Viongozi wetu na 'title' bandia

Viongozi wetu na 'title' bandia

Unyonge wa moyo , kutojiamini , kasumba , kukosa ufahamu.
Kwa mtu anaejiamini na kujitambua hasumbuliwi na vyeo / title za kidunia.

Naona upo sahihi lakini maswali ya kujiuliza 1.kujiona mnyonge zidi ya nani? 2.kasumba yaani hata baada ya miaka 50 ya uhuru bado tunakasumba? 3. Je Kutojiamini kutaweza kumletea mwananchi maendeleo? Ningeshauri viongozi kuwa wakweli na wawazi ingetusaidia sana kama taifa. Hivi vititle ambavyo ukifuatilia unakuta havina tija yoyote kwa taifa ni aibu tupu.
 
Tujikumbushe pia kwa viongozi wengine kama:

1. Dr. Madeleine Albright (Title yake Dr. haikuwahi kutumika katika kipindi chake chote alipokuwa Secretary of State, alipata PhD yake mwaka 1975) Reference: Madeleine Albright - Wikipedia, the free encyclopedia and Michael and Virginia Mortara Distinguished Professor in the Practice of Diplomacy - Mortara Center for International Studies - Georgetown University

2. Prof. Dr. Condoleezza Rice ( Title yake ya Professor haikuwahi kutumika popote kipindi chote alipokuwa Secretary of State, hta hivyo Dr. ilitumika muda wote) Reference: Condoleezza Rice - FSI Stanford and Condoleezza Rice - Wikipedia, the free encyclopedia

3. Dr. Bill Clinton (Title yake ya Dr.(Juris Doctor in Law) haiukuwahi na hata sasa bado haitumiki)

Kitu kingine cha kujifunza, wenzetu wenye taaluma wakimaliza muda wao kutumika kwenye siasa wanarudi kwenye taaluma zao kufanya kazi.
 
Nashukuru kwa kuadd kwenye hii list mkuu, naamini kama wataipitia hii thread watabadilika. Kama ulivyosema wataalamu wakimaliza muda wa vyeo vyao vya kisiasa wanarudi kwenye taaluma zao hapa kwetu wanang'ang'ania siasa mpaka wanazeekea humohumo wanaogopa hawawezi kucompete kwenye soko la ajira ndio maana wapo radhi kutetea ujinga ilimradi anabaki kwenye nafasi yake. TUBADILIKE tuwe wawazi na wakweli na tujiamini kwa vipaji/abilities tulizonazo.
 
Mkuu Malipesa unamaanisha nini hebu dadavua zaidi.
 
Mkuu Ngereja kumbe Bill Clinton phd holder? I see wenzetu wako makini sana sijawahi kumsikia akijiita Dr. Clinton
 
Ukimuuliza Phd yako imetusaidiaje wananchi na taifa kwa ujumla hana jibu, unajiuliza sasa hizi mbwembwe za kujipachika mititle inatoka wapi?
 
Mwanamama Condoleezza Rice pia ana Ph.D, lakini ni mara nadra sana kumsikia akijitambulisha kwa udokta wake. Sijajua sie waswahili kwa nini tunashoboka sana na tu-Ph.D 'twetu'
 
Unapokuwa na takribani watu mil 45 - ktk East Africa unaongoza kwa illiteracy rate, unategemea nn?
 
Mwanamama Condoleezza Rice pia ana Ph.D, lakini ni mara nadra sana kumsikia akijitambulisha kwa udokta wake. Sijajua sie waswahili kwa nini tunashoboka sana na tu-Ph.D 'twetu'
Ka-PhD na wewe unako???
 
Ka-PhD na wewe unako???

Mi sina ninaweza pata siku za usoni Mungu akinijalia lakini hapa tunajadili umuhimu wa viongozi wetu kuwa wa wazi na wakweli hii itasaidia sana kukuza uzalendo kwamba una Phd ya nuclear physics basi tueleze umuhimu wake kwa nchi yaani kama taifa tumenufaika vipi na thesis yako sio kuishia kuitwa docta au profesa tu hii haitoshi tunataka tuone impact ya elimu yako kwa jamii.
 
Unapokuwa na takribani watu mil 45 - ktk East Africa unaongoza kwa illiteracy rate, unategemea nn?

Inasikitisha! Kwakweli eti tunajivunia kuenroll watoto kwa 97% lakini watamaliza wangapi na wataelimika kujua kusoma na kuandika kuhesabu wangapi hilo hatujali.
 
Ona Zuma hafichi kitu.

Zuma was born in Nkandla, Zululand (now part of KwaZulu-Natal). His father was a policeman who died when Zuma was still a young iboy, and his mother a domestic worker.
He received no formal schooling.
As a child, he was constantly moving between Zululand and the suburbs of Durban in the area of Umkhumbane (near Chesterville). He has two brothers, Michael and Joseph.
Sasa viongozi wetu wana nini kwa nini sio wa wazi na sio wakweli wanafanya hivyo kwa faida ya nani?
Pia ana wake watatu na anawaweka hadharani. Ana kimada huko Mbabane Swaziland nacho kakiweka hadhani watu wanajua. Aliwahi kufanya ngono zembe na mfanyakazi wa ndani aliyekuwa na mambukizi ya ukimwi na baada ya tendo akaenda akanawa na hakupa ukimwi; hili pia aliliweka wazi mbele ya mahakama. Si ajabu kuweka wazi hilo la kukosa formal education! Hapa kwetu kiongozi gani anaweza kuwa muwazi kiasi hicho. At least mmoja amewahi kuwa muwazi kidogo kuhusu mahusiano.
 
Injinia fulani, dakta fulani, juma nkamia alikuwa mtangazaji wa radio sasa aitwe mtangazaji nkamia.
 
Pia ana wake watatu na anawaweka hadharani. Ana kimada huko Mbabane Swaziland nacho kakiweka hadhani watu wanajua. Aliwahi kufanya ngono zembe na mfanyakazi wa ndani aliyekuwa na mambukizi ya ukimwi na baada ya tendo akaenda akanawa na hakupa ukimwi; hili pia aliliweka wazi mbele ya mahakama. Si ajabu kuweka wazi hilo la kukosa formal education! Hapa kwetu kiongozi gani anaweza kuwa muwazi kiasi hicho. At least mmoja amewahi kuwa muwazi kidogo kuhusu mahusiano.
Hapa kwetu hakuna wote wanataka tuwaone wasafi lakini mambo yao wanafanya chini kwa chini na ndio maana tunaendelea taratibu mno kutokana na usiri huu. Yaani mtu ni incompetent lakini kwa sababu kaficha basi wananchi hatujui tunastuka tumeshamchagua. sijui dawa ya haya ni nini? Yaani watz tufanye nini ili viongozi wetu wawe wa wazi na wakweli.
 
Du! nami nitaitwa prof. Mcheza karate kuanzia leo. Kumbe unajiita tu hata zile ulizopewa kwa ukarimu ulipowatembelea RUKO, TEKU, SEKUKO, st. JOHN nk. Aaaaa hii nchi hadi kichefuchefu.
 
Du! nami nitaitwa prof. Mcheza karate kuanzia leo. Kumbe unajiita tu hata zile ulizopewa kwa ukarimu ulipowatembelea RUKO, TEKU, SEKUKO, st. JOHN nk. Aaaaa hii nchi hadi kichefuchefu.
Huko marekani uprofessor ni wa chuo kikuu hakuna uprofessor kwenye siasa. kama wewe ni professor wa chuo ikiwa mwanasiasa inaachana na title ya u professor kama akina Obama na Rice. Hapa kwetu mganga wa kienyeji anatumia jina prof. anatinga bungeni na bado anaonekana kuwa addressed kama professor! Ma dr. fake wanajulikana lakini bado wanaitwa ma dr katika taarifa rasmi za bunge na serikali!

Najua ID yangu nikiongeza Prof. litapendeza sana yaani kuanzi sasa nami niitwe Prof. Kimbunga. Kama wewe mkuu kisha nione nani ataniuliza.
 
Wajua,hawa wa kwetu,si kwamba wanawakoga wapiga kura? Wanataka wajitutumue kuwa wako kamili kwa kupata madaraka... Sidhani kama inferiority complex ni the right word.. Imagine watu wanaogombea uongozi hadi wanaenda kwa Kalumanzila,na kule Bagamoyo.. Ni watu wasiojiamini.. Kiufupi huo ni mtazamo wangu..
 
Naamini hata wao huwa wanatucheka sana wanapotutembelea au wasomi wetu wanapozuru kwenye nchi zao.Wanatuona majuha tu.matitle makubwa lakini hamna kitu.Huku hadi balozi ni title.(Balozi Seif Iddy).Huyo mwenye PHD ya nuclear physics anaitumia elimu yake kugawa kadi za chama Mtwara huku kozi ya Nuclear physics Udom(mdogo wangu shahidi)wanasoma kwa mtindo maarufu kama "extreme".Yani ile mnapigwa kozi nzima kwa wiki mbili na "mtaalam"kutoka out!
 
Back
Top Bottom