Viongozi wetu na 'title' bandia

DR. J.M Kikwete, DR G.Bilal, Eng. Stella Manyanya, DR Asharose Migiro, DR Mary Nagu, Eng. C. Chyzya, Prof. Maji Marefu, DR Shukuru Kawambwa, Prof I. Lipumba, DR. W.Slaa, Pof. Mark Mwanosya, DR. Hussein Mwinyi, Prof. Jumanne Maghembe, DR H. Mwakyembe.
Hyo ni THELUTHI ya orodha ya viongozi wetu. Ndo hvyo, elimu tittle, but how it helped us. GOD KNOWS
 
Huko marekani uprofessor ni wa chuo kikuu hakuna uprofessor kwenye siasa. kama wewe ni professor wa chuo ikiwa mwanasiasa inaachana na title ya u professor kama akina Obama na Rice. Hapa kwetu mganga wa kienyeji anatumia jina prof. anatinga bungeni na bado anaonekana kuwa addressed kama professor! Ma dr. fake wanajulikana lakini bado wanaitwa ma dr katika taarifa rasmi za bunge na serikali! Najua ID yangu nikiongeza Prof. litapendeza sana yaani kuanzi sasa nami niitwe Prof. Kimbunga. Kama wewe mkuu kisha nione nani ataniuliza.
Jamani tunashindwa kuwa serious hata kidogo inajulikana huu uprofesa wakujipa lakini bungeni anaitwa hivyo hivyo ajabu kabisa.
 
DR. J.M Kikwete, DR G.Bilal, Eng. Stella Manyanya, DR Asharose Migiro, DR Mary Nagu, Eng. C. Chyzya, Prof. Maji Marefu, DR Shukuru Kawambwa, Prof I. Lipumba, DR. W.Slaa, Pof. Mark Mwanosya, DR. Hussein Mwinyi, Prof. Jumanne Maghembe, DR H. Mwakyembe.Hyo ni THELUTHI ya orodha ya viongozi wetu. Ndo hvyo, elimu tittle, but how it helped us. GOD KNOWS
Umesahau dr. dr E Nchimbi.Labda tungekuwa tunawauliza kwenye mikutano ya kampeni, warsha. makongamano na vikaoni wateleze phd/thesis zao zimetusaidiaje kama taifa.
 
Tupo ndani ya mfumo wa usanii, kwa hiyo hizo title ni za kisanii zaidi. Nakumbuka wakati tunaelekea uchaguzi mkuu 2010 mgombea mmoja alitunukiwa PHD 2 za fasta fasta ili kukidhi mahitaji ya wakati huo.

Pia vyombo vya habari vikaelezwa kuitaja hiyo title yaani Dr, katika kila wanchoongelea kumhusu.

Ukiangalia hazina tija, Dr, professor everywhere lakini matendo hayaendani na title zenyewe. Shame on Them.
Pia nilimuona lady wa kwanza wa nchi akisema "serikali ya dr dr dr dr........ ina nia njema ya kuleta maendeleo"
Nikajisemea duh tuna kazi kwelikweli kuijenga jamii ya kizalendo.
 
Umesahau dr. dr E Nchimbi.Labda tungekuwa tunawauliza kwenye mikutano ya kampeni, warsha. makongamano na vikaoni wateleze phd/thesis zao zimetusaidiaje kama taifa.

Itasaidia sana sana. Pengine iwekwe sheria km ile ya kutangaza mali zao, basi waniike hadharani elimu zao, na wamezipataje, na waeleze wataifanyai nini Tanzania kupitia elimu zao.
 
huku hata kacheo ka kupewa mtu anakakomaliaaa usipokataja inakuwa nongwa!
 
Ni kweli hata mie naunga mkono kuwa wanataka kuwa "juu". Ndugu Bill Mwalimu Nyerere Alitunukiwa kuwa PROFESA na Chuo Kikuu Dar lakini alikataa kwa kusema: Nanukuu: "Neno Profesa asili yake ni Kifaransa, likimaanisha Mwalimu. Nyie (Watanzania) Mnaniita Mwalimu, kwa hiyo sijaukataa uprofesa wenu ila labda tu kuwa tofauti ya lugha". Hii ilikuwa kati ukumbi wa ATB pale Mlimani, mwezi Desemba 1997. Mie nilikuwa ndani ya ukumbi!
Hawa dawa yao moja tu: KuTOTUMIA title hizi TUNAPOWA adress!
 
Nashukuru kwa kutuharisha historia ujue Mwalimu alikuwa makini sana na matendo yake anastahili kuenziwa.
 
Itasaidia sana sana. Pengine iwekwe sheria km ile ya kutangaza mali zao, basi waniike hadharani elimu zao, na wamezipataje, na waeleze wataifanyai nini Tanzania kupitia elimu zao.

Nakuunga mkono majina ya kiacademic yaheshimiwe na yasitumiwe kiholela. Otherwise kuwe na sheria ya kukataza vijititle kwa viongozi.
 
Nakuunga mkono majina ya kiacademic yaheshimiwe na yasitumiwe kiholela. Otherwise kuwe na sheria ya kukataza vijititle kwa viongozi.

Haswaaa. Maana wamezidi Udr mwingine wanapeana bar, alafu wanatuletea sisi. Ijulikane km no dr umeipataje na je inakustahili?
Maana wamezidi.
Na kwani ukiitwa tu jina lako hata km una cheo, na umesoma sana utapungua nini?
 
DR. J.M Kikwete, DR G.Bilal, Eng. Stella Manyanya, DR Asharose Migiro, DR Mary Nagu, Eng. C. Chyzya, Prof. Maji Marefu, DR Shukuru Kawambwa, Prof I. Lipumba, DR. W.Slaa, Pof. Mark Mwanosya, DR. Hussein Mwinyi, Prof. Jumanne Maghembe, DR H. Mwakyembe.
Hyo ni THELUTHI ya orodha ya viongozi wetu. Ndo hvyo, elimu tittle, but how it helped us. GOD KNOWS

Kazi tunayo, ukiangalia wengi wao ni brain at rest.
 
Nadhani kabla ya 2015 tutakuwa na Dr. Wasira na Dr. Riz 1Just wait and see
 
Utasikia mtu anaitwa luteni, kanali, jenerali, meja jenerali ukitafakari uluteni, ukanali, ujenerali wake umelisaidiaje taifa haupati jibu. Kumbe lengo ni kogo/uspoon tu basi. TUBADILIKE jamani ukishalitumikia jeshi letu baki na jina lako la kawaida kama Chakunyuma sio luteni mstaafu Chakunyuma hiyo itabaki kuwa CV yako milele. Mbona wenzetu wanaweza sisi tunashindwaje? Angalia JFK, GW Bush, Ian Khama, J McCain walikuwa wanajeshi lakini hawana kogo za kujiita majenerali wastaafu.
 
Haswaaa. Maana wamezidi Udr mwingine wanapeana bar, alafu wanatuletea sisi. Ijulikane km no dr umeipataje na je inakustahili?
Maana wamezidi.
Na kwani ukiitwa tu jina lako hata km una cheo, na umesoma sana utapungua nini?
Afadhali basi uwe na udr. wa ukweli ina maana kidogo! kuliko huu wa kuchakachua. Bwana atusaidie sana sisi wananchi kwa sababu tukisikia dr. tu tunapagawa bia kujiuliza udr. huu ameupataje? na unatusaidia nini katika maisha yetu ya kila siku. Bwana aturehemu.
 
Kazi tunayo, ukiangalia wengi wao ni brain at rest.

Tunaweza kuprove uhalali wa phd zao kama watajitetea umuhimu wa thesis zao kwa taifa na wananchi kwa ujumla. Tuweke sheria ya kutotumia academic titles hovyo ili kulinda heshima ya taaluma yetu.
 
Nashukuru kwa kuadd kwenye hii list mkuu, naamini kama wataipitia hii thread watabadilika. Kama ulivyosema wataalamu wakimaliza muda wa vyeo vyao vya kisiasa wanarudi kwenye taaluma zao hapa kwetu wanang'ang'ania siasa mpaka wanazeekea humohumo wanaogopa hawawezi kucompete kwenye soko la ajira ndio maana wapo radhi kutetea ujinga ilimradi anabaki kwenye nafasi yake. TUBADILIKE tuwe wawazi na wakweli na tujiamini kwa vipaji/abilities tulizonazo.
Ahhahhh ndiyo maana akina kingunge, malecela wanang'ang'ania siasa tu hawana kingine cha kufanya? ivi huyu malecela nae ni dr. na kama ni dr. mbona sionagi hiyo taito kwenye jina lake au ni wale wasiosoma kabisa?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom