunukiwa kuwa PROFESA na Chuo Kikuu Dar lakini alikataa kwa kusema: Nanukuu: "Neno Profesa asili yake ni Kifaransa, likimaanisha Mwalimu. Nyie (Watanzania) Mnaniita Mwalimu, kwa hiyo sijaukataa uprofesa wenu ila labda tu kuwa tofauti ya lugha". Hii ilikuwa kati ukumbi wa ATB pale Mlimani, mwezi Desemba 1997. Mie nilikuwa ndani ya ukumbi!
Hawa dawa yao moja tu: KuTOTUMIA title hizi TUNAPOWA adress!
Itasaidia sana sana. Pengine iwekwe sheria km ile ya kutangaza mali zao, basi waniike hadharani elimu zao, na wamezipataje, na waeleze wataifanyai nini Tanzania kupitia elimu zao.
Nakuunga mkono majina ya kiacademic yaheshimiwe na yasitumiwe kiholela. Otherwise kuwe na sheria ya kukataza vijititle kwa viongozi.
DR. J.M Kikwete, DR G.Bilal, Eng. Stella Manyanya, DR Asharose Migiro, DR Mary Nagu, Eng. C. Chyzya, Prof. Maji Marefu, DR Shukuru Kawambwa, Prof I. Lipumba, DR. W.Slaa, Pof. Mark Mwanosya, DR. Hussein Mwinyi, Prof. Jumanne Maghembe, DR H. Mwakyembe.
Hyo ni THELUTHI ya orodha ya viongozi wetu. Ndo hvyo, elimu tittle, but how it helped us. GOD KNOWS
Nadhani kabla ya 2015 tutakuwa na Dr. Wasira na Dr. Riz 1Just wait and see
Afadhali basi uwe na udr. wa ukweli ina maana kidogo! kuliko huu wa kuchakachua. Bwana atusaidie sana sisi wananchi kwa sababu tukisikia dr. tu tunapagawa bia kujiuliza udr. huu ameupataje? na unatusaidia nini katika maisha yetu ya kila siku. Bwana aturehemu.Haswaaa. Maana wamezidi Udr mwingine wanapeana bar, alafu wanatuletea sisi. Ijulikane km no dr umeipataje na je inakustahili?
Maana wamezidi.
Na kwani ukiitwa tu jina lako hata km una cheo, na umesoma sana utapungua nini?
Kazi tunayo, ukiangalia wengi wao ni brain at rest.
What makes no sense, can you explain a little bitmore?It make no sense.
Ahhahhh ndiyo maana akina kingunge, malecela wanang'ang'ania siasa tu hawana kingine cha kufanya? ivi huyu malecela nae ni dr. na kama ni dr. mbona sionagi hiyo taito kwenye jina lake au ni wale wasiosoma kabisa?Nashukuru kwa kuadd kwenye hii list mkuu, naamini kama wataipitia hii thread watabadilika. Kama ulivyosema wataalamu wakimaliza muda wa vyeo vyao vya kisiasa wanarudi kwenye taaluma zao hapa kwetu wanang'ang'ania siasa mpaka wanazeekea humohumo wanaogopa hawawezi kucompete kwenye soko la ajira ndio maana wapo radhi kutetea ujinga ilimradi anabaki kwenye nafasi yake. TUBADILIKE tuwe wawazi na wakweli na tujiamini kwa vipaji/abilities tulizonazo.