Viongozi wetu hawataki wahalifu watetewe na mawakili, je ni utawala wa sheria?

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Nimekuwa nafuatilia masuala ya sheria hapa nchini. Nimewahi kusikia kiongozi mmoja akisema kuwa hategemei kusikia mawakili watawatetea watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Paulo Makonda wakati akiongea na wanasheria wa kujitolea aliwashukuru sana kusema kuwa Serikali hii inataka kutetea wanyonge na hatarajia wahalifu watatetewa.

Najiuliza utetezi huwa wa upande mmoja? Mbona serikali hii katika kesi za mauaji inatoa mawakili hata upande wa muuaji? Wakati muuaji katenda kosa la kutoa uhai wa mtu? Nadhani viongozi wetu kutetea mharifu lipo kisheria tusilete siasa kwenye haki ya mtu.
 
Hata mimi nashangaa sana kwani kumkamata mtu ndiyo imethibitika kuwa katenda kosa, so ina maana mahakama ibague makosa, only in Tanzania,,,,,,,,,,,,,,,
 
Mawakili wa serikali ni dhaifu, we tazama jinsi LISSU anavyocheza na akili zao. Anacheza nazo kama apendavyo yeye.
 
Hakuna mwanasiasa atakayeuona ufalme wa mumgu ingawa mashehe na maasofu watawaombea sana. A government is an instrument of oppression...... Sasa how do you enter the kingdom of god while you chair the council of oppression!
 
Back
Top Bottom