Viongozi wetu na 'title' bandia

Viongozi wetu na 'title' bandia

Duh, pamoja na kuandikiwa kuwa ile ni honorary degree (Honoris causa) bado tu unataka kujua thesis yake imesaidiaje taifa! Chuki binafsi? Kwa nini usiulize ya Dr Kikwete.

Samahani mkuu sina chuki na kiongozi yeyote nilikuwa sijatambua kwamba ni udocta wa heshima ndio maana nikauliza hilo swali maadamu umenielewesha basi swali langu halihold water, nimelifuta.
 
Tupo ndani ya mfumo wa usanii, kwa hiyo hizo title ni za kisanii zaidi. Nakumbuka wakati tunaelekea uchaguzi mkuu 2010 mgombea mmoja alitunukiwa PHD 2 za fasta fasta ili kukidhi mahitaji ya wakati huo.

Pia vyombo vya habari vikaelezwa kuitaja hiyo title yaani Dr, katika kila wanchoongelea kumhusu.

Ukiangalia hazina tija, Dr, professor everywhere lakini matendo hayaendani na title zenyewe. Shame on Them.

Ukweli mtupu!!!
 
Title hizi zitumike kwa wale wanaofundisha vyuo na watafiti. Ukiingia ktk siasa ama kazi yoyote ambayo siyo ya taaluma yako basi uitwe kwa jina lako la kawaida. Wapo wengi tu,wengine wanapenda jiita majaji wastaafu,mkuu wa mkoa mstaafu,nk.
 
Naunga mkono hoja
 
Ona wenzetu ni profesa lakini anaaddressiwa kwa majina yake ya kawaida hawa ni wachumi ambao walinomenitiwa kwenye Central bank ya US. Chakufurahisha zaidi ni watumishi wa umma lakini wanajulikana ni waumini wa ideology gani/chama gani.
In late December, 2011, President Barack Obama nominated two individuals to fill the vacant seats on the board, Jeremy Stein, a Harvard University finance professor and a Democrat, and Jerome Powell, formerly of Dillon Read, Bankers Trust and The Carlyle Group and a Republican. Both candidates also have Treasury Department experience in the Obama and George H.W. Bush administrations respectively.

"Obama administration officials regrouped to identify Fed candidates after Peter Diamond, a Nobel Prize-winning economist, withdrew his nomination to the board in June [2011] in the face of Republican opposition. Richard Clarida, a potential nominee who was a Treasury official under George W. Bush, pulled out of consideration in August [2011]", one account of the December nominations noted. The two other Obama nominees in 2011, Yellen and Raskin, were confirmed in September. One of the vacancies was created in 2011 with the resignation of Kevin Warsh, who took office in 2006 to fill the unexpired term ending January 31, 2018 and resigned his position effective March 31, 2011
 
Ndugu Chakunyuma, hii PhD ya Malecela ya 1977 HAINA THESIS! Honoris Causa ni SHAHADA ya HESHIMA! Na kawaida yake MTU HAPASWI kujiita ama kuandika PhD baada ya jina lake. Hivyo Cigweimis kama haitumii anafanya jambo lililo jema. Hawa wengine (Kama Kikwete, Lwakatare, Mkapa, nk) hawajui matumizi yake.
 
Hivi ni kwa nini hapa nchini kwetu (TZ) huwa ni muhimu sana au tuna mazoea ya kumuita mtu mwenye PhD, Dr. fulani au Prof. fulani kama vile Dr.Magufuli, Dr.Slaa au Dr.Kikwete, Dr.Lamwai au Prof. Muhongo au sijui Prof.Kapuya au Prof.Magembe n.k?
Mbona nchi nyingine hasa za Wazungu hakuna hayo mambo?
Kwa mfano Raisi wa Marekani Baraka Obama ni prof. lkn sijawahi kusikia hata siku moja Mtu akisema Prof. Obama kwanza wanasiasa wengi sana wa Ulaya na Marekani wana PhD lkn sijawahi kusikia Mtu akiwaita Dr.!

Kwa Wazungu au Nchi za Ulaya na Marekani Mtu ataitwa kwa kutumia Dr. au Prof. pale tu anapokuwa yuko kwenye mambo ya kielimu, kwa mfano Raisi Baraka Obama akienda Chuo kikuu cha Harvard basi watamuita Prof.Obama lkn sio mitaani kama hapa kwetu, utakuta hata mitaani kama mtu ana PhD ukimuita bila ya kuweka hilo Dr. ni ugomvi sasa ni kwa nini?
 
Hao ma Prof , Dr., Hon. Ni wanasiasa wenye dhambi za kitaifa!
 
Unachotaka kusema nini unaonekana mambo ya hapa duniani hujui kabisa pengine tukusaidie hebu sema unachotaka ni nini hasa?
 
Hivi ni kwa nini hapa nchini kwetu (TZ) huwa ni muhimu sana au tuna mazoea ya kumuita mtu mwenye PhD, Dr. fulani au Prof. fulani kama vile Dr.Magufuli, Dr.Slaa au Dr.Kikwete, Dr.Lamwai au Prof. Muhongo au sijui Prof.Kapuya au Prof.Magembe n.k?
Mbona nchi nyingine hasa za Wazungu hakuna hayo mambo?
Kwa mfano Raisi wa Marekani Baraka Obama ni prof. lkn sijawahi kusikia hata siku moja Mtu akisema Prof. Obama kwanza wanasiasa wengi sana wa Ulaya na Marekani wana PhD lkn sijawahi kusikia Mtu akiwaita Dr.!

Kwa Wazungu au Nchi za Ulaya na Marekani Mtu ataitwa kwa kutumia Dr. au Prof. pale tu anapokuwa yuko kwenye mambo ya kielimu, kwa mfano Raisi Baraka Obama akienda Chuo kikuu cha Harvard basi watamuita Prof.Obama lkn sio mitaani kama hapa kwetu, utakuta hata mitaani kama mtu ana PhD ukimuita bila ya kuweka hilo Dr. ni ugomvi sasa ni kwa nini?
Unaonekana hujui kitu sijui usaidiweje mkuu.
 
Huyu jamaa si ndo aliomba serikali ipige marufuku ulaji wa igali??
 
NI kweli Mkuu. Ukweli ni kwamba huko ulaya na Marekani hata wakiwa katika mazingira ya vyuo hawahusudu hizi title, utakuta maprofessor wanataka waitwe tu kwa majina yao ya kwanza. KUna watu kule wanakasirika ukiwaita Prof., lakini huku kwetu Prof linakuwa jina la mtu, watu wanalikubali bila hata kutaja Prof na jina lake halisi. Unakuta mtu anasema, "naomba kukuona Prof", na jamaa anakubali kuitwa hivyo.

Tatizo hapa kwetu ni malimbukeni wa title. Watu wanaona ujiko sana kuwa na hutu tu-degree walitotupata kwa shida sana, na ndio maana wanataka kutukuzwa na hizi title wakati hawana lolote la maana wanalochangia katika maendeleo ya nchi na jamii.
 
Waafrika wanapenda kukwezwa. Mkishindwa kuwakweza, wanajikweza wenyewe.
 
Mkuu pamoja na maswali yako unayo yahoji ila mimi nataka uzitendee haki PhD za watu hapa kati ya wote uliowaorodhesha hapo kuna mmoja hastahili kutumika kama mfano ktk bandiko lako kwasababu hakuna chuo chochote kilichobainishwa kamba alisoma nakupata hiyo PhD hivyo tafadhari kwaheshima ya PhD za watu unatakiwa kumwondoa haraka hapo

Sikazi yangu kubainisha ni nani bali hata matendo yake hubainisha elimu ndogo Aliyonayo na tayari kesha shindwa kuongoza nchi ipoipo tu inajiendea kanakwamba haina kiongozi.

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom